JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

Udogo na ukubwa wa faida unaupima kwa vigezo vipi? Ukinipa m100 yako nikawekeze shambani kwa gharama zangu kisha nikakurudishia m101 na mm nikachukua m29 ya faida unapimaje kuwa ni unyonyaji iwapo huna ushiriki katika utendaji?
Mimi nafanya kilimo hivyo najua gharama zote za kuanzia kwenye kulima mpaka kuuza mazao.
Ukisimamia shamba lako wewe mwenyewe faida ni kubwa sana tena sana kuliko kujiunga na hao wahuni wa JATU.
Bahati nzuri niliwashitukia mapema, niliposoma mchakato wao nikagundua hao ni "wanyonyaji" maana uzoefu wa kilimo ninao.
 
Unawalaumu DSE bure, kabla ya mwekezaji kununua hisa inabidi yy afanye uchunguzi au awatumie wataalam ili ajue kama uwekezaji wake utamlipa. Kosa sio la dse kosa ni watu kuwekeza kwa kukurupuka. DSE wana conditions zao kama ilivyo NASDAQ au NSE na yyt anaetimiza conditions basi ana haki ya kuwa listed mule.

Tatizo hii jatu naona inapigiwa promo hadi na millardayo, kitu ambacho kinafanya wengi wanunue kwa kufuata mkumbo tu. Shida kubwa ni ukosekanaji wa elimu ya uwekezaji kwa wananchi, hayo mengine utalaumu watu bure.
 
DSE wana conditions zao kama ilivyo NASDAQ au NSE na yyt anaetimiza conditions basi ana haki ya kuwa listed mule.

NASDAQ na NYE do not list any company that has elements of a Ponzi scheme!! Millard Ayo sio authority wa investments wao wanafanya advertisement na kulipwa; wanajali malipo ya matangazo hawapo hapo kuwaelimisha watu jiu ya JATU!!
 
Mkulima nikikupa pesa uache kazi zote ukashinde shamba ukishavuna wewe ndo ununue utajua utapopeleka utaniletea faida % kiasi gani cha fedha nilichokupa ?
 
Elimu elimu, tupende kusoma kuuliza hata kama tutatukanwa, tusiogope kushambuliwa.

Tusipende kuhadithiwa hata tukihadithiwa basi za kuambiwa uchanganye kidogo na za kwako.

Binafsi nimejifunza SANA, hisa sitonunua tena, soko letu kuna kitu mahali hakijakaa fresh. BORA nijichange niende kule kwenye hati fungani.

Everyday is Saturday...............................
 
Bonds(hati fungani) ni option nzr sana, uwe na mtaji tu.
 
Hati fungani nako majanga
 
Ukicompare na hisa, hati fungani ni bora.

Ziwe bonds za serikali au za makampuni

mwekezaji ana uhakika wa kulipwa kabla ya wanahisa endapo kampuni likifirisika.

Pia bonds hazishuki thamani, labda uanze kuongelea issue ya inflation
Mkuu hati fungani ukitaka hela yako insrudi kwa wakati au mpka uzungushwe?
 
Sasa hivi wanapita masokoni/mitaani na mfuso wao(kama mashirika ya simu) ....wanapiga muziki na kuuza hisa kwa shs 5000. ...sijui kama wanaoshawishiwa wanalewa kitu wanachoshawishiwa kununua.
 
Mwezi ukiisha na IPO inaisha hizo 500 per zinarudi pale zilipokuwa 1200 per share. Uzi usiishie hapa njoo mtoe madini tena
 
Sijaridhika ngoja nicheke vizuri πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Nilitegemea ofisi zao kuwa shambani sasa wako mjini hapo nssf tower πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Hawa jamaa wamenishawishi sana leo kwenye 7.7..hadi CEO wao akaomba nionane nae..ila mh..nashukuru kwa uzi huu
 
Liko wazi sana, sema kwakuwa Watanzania tuna uvivu wa utafiti basi anatutandika sawa Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…