Wachezaji wanaoongoza kwa kufunga pointi nyingi NBA

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Nyota wa Ligi ya Kikapu ya NBA, LeBron James amefanikiwa kuwa mchezaji anayongoza kwa kufunga pointi nyingi katika ligi hiyo baada ya kufikisha zaidi ya pointi 39,000.

LeBron (38) anayeichezea Los Angeles Lakers amefikisha rekodi hiyo akimpita nguli mwingine wa Lakers, Kareem Abdul-Jabbar ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa kufunga pointi 38,387.

Hadi kufikia hatua hiyo, LeBron aliyeanza kucheza NBA Mwaka 2003 pia amezitumikia Timu za Cleveland Cavaliers na Miami Heat.

Aidha, LeBron bado ana nafasi ya kuendelea kuongeza pointi kwa kuwa anaendelea kucheza.

1. LeBron James 39,038
2. Kareem Abdul-Jabbar 38,387
3. Karl Malone 36,928
4. Kobe Bryant 33,643
5. Michael Jordan 33,643
6. Dirk Nowitzki 31,560
7. Wilt Chamberlain 31,419
8. Shaquille O’Neal 28,596
9. Carmelo Anthony 28,289
10. Moses Malone 27,409
 
Back
Top Bottom