Hivi, wewe ni Mwili wako au Roho yako?⁣⁣⁣⁣

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
340
300
Kuna nyakati tunakuwa na vita vikali sana na miili yetu kiasi kwamba tunajichukia na kujikinai wenyewe.⁣⁣

Mara nyingi nyakati hizi huja pale ambapo tunapo jaribu kubadili tabia hasa kutoka tabia hasi kwenda chanya na kushindwa.⁣⁣

Kutokana na kushindwa kwetu tuna uhukumu mwili na kuutoa thamani kabisa matokeo yake ni kuuchuki mwili wako bila sababu.⁣⁣

Nyakati nyingine tunatoa adhabu kali dhidi ya miili yetu na kudhani wenyewe ndio chanzo cha wewe kubadili tabia au maisha yako unayoyaishi.⁣⁣

Hapo tunakuwa tumesahau ya kwamba kwamba utu wako wa ndani ndio wenye matatizo na mwili ni chombo tuu ambacho hupokea na kufanyia kazi yale yaliyoko ndani yako. Kwa lugha ya Bibilia mwili umeitwa hekalu.⁣⁣
⁣⁣
Maandiko ya Bwana yanasema;⁣⁣
⁣⁣
"Je, hamjui kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Nyinyi basi, si mali yenu wenyewe. Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu."⁣⁣
⁣⁣
1 Wakorintho 6:19-20⁣⁣
⁣⁣
Mwandishi Erck heart Toll kutoka kwenye kitabu chake cha The Power of now Ukrasa 122 anasema;⁣⁣
⁣⁣
"Usipigane na mwili, kwani kwa kufanya hivyo unapigana dhidi ya ukweli wako mwenyewe. ⁣

Wewe ni mwili wako.⁣⁣ Mwili ambao unaweza kuona na kugusa ni pazia nyembamba tu la uwongo. Chini yake kuna mwili wa ndani usioonekana, mlango wa kuwa Kiumbe, kwenye Uzima Usiofunuliwa.
⁣⁣
Kupitia mwili wa ndani, umeunganishwa bila kutenganishwa na Maisha haya yasiyodhihirishwa bila kuzaa, yasiyokufa, ya milele.
⁣⁣
Kupitia mwili wa ndani, wewe ni mmoja milele na Mungu."⁣⁣
 
Kitu cha ajabu ni kwamba, kila kiumbe chenye mwili ana mwili wake mwingine wa ulimwengu wa kiroho, yaani kiumbe kinacheza sehemu mbili, ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa kiroho.

Ajabu sana!
 
Kitu cha ajabu ni kwamba, kila kiumbe chenye mwili ana mwili wake mwingine wa ulimwengu wa kiroho, yaani kiumbe kinacheza sehemu mbili, ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa kiroho.

Ajabu sana!
Yes kuna siri kubwa sana katika hili.
 
Kitu cha ajabu ni kwamba, kila kiumbe chenye mwili ana mwili wake mwingine wa ulimwengu wa kiroho, yaani kiumbe kinacheza sehemu mbili, ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa kiroho.

Ajabu sana!

Mwanadamu jinsi alivyo, as far as UHAI is concerned, hana tofauti na mnyama yoyote yule. Mwili, roho, nafsi, akili, nia, ni power ya ziada aliyo nayo mwanadamu kiufahamu kwa Mungu na mazingira yake. Lakini haya yote ni unity -- one thing -- no separation! Simply put, there is no such thing as roho kama roho; hakuna separate entity inayoitwa roho kwa mwanadamu. TOTAL ama WHOLE mwanadamu with respect to God, anatajwa kuwa ana roho ama ni roho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom