Je benki zinatuibia?

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Hili ni swali kwa wafanyakazi, wataalamu na weledi wa shughuli za kibenki.



Bazazi ni mwanachama (sio mwanahisa) ktk benki ya benki mojawapo hapo Tanzania kwa kitambo sasa. Mwezi uliopita yaani 12/2008, Bazazi amefahamu kitu ambacho kwa muda wote huo alikuwa hakifahamu kuhusu mabenki. Alichokifahamu ni gharama au ada anazolipa kwa kuhifadhi vijisenti vyake huko. Gharama anazolipa Bazazi ni za aina tatu kwa mchanganuo ufuatao;
-ATM service charge TAS 350/- kwa kila atumiapo huduma hiyo.
-Monthly service charge TAS 400/-
-Annual card fee 5000/-.

Kwa maelezo hayo BAzazi anaomba kufahamishwa haya;
-Je ni halali yeye kulipa ada hizo?
-Hela wanazopata benki kutokana na kukopesha pesa yake bila ridhaa yake inafanya kazi gani?
-Je wazungu walioanzisha utaratibu wa benki nao wanalipa ada hizo?
-Je huko sio kuwaibia wateja hasa ukizingatia kuwa Bazazi analipa ada isiyopungua TAS 15200/- kwa mwaka.

Bazazi anategemea majibu MUJARABU na wala sio kashfa na matusi.


Bazazi anatanguliza shukurani zake za dhati.
 
Bank zote ni jizi kimsingi hasa ukilinganisha na hali ya uchumi wa watanzania. nyingine hazina interest. Na zinaoperate kama zinachuma fedha za watanzania bila uchungu. Waliouwa benki za taifa were deadly infected in their mind. Angalia hata NMB ilivyochoka ili tu wapeane kama walivyopeana makampuni ya umma. This is pathetic.
 
Hili ni swali kwa wafanyakazi, wataalamu na weledi wa shughuli za kibenki.

-ATM service charge TAS 350/- kwa kila atumiapo huduma hiyo.
-Monthly service charge TAS 400/-
-Annual card fee 5000/-.

Kwa maelezo hayo BAzazi anaomba kufahamishwa haya;
-Je ni halali yeye kulipa ada hizo?
-Hela wanazopata benki kutokana na kukopesha pesa yake bila ridhaa yake inafanya kazi gani?
-Je wazungu walioanzisha utaratibu wa benki nao wanalipa ada hizo?
-Je huko sio kuwaibia wateja hasa ukizingatia kuwa Bazazi analipa ada isiyopungua TAS 15200/- kwa mwaka.
Mimi nadhani ni halali, ingawa inaweza kuwa ghali ukilinganisha na kwingineko duniani- dukuduku zote ulizotoa unakuwa unafahamishwa kabla ya kujiunga, hivyo unapokubali kwa hiari yako kuwa mwanachama wa benki au kutumia huduma fulani unakuwa umependa mwenyewe. Ushauri, usipende kutumia sana ATM card yako, jua matumizi yako kwa mwezi, basi unakuwa na hela ndani kwa ajili hiyo- ikitokea emergency iwe mara moja, mbili kwa mwezi, hivyo utajikuta unatumia wastani wa TZS 6500/- kwa mwezi badala ya 15200/-.
 
Hawaibi cho chote kwa maana ya neno mkataba, ila kweli gharama za huduma hizo zaweza kuwa juu. Tunasema ziko juu dhidi ya nchi gani? La pili ni suala la gharama za uendeshaji wa benki yenyewe, mfano mishahara,matangazo,miundombinu ya benki,kuchangia maendeleo ya jamii na burudani kama NMB wanavyogawa pesa kwa Kili Boys, kaa ukijua kuwa benki hawana shamba,shamba lao ni wewe. Lazima uvunwe.

Ukisikia nbc wametoa fedha kuchangia vitabu kule Kibondo ujue ndo vi-service charge vyako na vyangu. Naamu pesa wanayopata baada ya kukopesha watu hela ulizopeleka wewe kwao ndo huwa wanagawana(wenye benki) na kiduchu ndo wanatangaza kuwa mwaka huu sisi tumepata faida Sh kadhaa.

Nimechangia kidogo mzee.
 
Wizi mtupu kuna,kama sijabank via tellers for six month but only using TAM iyo monthly service charge ni ya nini?
 
For the last six month nimekuwa natumia ATM thus not using tellers as niko bize.
Sasa apo monthly service charge inakatwa kwa ajili ya nini wakati via ATM daily wanalamba
 
Sijaelewa hapo aliposema unakatwa Annual card fee 5000, unamaanisha kila mwezi au?

je kuna anayefahamu interest za hizi bank zatu ktk aina mbalimbali ya account zao walizonazo? ningependa kujua ipi ina interest zaidi ya ipi.

Asanteni
 
unatakiwa kabla ya kufungua account uhulize wakupe masharti ya uendeshaji wa account zao kwani kuna nyingine hazina makato kabisa wakati nyingine zinakatwa sana. it depends na unataka kuoperate account ya aina gani.

ukifungua account bila kuhuliza kwa sheria za benki ni kwamba umekubaliana na masharti ya account uliyofungua, na kutokana na contract of sale/purchase consideration inaweza kuwa ni kubwa sana provided mmekubaliana hakuna tatizo.
 
Jibu ni Hapana. Benki haikuibi. Wewe uliingia nao mkataba kwa kuchukua fomu na kuzijaza na kusema unakubaliana na masharti yao ikiwa ni pamoja na hizo garama zakuendesha akaunti yako. Pia ulikubaliana na kiwango cha riba utakayopata kutokana na kuhifadhi pesa zako nao. Kwa vile ni mkataba ulioridhia mwenyewe hapa sioni utaulizaje kama unaibiwa. Yawezekana uliingia huo mkataba bila kuusoma na/au bila kuuelewa vizuri. Nasema hivyo kutokana na unavyosema umeshtushwa kujua karibuni kuhusu hizo garama. Hapo bado kutokujua kwako hakufanyi uwe ni wizi.

Nadhani Swali ni je mkataba huo unamanufaa kwako ukilinganisha na kutumia pesa zako katika shughuli nyingine au kuzihifadhi chini ya godoro? Hapo utapima faida ya kuitumia hio pesa katika shughuli nyingine (mfano biashara). Je itakulipa zaidi kuliko kuziweka benki chini ya mkataba wa sasa? Ikiwa unaona inalipa kuzitumia vinginevyo basi huna haja kuziweka benki. Natumaini ulifikia uamuzi wa kuweka pesa yako benki baada ya kupima faida na hasara za kutokufanya hivyo. kwa hiyo wewe wajua kama mkataba huo wa kuweka pesa na benki ni wamanufaa kwako au la. kama hujafanya hivyo nakushauri ufanye mara moja. Wengi wetu tunaingia mikataba na mambenki kama mazoea tu. kwamba ukiwa na pesa basi lazima ziende benki. Inatakiwa tujue tunapata faida gani kwa kuziweka pesa benki na nini tunapoteza kwa uamuzi huo. Inabidi maamuzi yetu yawe kutaka kuongeza faida. La sivyo hatutakuwa na tofauti na mtu mwenye Ng'ombe wengi lakini anaishi maisha duni. Inabidi pesa ifanye kazi izalishe kwa ajili yako. Je benki inazalisha zaidi?

Swala la pili ni kwamba benki ni biashara kama ilivyo biashara nyingine. Nia yao kubwa na ya kwanza ni kutengeneza faida. Kusaidia jamii na mambo mengine kama hayo huchukua nafasi ya pili au ya tatu. Kazi kubwa ya benki ni kuuza pesa na hufanya hivyo kwa faida. Wewe unataka Shilingi Mbili watakupa chini ya mkataba kwamba utakapolita utalipa shilingi mbili na thumni. Hivyo Benki yoyote ile duniani inajiendesha hivyo kwa kutengeneza faida kwa kuuza pesa. Ila pia garama za uendeshaji wa akaunti yako ni chanzo kimojawapo cha mapato kwao. Kila benki inaviwango vyake kutokana na huduma wanayotoa kwa wateja wao. Swala hapa si lazima kuweka pesa kwa mhudumu ndio kulipia garama za uendeshaji wa akaunti yako. Kuna mambo ya kuweka takwimu zako salama, kuhakikisha unapata pesa yako unapoitaka na mengine mengi ambayo hata kama hautaweka pesa kwa mhudumu bado hizo garama za kuiendesha akaunti yako zipo pale pale.

Naamini tukianza kuangalia kuweka pesa benki kama biashara, basi tutatafuta benki ambayo itatupa faida kubwa zaidi kwa pesa zetu. Na kama tukipima na kuona faida za kuitaumia hio pesa kwa shughuli nyingine ni bora zaidi, basi tufanye maamuzi hayo.

Benki haikuibi kwani hayo ndio makubaliano yenu. Kama unaona sasa mkataba huo unakula kwako, zunguka tafuta benki nyingine ambayo wote (wewe na benki) mtafikia makubaliano ambayo yatakuwa ya manufaa kwako. Kikubwa safari hii usome na kuuelewa mkataba wanaokupa. (Tuwatumie wanasheria wetu inapobidi, maana lugha nyingi za mikataba hii huwa ya kisheria zaidi)
 
For the last six month nimekuwa natumia ATM thus not using tellers as niko bize.
Sasa apo monthly service charge inakatwa kwa ajili ya nini wakati via ATM daily wanalamba

whether umetumia atma au manual teller lazima ulambwe kwa kila withdrawal. WATAKULA WAPI?
 
J Wengi wetu tunaingia mikataba na mambenki kama mazoea tu. (Tuwatumie wanasheria wetu inapobidi, maana lugha nyingi za mikataba hii huwa ya kisheria zaidi)


Ni kweli sikusoma mkataba barabara, lakini kwanini benki hazisemi mambo muhimu wakati ukijiunga? Ila mkuu ninarudi tene benk kuutafuta nione kama kuna lolote katika masuala ya gharama.

Mkuu ni mtanzania gani wa kawaida anayeweza kuajiri mwanasheria hata ktk masuala yanayohusu maisha yake? Mfano kesi ya mauaji ilhali wewe kwa uhakika unajua hukuua na adhabu yake unajua ni kifo. Kwa ufupi kuwa na mwanasheria ni ngumu.
 
Kwangu mm naona kama ni wizi tena wa khari ya juu sana.Hiyo hela ni kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida nasema hivyo kwa maana kwamba kuna wengine hata mia moja hawaioni kwa siku,atakuwa na haja hata ya kuweka hela bank?.Na isitoshe hata hiyo riba ambayo wanatoza wakikupa mkopo ni kubwa mnoo.Kuna baadhi ya nchi riba iko chini ya asilimia sita(6) wakati nyumbani Tanzania ni kati ya asilimia 12% hadi 17%.Na pia kwenye swala la ATM mbona nchi zingine huduma hii ni bure?tena kwa bank zote ndani ya nchi ilimradi uwe na Visa,Maestro na nk.
 
Wizi ni mkubwa sana katika haya mabenki yetu lakini naona wanajamii wanatetea kama ni mkataba na benki. Mikataba ya wizi iko mingi tu natumeiona toka enzi za kina Mangungo wa Msovero mpaka kina Barrick nao wanatuibia kimikataba.
Kwanza, Ukiwa na saving account ukiweka hela yako wanakupa riba ya asilimia 5% ambayo ni chini ya mfumuko wa bei (inflation) mfano asilimia 7% kwa hiyo ukiweka hela yako mwaka mzima unachopata ni hela pungufu kuliko uliyoweka kwa thamani.
Pili, Ukikopa benki unalipa riba ya 15% na kuendelea. Sasa tofauti ya riba za kukopesha (15%) na kuweka (5%) ndio faida ya benki na ndio wizi unapotokea. Kwa mfano ripoti ya ya CRDB (Income Statement for the Quarter ended 30th September 2008) inaonesha wamepata riba kutokana na shughuli za benki kama kukopesha watu (Interest Income) sh 26,949 milioni na wametoa riba kwa walioweka (save)(Interest expense) sh 4,628 milioni.
Tatu, Nakubaliana na wanajamii kwamba benki ni biashara lakini kinachoendelea hapa Tanzania ni unyonyaji.
 
There is no way banks would make the super profits that they make if they charged you fair fees. They steal from you if they overcharge you, and they do!

So, do banks steal from you? Absolutely! If you want less stealing then you must shop around for banks with more just rates.

Hizo rate za ajabu ajabu ndio Nyerere aliita MIRIJA. Ikiwezekana, weka fedha zako kwenye benki ambayo wewe mwenyewe una shea. That way, some of the loot will at least come your way.
 
There is no way banks would make the super profits that they make if they charged you "fair fees.

Unaposema "fair fee" unamaanisha nini? Fair kwa nani? Nani anaamua kwamba ni 'fair'? Naona tunasahau jambo moja la muhimu. Benki ni biashara kama nyinginezo, na faida ndio lengo lao. Hazifanyi kazi kama msaada kwako na kwa Mzeeba. Hivi muuza genge nani anamwuliza kama bei ni 'fair'? kama hutukubaliani na bei basi tunahamia genge la mbele. Na akikosa wateja basi itabidi aangalie utaratibu wa kuweka bei zake sawa. Huo ndio mfumo wa soko. Bila hizo faida hakuna ambaye angetaka kufanya biashara ya Benki au kuwekeza kwenye mabenki. Fikiria hata wewe mwenyewe huwezi fanya biashara isiyokulipa.

Pili benki kama CRDB (mfano) ina washika dau ambao wameweka pesa zao kwa kununua hisa. lengo likiwa lile lile kuzalisha pesa yao. sasa wao wanategemea benki hio iendeshe biashara zake na kupata faida ndio nao wapate faida kwa uwekezaji wao. Na ukubwa wa faida ya benki ndio ukubwa wa gawio lao. kwa hiyo utaona sio mzunguko mdogo huo tena ukizingatia wenye hisa nao wana akaunti zao kwenye mabenki.Ndio maana mwanzo nilishauri kabla ya kuweka pesa yako benki jiulize, Je hii ndio njia bora kabisa ya mimi kutumia pesa niliyonayo? au Je kwa kuweka benki ni faida gani napata na zipi nakosa? Weka kama italipa na acha kama hailipi. Tusifanye mazoea tu kuwa na akaunti za akiba benki, tena bila hata kuangalia kwa umakini katika benki gani.

Bila uwekezaji uchumi hauwezi kukua. Na mabenki kwa kufanya biashara zao vizuri watu wanaweza kuwekeza. Riba iwe 9% au 15% mwekezaji kashafanya mahesabu inalipa au la. (Je riba ni kubwa sana au la hilo ni swala lingine)

Kubwa ambalo mimi najiuliza Kama Mtu anakuibia (bila panga wala nyundo ya kukutisha), na wewe unajua anakuibia, kwa nini unaendelea kumpa nafasi akuibie wakati njia mbadala za kujilinda zipo? Je faida inayopatikana (riba, usalama wa pesa, urahisi wa kupanga, nk. ) ni kubwa zaidi kuliko kuweka chini ya godoro au kuanzisha genge?

 
Ikiwezekana, weka fedha zako kwenye benki ambayo wewe mwenyewe una shea. That way, some of the loot will at least come your way.

Sasa tuna kwenda mbele. Asante Moshi. Tusibaki walalamikaji tu. Cha muhimu ni namna gani tunaweza kujinasua katika matatizo tuliyonayo
 
Sijaelewa hapo aliposema unakatwa Annual card fee 5000, unamaanisha kila mwezi au?

je kuna anayefahamu interest za hizi bank zatu ktk aina mbalimbali ya account zao walizonazo? ningependa kujua ipi ina interest zaidi ya ipi.

Asanteni

Ni kwa mwaka kama sijakosea.

Wizi wa kwanza nadhani upo Barclays...gharama zao sitaki kuzisikia. Unaweza pasuka!!!
 
Back
Top Bottom