JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,816
6,748
Kuna mtu anajiita JATU na yeye ana model kama ya Mr kuku, ile ya kwamba toa pesa ulimiwe na uvuniwe.

Huyu JATU kawavuta watu wengi sana mara mashamba Kitetto mara Morogoro.

Model anayo tumia ni ya upatu ni Pyramid ambapo watu wa mwanzo hufaidika ili kuvuta watu wa mwesho ambao huja kuwa victim.

Hawa watu huwa kujitangaza sana ndo jadi yao, kufanya mikutano kwenye hoteli kubwa kubwa ndo jadi yao ila zote hizo huwa ni mbinu za kuvuta watu waingie wapigwe pesa.

Kama JATU anaona kilimo kinalipa kwa nini asiingie akalima pekee akapiga pesa? Kwa nini asichukue mkopo alime huko kiteto apige pesa? Mbona Summury analima pekee yake huko kwao Sumbawanga?

Watu wawe makini na hizi Pyramidi za kwamba toa pesa ulimiwe. Kwa nini asilime yeye?

Mboma MO hawaiti watu wakalime katani huko Tanga? au mbona Interchick hawaambii watu waende wafuge wote kuku?

Jamani tujizidishe Watanzania tunapigwa kirahisi sana.
 
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika
 
Kwa kuwa wajinga hawaishi hizi kelele hazitosaidia

Kitachowashtua ni muda tu, jinsi watakavyokuwa wanapigwa au kushuhudia watu wakipigwa ndio akili zitavyokaa sawa

Walianzaga Deci, wakaja kina Ontario, Mr. kuku n.k itafikia mwisho watu watashtuka wenyewe lakini kwa utaratibu wa kuwaambia namna hii utaitwa majina mengi
 
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika
Same old Namaingo story. Mtapigwa sana kilimo hakijawahi kuwa rahisi kiasi hicho. Same old story za tutakutafutia soko hapo wataenda kuuzia hizo pembejeo zao then watawakimbia.
 
Utalimiwa vipi shamba?
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika
 
Kama unataka kulima ingia front mwenyewe

Mkuu kwa tanzania hii hicho kitu hakipo hapo unatafuta kupigwa tuu, kama sio mwanzo mwanzo basi baadae lazima utapigwa.
 
Duu nilishafanya nao mchakato nijiunge na jatu wamenambia ada ni 30,000 ndo nlkuwa najipanga niingie,wanasema wanatoa mikopo isiyo na riba afu uwe active member,at least everythree months uwe unanunua bidhaa zao.

Wanakupa mchanganuo wa gharama za kulima zao fulani kisha Wanakutafutia shamba, wanakulimia(vibarua+madawa/mbolea), wanakuhifadhia wanakutafutia soko then utalipwa kutokana na bei ya soko la zao husika
Aisee na wewe ukawaamini. Kweli mtu akufanyie hivyo vyote bure na bado hela yako akupe kama ilivyo + faida juu!

Amekua msamaria mwema ameshushwa toka juu au anakupenda sana?
Aki watanzania we need to wake up jamani na tusipende vitonga, hamna hela ya rahisi kiasi hiko.
 
Back
Top Bottom