ndio maana nikaweka space kwa kuna gari za bei ghali zina huo mfumo wa compressor za umeme, ila Ac ya umeme kwa magari sio practical maana ufanyaji kazi kwa muda mfupi sana kabla ya battery hazijakuwa flat charge, Volvo waliweka system hiyo Battery Ac kwa battery mbili za 230 Mah walikuwa hawapati masaa mawil ya air con , imebidi waongeze battery tatu kwa ajili ya leisure amabyo ipo separate battery za kuwashia gari ,
Shughuli nzima ya kugandamiza freon gas sio ndogo ndio sababu hata mada inazungunzia hilo , maana compressor inapofanya kazi lazima mzigo uongezeke kwenye engine na ndio sababu gari huongeza ulaji wa mafuta ,wataalamu wa mahesabu wanasema mzigo inaobeba engine kwa ajili ya compressor inayopooza cabin ya saloon car , ni mkubwa zaidi kuliko mzigo wa kubeba abiria watatu kwenye saloon hiyo, kwa maana halisi ni kuwa unaweza ukatoka na familia yako yote kwenye gari na usihisi tofauti ya ulaji wa mafuta kama hujawasha Ac , ila hata kama hujabeba mtu ,upo peke yako kwenye gari ukiwasha Ac utaiona tofauti kubwa ya ulaji wa mafuta.