Je, asili ya majini ni ipi?

Sawa mkuu
 
Mkuu wewe unawashangaa waislamu kusema kuwa kuna majini wazuri na wabaya kama tuluvyo binaadamu,ila na waislamu hushangaa pia wakristo wanaposema kuna malaika waovu.
 
Mkuu wewe unawashangaa waislamu kusema kuwa kuna majini wazuri na wabaya kama tuluvyo binaadamu,ila na waislamu hushangaa pia wakristo wanaposema kuna malaika waovu.
Hakuna Mkristo anayesema kuna Malaika Waovu.
Wala andiko linalosema hivyo halipo. Malaika ni viumbe wa ufalme wa Nuru.
Mfano,
kiumbe Ibirisi ni mwovu tu na hakuna Ibirisi mwema.
Biblia inasema, Majini ni viumbe waovu kama alivyo Ibirisi au Lucifer.
Majini ni aina mojawapo ya miungu inayotaka kuabudiwa kama Mungu, ndio maana katika Biblia Mungu amekataza kuyafanyia ibada na kuyatolea sadaka.

" 7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi "

Yesu Kristo alipokutana na mtu aliyepagawa na Majini au Mapepo wala hakuyapa nafasi ya kutubu, wala hakuwahi kufundisha kuwa kuna majini mema, ni kwamba aliyakemea ili yamtoke huyo mtu.
Majini yakimpagawa mtu huwa yana mtesa tu huyo mtu, haijawahi kuonekana Jini anamsaidia binadamu katika kufanya jambo jema.
Hivyo majini ni viumbe wa ufalme wa giza, pamoja na jamii zake kama ma Ibirisi, mamizimu, mapepo, mandondocha, mapopobawa, mavinyamkera, na jamii zake.
Kama kuna kitabu kinasema hayo maviumbe ni yanaweza kutubu na kutoka ufalme wa Giza na kuja ufalme wa Nuru basi ni mafundisho ya hicho kitabu lakini Biblia haisemi hivyo.
 
Hivi kwanini sijawahi kuskia majini yenye majina ya kikristu eg. John,Mary, Paul, Eugene etc. Utaskia maimuna sijui nani vile...
 
Pia naomba msaada kwa ndugu zangu waislamu, naskia kuna swala moja ukiisali sijui mara ngapi vile kufumba na kufumbua unamuona jini
 
Mkuu ukristo ndio unafundisha kuwa majini asili yao ni malaika waliyoasi,hivyo kwa mujibu wa ukristo majini ni malaika na ndiyo maana nasema waislamu nao hushangaa kwamba kuna malaika waovu ambao ndio hao majini.

Tatizo wakristo huchukulia majini kama viumbe vyengine kabisa wakati wanafundishwa kuwa wale ni malaika.
 
Hivi kwanini sijawahi kuskia majini yenye majina ya kikristu eg. John,Mary, Paul, Eugene etc. Utaskia maimuna sijui nani vile...
Tatizo majina mengi tunayotumia ni ya waarabu na wazungu,sidhani kama wazungu nao kuna jini wanaloliita Maimuna kama ambavyo tunavyofanya huku wabongo.
 
Tatizo majina mengi tunayotumia ni ya waarabu na wazungu,sidhani kama wazungu nao kuna jini wanaloliita Maimuna kama ambavyo tunavyofanya huku wabongo.
Sahihi kabisa. Ni suala la mapokeo tu.

Kama ambavyo wazungu Daudi wakamuita David.. Jibril Gabriel.. Yahya John.. Musa Moses.. Yusuf Joseph.. Mariamu Mary/Maria.. Issa Jesus.. Haruni Aaron.. Nuh Noah.. Is-haq Isack..

Niendelee?
 
Sahihi kabisa. Ni suala la mapokeo tu.

Kama ambavyo wazungu Daudi walivyomuita David.. Jibril Gabriel.. Yahya John.. Musa Moses.. Yusuf Joseph.. Mariamu Mary/Maria.. Issa Jesus.. Haruni Aaron.. Nuh Noah.. Is-haq Isack..

Niendelee?
Inatosha mkuu umeeleweka kabisa.
 
Ila wenzetu naona mnayapenda sana majini hadi mnatoa macho kuyatetea.
Utasikia mnasema.

" (-Majini ni viumbe tu wa mwenyezi Mungu kama tulivyo sisi wanadamu.
-Kuna Majini wema na wabaya kama tulivyo sisi wanadamu.
-Yako baadhi ya Majini yamesilimu na ni maislamu kama sisi tu.
-Majini yaliumbwa ili yamwabudu Mungu kama sisi.
-Msiyachukie majini kwa maana yako mengine ni machamungu sana na wanaijua dini kupita hata baadhi yetu sisi wanadamu.
- Majini hayana uhusiano wowote na Ibirisi Shetani.
- Tuwapende tu ndugu zetu wa Kijini kama tunavyopendana sisi watu.
-Mnayaonea tu Majini kwa kusema eti yote yamemuasi Mungu, yako mengine yanamtumikia Mungu kama tulivyo baadhi yetu sisi.
- Hata hiki kitabu chetu cha dini kinatumiwa pia na Majini, kwakuwa wao na sisi dini yetu moja.
-Acheni kuyasema vibaya Majini, kwani sisi na wao walio wema tutaenda kuishi peponi kwa pamoja baada ya Kiyama.) "

Poleni ndugu zangu.
 
Point ya msingi sio kuwa na majini wazuri au wabaya,bali ni asili ya hao majini ndio tatizo lililopo.

Maana wewe ndugu unapowazungumzia majini ni kama vile unazungumzia viumbe ambavyo vimeumbwa na vikiwa na ushetani kabisa yani asili yao ushetani.
 
Nimecopy kipengele hiki ulichoongelea kuwa....


Kwa hiyo aya hizi zinaonyesha kuwa Quran ilipokuja ndipo majini waliposilimu. Kumbuka kuwa Quran imeanza mwaka 610 B.K kipindi ambacho Biblia tayari ili kuwepo kwa karibu karne 6.


Kudeclear interest....Mimi ni muislam.

Kwanza ujue quraan ndo kitabu cha mwisho kuja,
Na mtume aliekuja na mafundisho ya quraan ni Muhammad s.w.

Quraan ni majumuisho ya vitabu vilivotangulia.. Baadhi yake ni ..zaburi...torat ....idjil na vingine...

Hoja yangu hapa, nabii Issa s.w ambaye wengine walimwita yeasu.
Huyu yy aliekuja kabla ya Muhammad s.w.
Na alikuja na kitabu kinaitwa injil.

Hiyo biblia unayosema ww ilikuwepo karne 6 kabla ya quraan ni ipi? Yaani ni mtume yupi aliekuja kuitetea biblia!?

Kama huna ulijualo kuhusu dini ni vema ungesoma zaidi kuliko kuzusha yasi0kuwepo!
 
Ndicho ulichovishwa hiki leo kanisani!!!?
 
Wacheni kuyatetea Majini, acheni yajitetee yenyewe.
Kwa ninyi nanyi ni Majini ?
 
Kwa kifupi kwa mujibu wa Quran mungu ameumba binadamu kwa udongo ,ameumba majini kwa moto na ameumba malaika kwa nuru
Binadamu na majini tunafanana kwa kila kitu ila wao walitangulia kuumbwa
Pia mungu anasema katika qurani nimeumba majini na watu ili waniabudu
Pia ktk aya nyingine anasema nimeweka pepo na jahanamu kwa ajili ya majini na watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…