FourTwoNet
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 1,403
- 2,749
Ee bwana ee!
Juzi kati katika hali ya kupita pita hivi niko na mchizi wangu, si tukajikuta tumetulia eneo flani tunapiga stori na mrembo flani wa kishua huku tukimwagilia moyo.
Nikawa najipigia zangu stori tu kiaina, mara pap! Mchizi kaniita pembeni kanipiga na kitu cha "Huyu sista anakufeel ile mbaya". Nikamuuliza, "Umejuaje". Jamaa akafunguka, "Unaweza ukaona tu, anakuuliza maswali kibao, kila saa anakuangalia, na pia anaonyesha kukujali".
Kusema kweli wakuu, hilo sikuwa nimelitazama. Kidogo kidogo, jamaa flani mwingine kaja pale katulia na sisi, katupiga raundi za mvinyo za kutosha, alionekana mtu mwenye mawe yake. Likawa vibe kweli kweli, baada ya muda naona wanapigana mabusu na yule mrembo pale.
Sasa mchizi wangu alishachukuaga namba ya mrembo, akawa amemtext kwa kutumia simu yangu. Ikawa tabia ya mrembo kunipigisha chat hapa na pale. Sasa si nimemtania mrembo anifanyie muamala nikaogeshe moyo. Mara kitu hicho, ujumbe kutoka M-Pesa.
Hivi atakuwa ananipenda au kaamua tu kunioshea wakuu?