CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
Kwa miaka ya hivi karibuni idhaa ya kiswahili ya BBC imejikita Tanzania kana kwamba hakuna habari katika nchi nyingine. Halitokei jambo Tanzania BBC ikaacha kulitangaza tena mara nyingi bila weledi wala kuzingatia taaluma.
Jana kumetokea tukio la kihistoria na lenye manufaa si kwa Tanzania pekee bali kwa nchi zote za kiafrika zilizobarikiwa utajiri wa madini. Serikali imefikia makubaliano na moja ya makampuni makubwa kabisa duniani ambapo mkataba umeingiwa kumaliza uporaji dhahabu ya Tanzania.
Vyombo mbalimbali vya kimataifa ambavyo hata panya akifa Tanzania vinafanya ni habari kuu vyote kimya kulikoni?
Hatuwasikii BBC, VOA wala DW!
Lakini subiri punda achakatwe Tanzania usikie taarifa zao!
Lakini hakuna ambao wamegeuza Tanzania ndio habari yao kuu kuliko BBC! Hata mwakilishi wao ambaye huwa na kiherehere kutangaza mpaka vifo kimya! Kimya chao ni ushahidi tosha siku hizi wao ni BIASED BROADCASTING CORPORATION.