Hapa kuna ukosefu wa taarifa unaosababisha Upotoshaji wa Mambo
NOTICE OF SUSPENSION
Kampuni ya JATU imekuwa suspended kwenye soko la hisa kwababu inafanya IPO kwa mara ya kwanza.
Kampuni ya JATU ilikuwa ipo Listed na inatoa audited financial statements zote
Kampuni ya JATU imeingia kwenye kipindi cha IPO sasa hivi.
Kuna mwandishi amesema JATU ni kampuni ya UTAPELi, je ametapeliwa nini? au utapeli uko wapi? Tuache habari za kupotosha UMMA kwenye mambo usiyo na ufahamu nayo. leta Hoja ya msingi mezani na sio UMBEYA
PFA : JATU PROSPECTUS , JATU FINANCIALS FOR 3 YEARS
Ebu tuangalie mtu aliyelima hekari moja mwaka jana na mwaka huu anapata nini (kama atakipata)
Gharama za kulima shs. 904,200
Kati ya hizi, wanakukopa 2/3 =shs. 602,800
Wewe unlike shs 301, 399
Mwaka huu wamesema wamevuna gunia 22 kwa ekari.
Kwa hiyo:
Wao wananunua gunia moja kwa shs. 56,000
22 x 56,000 =shs. 1,232,000 (Hii ndio pesa wanayokwambia ni faida) kwenye vikaratasi.
Hawakwambii yafuatayo.
Tax 2% of 1,232,000=24,640
Kuna gawiwo (hili ni kichaa tu ndo anaweza kulielewa) shs. 3000 kila gunia =3000 x 22 =66,000
Mkopo wao 2/3 =602,800
Eti mwaka huu kulikuwa na ongezeko la shs. 53,000 kwenye gharama za kilimo.
Kukodisha ekari moja ni shs. 100000
Jumla ya makato yote haya ni shs. 846,440
Chukua sasa faida yako shs. 1,232,000-shs. 846,440 =shs.
385,560
laki 385,560 ndo hela utakayopata baada ya kusubiri mwaka mmoja. Sasa hii laki tatu kuja kuipata! Unaweza kusubiri hata miezi mitatukabla hawajakupa, kupokea simu yako nk.
Sasa jiulize. Wewe ungejilimia mwenyewe muda wa mwaka mzima ungekuwa wapi?
Ukiongeza usumbufu wao? By the way, katika huo muda, wanakulazimisha kununua kilo 100 za chakula. Hiyo inapunguza sana balance yako ya laki 3.
Sasa hii ndio Jenga Afya Tokomeza Umaskini??
Au "lima na sisi ondoa stress"?
Pima mwenyewe na chukua hatua! Kama kuna mtu wa Jatu anayepinga hizi data aje hapa aseme. Maana huko nyuma nimeona mnaleta karatasi.