GE2025 Jawadu: Polepole na Gwajima wana chuki na ubinafsi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amesema kauli zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, wakiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kawe (CCM) ,Askofu Josephat Gwajima, na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, hazina mashiko ya hoja, bali zimejawa na chuki, ubinafsi, na kukosa ushahidi wa msingi dhidi ya uongozi uliopo madarakani.

Jawadu ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa baadhi ya wanachama wa CCM waliotoa matamko ya ukosoaji dhidi ya serikali.

“Mimi natofautiana na kauli za baadhi ya wanasiasa wenzetu, hasa ndugu Polepole na Gwajima. Kauli zao zimejikita zaidi katika mtazamo wa chuki binafsi kuliko uhalisia wa mambo. Unapodai kuwa kuna kuyumba kwa mifumo ya kiuongozi pasipo ushahidi wa wazi, wakati huo huo serikali hiyo hiyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa – hoja hiyo haiwezi kusimama,” amesema Jawadu.
 
mtaongea mengi safari hii yani mtaunganisha hata paka akitoa mulio mtaunganisha tu.CCM mnakazi
 
Huyu atakuwa na uwendawazimu wa aina fulani. Hivi nani mwenye chuki kati ya anayeteka na kuwauua wanaomkosoa au anayesema kuteka na kuua ni uovu, na uovu ukomeshwe?

Kama hawa ndiyo viongozi wa UVCCM, basi hiyo UVCCM imajaa takataka!!
 
Gwajima mlibomoa kanisa lake na kuyafungia mengine
Huyu polepole mtanya nn?
Mumpeleke kwa msajili ili akawafungulie kesi za hati za dharura huko mahakamani
 
1111111111111111111111111111111111111111111111111111..1.jpg

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2025
 
Aliyekua mbunge.

Kwani Bunge limevunjwa?
 
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, amesema kauli zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, wakiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kawe (CCM) ,Askofu Josephat Gwajima, na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, hazina mashiko ya hoja, bali zimejawa na chuki, ubinafsi, na kukosa ushahidi wa msingi dhidi ya uongozi uliopo madarakani.

Jawadu ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa baadhi ya wanachama wa CCM waliotoa matamko ya ukosoaji dhidi ya serikali.

“Mimi natofautiana na kauli za baadhi ya wanasiasa wenzetu, hasa ndugu Polepole na Gwajima. Kauli zao zimejikita zaidi katika mtazamo wa chuki binafsi kuliko uhalisia wa mambo. Unapodai kuwa kuna kuyumba kwa mifumo ya kiuongozi pasipo ushahidi wa wazi, wakati huo huo serikali hiyo hiyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa – hoja hiyo haiwezi kusimama,” amesema Jawadu.

Jibuni hoya ! No reform no election
 
Back
Top Bottom