Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Wa kwanza alikuwa MWALIMU akatuyeyushaweeee kumbe naye alikuwa anapenda kuishi Dar.Wanajeshi wakamjengea bonge la HEKALI huko BUTIAMA lakini wapiiii, Mwalimua aliamua kuishi butiama ya DAR
Akaja MWINYI, na kama jina lake lilivyo, huyu yeye ni MWINYI sasa nadhani mnaelewa kuwa mamwinyi sikuzote hawajiwezi kwenye miji isiyo na bahari.
Akaja MKAPA, huyu alikuwa anajidai ana mambo ya KIZUNGU na vile vile ile mitikasi ya mkewe MAMA ANNA MKAPA kuwatapeli wazungu na NGO za kimataifa zisingewezekana kama MKPA angehamia DODOMA
JK of course huyu naye ni MWINYI na mtoto wa MJINI na ninahakika huko Dodoma hawana SAIGONI hivyo lest rule him out kuhamia huko
MZEE KINGUNGE ndio nasikia peke yake ndio yuko huko
Lawama zaidi nazielekeza kwa MZEE MALECELA alitakia apush zaidi lakini wapi!
WAPINZANIA nao wote wako mjini Dar wanazuga tuuu
inaonekana wote mmemiss jibu la Waziri Mkuu jana.. kasema watahamia Dodoma kwa awamu..! (whatever that means)
Mtizamo Mwingine,
Nadhani tufuate Africa Kusini (South Africa) Wanavyofanya!!! Tuachane na Dhana ya kuhamisha kila kitu Dodoma!!! Badaya lake tuangalie namna gani tutaweza tawanya Makao Makuu ya mihili mitatu ya Jamhuri!
BUNGE --- DODOMA
SERIKALI KUU --- DAR ES SALAAM (Maana hapaonyeshi kwamba wanataka kuhama)
MAHAKAMA --- MWANZA/ARUSHA
SERIKALI ZA MITAA --- DODOMA
Kwa maoni yangu hii inatekelezeka na haitaicost serikali Hela Nyingi, lakini pia ina faida ya kuijenga miji yote hence kufanya kasungura kagawanywe vizuri,,, South Africa Wanafuata Mfumo huo...
AIDHA Nakubaliana kwamba Wizara Ya Afrika Mashariki, Makao Makuu yawe Arusha
Naomba kuwasilisha
Mkuu mawasiliso yako yamefika JF na yamepokelewa.
Mkuu sio siri hii issue inakula pesa hata kuliko hayo mashangingi ya serikali. By the way nilisiki chuo kikuu cha Dodoma kingeanza kazi vipi kimeshaanza?
Chuo kikuu cha Dodoma kimeanza kwa wanafunzi 1000 kama sikosei na mkuu wa chuo ni HE. Ben Mkapa...
sijui website yao well hii inawezakukusaidia kidogo
By the way mtoto wa mkulima, ulikuwa maeneo ya mwenge ukifanya shughuli zako miaka 3-5 iliyopita? kidogo kama na-recall kitu kuhusu wewe!
Unajua ofisi zote za sirikali kukaa posta kunachangia sana foleni Dar? na hili ukitaka kujua wakati wabunge barabara ni nyeupe.
Nadhani tumuulize muungwana kuwa ni lini atahamishia Ikulu Dodoma ili kila mtu amfuate?
mkuu akihamia DODOMA wengine watafuata ila sasa Dar ni kama administration cluster maana mashirika yote kama UN,Labour, WB & IMF, Balozi zote ziko Dar sasa kama serikali ikihamia kule transaction cost nazo zitakuwa kubwa sana.
Mkuu nimekuelewa kabisa na hapa kunaishue ya kumake shure bara bara iko safi kabisa na pia reli ya kati ikiwa inafanya kazi freshi nadhani usafiri wa mabasi unaweza kuwa bomba tuu ila kwa hali kama sasa nasikia kunawakati hata kupata tiket ni shida maana tren ya kati (Mwanza,tabora na Kigoma) huwa inaanzia Dom kwa hiyo watu wanakuwa wengi sana. Unajua kweli mambo mengine ni aibu yaani reli iliyojengwa na Mkoloni mjerumani zaidi ya karine moja tunashindwa hata kuikarabati? kweli we are not serious. Unajua ukitoka Dar ukifika Mezani kibaha unakuta foleni kubwa ajabu ya malori na hakika reli ingefanya kazi hili lisingekuwepo na hata bara bara zisingechakaa haraka vile maana magari yanabeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wa bara bara na ajili za magari pia zingepungua. (sorry ni nnje ya topic ila wazo limenijia tuu)As said before siungi mkono serikali yote kuhamia Dodoma, it is expensive and it is not priority now!
BUNGE- DODOMA
MAHAKAMA - ARUSHA/MWANZA
SERIKALI KUU - DAR ES SALAAM
SERIKALI ZA MITAA - DODOMA
WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI - ARUSHA....
Issue ya cost ya wakati wa vikao vya bunge,,, ni ujina wetu tu,,, kama kungekuwa na shutle busses first class za serikali za kuondoka kila baada ya saa 3-4 nne, tungekataa kabisa zaidi ya mawaziri watu wengine kuwa na magari ya serikali wakati wabunge period,,, problem ya nchi yetu watu wetu wakigombea ubunge wazuri baada ya hapo wanatusahau!!!
Siku Bahari ikihamia Dodoma