JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

Hakunaga pesa ya bure brother , hakuna mchongo wwte wa haki hapa duniani , pesa ili uipate mzee Baba lazima upite Kona kibao, ....iwe biashara , kilimo , iwe makazini , upate pesa ndefu lazima sarakasi zihusike Mzee ...!! Hayo makampuni ni wizi mtupu cha msingi ni kwekeana timing tu, wakikuwahi kwenye angle umekwisha , ukiwawahi unapiga hela unatembea
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Hawa Leo Walikuwa Wanahojiwa Na Kipanya Wakawa Wanyonge Kumbe Ni Wapigaji Ila Nasi Tumezidi Yaani Hata Tukiambiwa Tunapigwa
Lazima Utakuta Idadi Kubwa Wamepigwa WAmechakaa Hoi
Ukihoji kidogo Tu. Utasikia wenzako wanapata, wanafaidika wewe unapoteza muda kuulizauliza maswali!
Unapigwa Vita. Unasimangwa hujui lolote! Negative

Ila tuliwaonya! Ukae town. Utegemee wenzako wakae shambani. Waungue na jua, walowane na mvua. Wakuletee faida!

Na kuna michezo walicheza Sana walipoingia DSE, kupandisha hizo hiza zao, nunua uza, nunua uza!
Tulioumizwa na Hilo soko la DSE tulikuwa tunawacheki Tu na kusema hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, mind you mwendazake alikuwepo!
 
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika
Ikawaje
 
Ukihoji kidogo Tu. Utasikia wenzako wanapata, wanafaidika wewe unapoteza muda kuulizauliza maswali!
Unapigwa Vita. Unasimangwa hujui lolote! Negative

Ila tuliwaonya! Ukae town. Utegemee wenzako wakae shambani. Waungue na jua, walowane na mvua. Wakuletee faida!

Na kuna michezo walicheza Sana walipoingia DSE, kupandisha hizo hiza zao, nunua uza, nunua uza!
Tulioumizwa na Hilo soko la DSE tulikuwa tunawacheki Tu na kusema hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, mind you mwendazake alikuwepo!
Tanzania ukitangaziwa fursa basi juwa wewe ndio fursa yenyewe.
 
Wanakulazimisha kununua mazao kilo 100 hadi 200. Ukishamaliza kununua, wakivuna mazao huwezi kulipwa hata ufanyeje. Watakuzungusha mpaka utachoka.

Taratibu zao, wao pekee ndo wanajiuzia mazao kwa bei ya kutupwa. Wakishanunua kwako, wanakulazimisha kukuuzia kwa bei karibu mara mbili ya ile walonunua kwako.

Wakigundua kwamba unahitaji pesa zako hili utoke, faida yako wanaikata asilimia 70. Watakudanganya kwamba kuna gharama za kilimo ziliongezeka kila ekari. Kumbuka mwanzoni wameishakutoa gharama kubwa sana za kulima ekari moja.

Pia wanakutoa gharama nyingine za ajabu. Yaani faida yako kama ni millioni moja, wanaweza kukupa laki mbili.
Viongozi wa hiyo kampuni ni waongo haswaa. Wakati wa kudai pesa, hakuna mtu atakayeongea na wewe mule ndani. Wote watajifanya hawafanyi kazi hapo.

Kwa ufupi sijui ni kitu gani kile. For sure sio kampuni. Operation zake ni kama upatu. Yaani hawa wanalipa hawa wanalipwa. Wasipolipa hawa, kila kitu kinakufa. Mfumo wao upo hivo hivo. Nina wasi wasi kama mashamba wanayosema yapo kweli. Inawezekana kuna ekari 20 za mahindi ila wao wanasema ekari 2000. Hawajali wateja hata kidogo. Naandaa report yao yenye data zao zote na maneno yao. Kwa wanaofatilia mtashangaa.

Kama unapenda kulima, jilimie mwenyewe. Hawa watakupotezea muda wako na akili yako. Wamekaa kama either hawajui wanafanya nini au wapo hili kupiga pesa yako.
Maamaaaae almanusura nijiunge
 
Tatizo Watanzania wengi tuko Lazy sna. Sasa mtu akisikia tu kuwa "Unalimiwa Shamba" then wew unakunja 4 tu na kusubiria Faida atakimbilia fasta sana Ila mwambie akalime mwenyewe hapo ndio kasheshe. Tu wavivu sanaa kwakweli.
 
Hahahahahah watu wanabadili mifumo tu ila upigaji uko pale pale tu
Mwenyewe nataka kufungua michongo miwili ufugaji ng'ombe Kwa pamoja na ufugaji mbuzi Kwa pamoja!
Nikishawasminisha ng',ombe wanazaa mpacha vmbuzi vinazaa triplets, nitawadaka Tu!
Na maziwa tunauza uarabuni kombe la dunia!

Nikishafikisha malengo Tu. Namtumia Mange Mchongo anilipe Kwanza kisha alipue kampuni ni feki!

Mbona easy Tu. Mapichapicha Instagram na YouTube, ninaukimbia umaskini! Kwa Kasi ya escape velocity!
 
Hata mimi naliwaza hiki kwani qatanzania ni mbumbumbu sana
 
JATU Plc imefikia leo tar 9 Sep 2021 Shs 940 kwa hisa moja. Kutokea ile bei waliotumia kufanya listing ya Shs 500 kwa hisa.

Kwa ufupi, kama ulikuwa na Shs 20,000,000 benki imetulia mwezi wa 6 au wa 7. Ukajipiga kununua shares 40,000 kwa Shs 500. Leo ukiamua kuziuza unapata cash money Shs 37,600,000 (yani 40,000 x Shs 940).

Profit yako ni Shs 17,600,000 ambayo hujaitolea hata tone la jasho. Ni balaa tupu.

View attachment 1930961
Duuuuuuu
 
Back
Top Bottom