kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,188
- 5,668
Hello bosses and roses, it has been a while...
Leo ngoja nimuongelee huyu kinda wa NBA kwa jina la Antony Edwards au Ant-Man, dogo wa 2001 tu hapa anaekipiga kwenye team ya Minnesota TImberwolves.
Huyu dogo ni hatari, kama umefuatilia NBA playoffs utaona kaongoza timu yake kuingia semi-final kwa mara ya kwanza in 20 years lkn pia kaongoza timu yake ishinde hizo semi-finals na kuingia final kwa mara ya kwanza kabisa toka timu ya wolves ianzishwe.
Huyu dogo ana energy fulani hivi kama alokua nayo marehemu Kobe Bryant, lakini pia uchezaji wake unataka kufanana na Michael Jordan hivo kupelekea watu wengine kuweka utani kwamba ni mtoto wa nje wa MJ.
Binafsi nikimuangalia akiwa anacheza naona ni combination ya Kobe Bryant na Michael Jordan ndani ya mtu mmoja.
Makinda wengi wamejikuta wanapotea sababu ya kukosa nidhamu na kutokuwa makini ndani ya uwanja hivyo kupelekea majeraha, mfano mzuri ni Ja Morant, ni dogo aliepata mafanikio makubwa sana ila tabia zake nje ya uwanja kama vile kuonesha bunduki hadharani na pia kutokuwa makini ndani ya uwanja ambapo kulimpelekea kupata majeraha kumemfanya afungiwe mara kadhaa kushiriki NBA na kukosa baadhi ya mechi muhimu. Ila kwa upande wa Anthony Edwards ni tofauti. Dogo anacheza moves hatari ndani ya uwanja ila yupo makini kuepusha majeraha, vile vile hana scandal mbovu mbovu nje ya uwanja.
Mwisho nitoe pole kwa waliompa Nuggets Game 7, najua imewashangaza sana kuona Wolves ameshinda. Nuggets mwanzoni alitawala mchezo, Kuna muda Nuggets alikua anaongoza hadi kwa tofauti ya alama 15, ila quarter ya mwisho akanyooshwa na kuishia kupigwa kwa tofauti ya points 6 (96 kwa 90).