Je, Binadamu ameshaenda umbali upi chini ya ardhi?

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,812
Wakuu habari za jioni..
Kumekuwa na makala mbalimbali zinaozo elezea umbali ambao wanasayansi wameshafikia angani. Wameweza safiri mpaka kwenye mwezi na wameweza tuma vyombo vya uchunguzi katika anga kujua sayari nyingine na umbali wake.

Je Binadamu ameshakwenda umbali gani chini ya ardhi kwa rekodi zilizopo? Je binadamu wameshasafiri kwa umbali upi kwenda chini na wamegundua kitu gani chini ya ardhi ya sayari yetu katika kudrill. Ama kuchimba?
Nawasilisha kwa wataalam wa Elimu ya miamba..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa somo la Geografia nililosoma, sehemu ya mwisho ya ardhi, dunia inaitwa inner core, inajoto sana hadi udongo unachemka kama uji, ukitoka nje inajulikana kama volkano, ndivo nilivoelewa kwa uelewa wangu , kuhusu kufika chini ya arthi sinauhakika kama kunamtu alishafanikiwa kufanya hivo nakurudi salama.
 
12km, huko kola penisula ya urusi, miaka ya 70s na ilichukua zaid ya miaka 10 kufikia urefu huo,

lengo lao ni kuchimba mpk wapite earth crust yote, wakachimba walipofikia mita 12,262 walipogundua ndio kwanza wapo robo ya program yao wakafungasha ma mashine zao wakafa.

kumbuka hapa zilizofikia urefu huo ni mashine sio watu, urefu mkubwa kbsa uliofikiwa na binadam ni 2.2km huko georgia, na walishindwa kutokana na joto kali,

kumbk: kila km 1 kwenda chini temp inaongezeka kwa zaid ya asilimia 15, sbb ni nini? Refer to state of thermodynamic equlibrium che&phyz advance level.

hapa napo walipooona joto linawatesa hawakutaka shida na ntoto ya ntu wakafungasha sululu zao wakarudi wakakufa.

Haya njoo futuhi land sasa!!!! Kisima tuuu kikichimbwa yakaanza ktoka maji, njemba zinaacha utasikia nimechimba mpk nimekuta maji, pasipokujua sio yy amekuta maji ila maji ndio yamemkuta yeye.

kaburi nalo likichimba ukikutana na mwamba mtu anatoka half anaanza kusingiziwa marehemuu,
oooh sijui marehemu hakutaka azikwe hapa , mara ooh marehemu hataki kuzikwa leo, mara ohhh marehemu amekasirika, yaani futuhi land kumsingizia marehemu ni jambo dogo sana, ka stail hii hata malaika wataishia kwa wenzetu tuu, au pengine huu ndio uzao wa yuda!
ukija kuangalia huo wote ni uvivuuu.
 
Amini tu mkuu kwamba watu wamefikia mwisho kabisa ya ardhi huku ambako ndio sehemu isiyotakiwa kufikwa baada binamu ni watundu sana
 
Mkuu wanasayansi wameweza kugundua vifaa ambavyo vinahimili joto kwa kiasi kikubwa sana.
Je wameshindwa kugundua kifaa kinachoweza kuhimili joto la magma na kutupa taarifa za mwisho kabisa kwenye kina cha ardhi..?
Je sayansi yetu binadamu ya kijiographia imefikia ukomo?
Kwa somo la Geografia nililosoma, sehemu ya mwisho ya ardhi, dunia inaitwa inner core, inajoto sana hadi udongo unachemka kama uji, ukitoka nje inajulikana kama volkano, ndivo nilivoelewa kwa uelewa wangu , kuhusu kufika chini ya arthi sinauhakika kama kunamtu alishafanikiwa kufanya hivo nakurudi salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom