JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

Apr 8, 2021
46
95
Kuna mtu anajiita JATU na yeye ana model kama ya Mr kuku, ile ya kwamba toa pesa ulimiwe na uvuniwe.

Huyu JATU kawavuta watu wengi sana mara mashamba Kitetto mara Morogoro.

Model anayo tumia ni ya upatu ni Pyramid ambapo watu wa mwanzo hufaidika ili kuvuta watu wa mwesho ambao huja kuwa victim.

Hawa watu huwa kujitangaza sana ndo jadi yao, kufanya mikutano kwenye hoteli kubwa kubwa ndo jadi yao ila zote hizo huwa ni mbinu za kuvuta watu waingie wapigwe pesa.

Kama JATU anaona kilimo kinalipa kwa nini asiingie akalima pekee akapiga pesa? Kwa nini asichukue mkopo alime huko kiteto apige pesa? Mbona Summury analima pekee yake huko kwao Sumbawanga?

Watu wawe makini na hizi Pyramidi za kwamba toa pesa ulimiwe. Kwa nini asilime yeye?

Mboma MO hawaiti watu wakalime katani huko Tanga? au mbona Interchick hawaambii watu waende wafuge wote kuku?

Jamani tujizidishe Watanzania tunapigwa kirahisi sana.
Naheshimu mawazo yako juu ya JATU, ila sikubaliani nayo! JATU analenga katika kukamilisha dhana ya kukusanya mtaji au mitaji ili awekeze, pamoja na hao wenye fedha zao, kwenye kilimo au eneo jingine lolote analodhani au watakalodhani, hao wachangiaji kuna TIJA. JATU anatafuta nguvu ya wengi ili kuondokana kwenye umasikini wa kipato (income poverty). Kwa siku za karibuni, dhana hiyo inatumiwa ma wale jamaa wa VANILLA VILLAGE wa Njombe. Umewasikia?
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,292
2,000
Kipigo kiko pale pale, wacha nikamate fuko la popcorns. Hamna hela nyepesi kmmmk

It is unfortunate kwamba watu wanategeka kwavile JATU wako listed kwenye DSE!!! Unaponunua hisa ni muhimu sana kuwachunguza management ya hiyo kampuni inayouza hizo hisa!!! DSE as is currently constituted haina watu wenye weledi wa kutosha kuzichunguza kampuni zinazoingia kwenye soko lao kuwa kweli wana vigezo vya kuweza kuwafaidisha wanahisa wao!!! Sidhani hata kama wanaweledi wa kuthibiti INSIDE TRADING kwenye soko lao!!!! Hapo ndio maana watu wanapigika kwani viongozi wa DSE wanapasisha PONZI schemes kama acceptable investors!!
 
JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
646
1,000
Wewe ukienda kinyume na sheria zilizopo kuhusu masoko ya mitaji inabidi uchukuliwe hatua.
Hiyo ndo akili yaaani.

Unamuacha mtu anakusanya pesa za watu zikijaa ndo unagundua kuwa hajafata taratibu sheria ichukue mkondo wake unamchukulia hatua kwa kuchukua mtaji bila kuwarudishia wenye mtaji. Busara ya hali ya juu hiyo.
Wajinga ndo waliwao ila kama kuku ni tapeli basi yupo na ushirikiano na tapeli mwingine mkubwa.
 
Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,607
2,000
Udogo na ukubwa wa faida unaupima kwa vigezo vipi? Ukinipa m100 yako nikawekeze shambani kwa gharama zangu kisha nikakurudishia m101 na mm nikachukua m29 ya faida unapimaje kuwa ni unyonyaji iwapo huna ushiriki katika utendaji?
Mimi nafanya kilimo hivyo najua gharama zote za kuanzia kwenye kulima mpaka kuuza mazao.
Ukisimamia shamba lako wewe mwenyewe faida ni kubwa sana tena sana kuliko kujiunga na hao wahuni wa JATU.
Bahati nzuri niliwashitukia mapema, niliposoma mchakato wao nikagundua hao ni "wanyonyaji" maana uzoefu wa kilimo ninao.
 
kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
892
1,000
It is unfortunate kwamba watu wanategeka kwavile JATU wako listed kwenye DSE!!! Unaponunua hisa ni muhimu sana kuwachunguza management ya hiyo kampuni inayouza hizo hisa!!! DSE as is currently constituted Haifa watu wenye Weledi wa kutosha kuzichunguza kampuni zinazoingia kwenye Sokoine lao kuwa kweli Wana vigezo vya kuweza kuwafaidisha wanahisa wao!!! Hapo ndio maana watu wanapigika kwani Viongozi wa DSE wanapasisha PONZI schemes kama acceptable investors!!
Unawalaumu DSE bure, kabla ya mwekezaji kununua hisa inabidi yy afanye uchunguzi au awatumie wataalam ili ajue kama uwekezaji wake utamlipa. Kosa sio la dse kosa ni watu kuwekeza kwa kukurupuka. DSE wana conditions zao kama ilivyo NASDAQ au NSE na yyt anaetimiza conditions basi ana haki ya kuwa listed mule.

Tatizo hii jatu naona inapigiwa promo hadi na millardayo, kitu ambacho kinafanya wengi wanunue kwa kufuata mkumbo tu. Shida kubwa ni ukosekanaji wa elimu ya uwekezaji kwa wananchi, hayo mengine utalaumu watu bure.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,292
2,000
DSE wana conditions zao kama ilivyo NASDAQ au NSE na yyt anaetimiza conditions basi ana haki ya kuwa listed mule.

NASDAQ na NYE do not list any company that has elements of a Ponzi scheme!! Millard Ayo sio authority wa investments wao wanafanya advertisement na kulipwa; wanajali malipo ya matangazo hawapo hapo kuwaelimisha watu jiu ya JATU!!
 
JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
646
1,000
Mimi nafanya kilimo hivyo najua gharama zote za kuanzia kwenye kulima mpaka kuuza mazao.
Ukisimamia shamba lako wewe mwenyewe faida ni kubwa sana tena sana kuliko kujiunga na hao wahuni wa JATU.
Bahati nzuri niliwashitukia mapema, niliposoma mchakato wao nikagundua hao ni "wanyonyaji" maana uzoefu wa kilimo ninao.
Mkulima nikikupa pesa uache kazi zote ukashinde shamba ukishavuna wewe ndo ununue utajua utapopeleka utaniletea faida % kiasi gani cha fedha nilichokupa ?
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,563
2,000
Unawalaumu DSE bure, kabla ya mwekezaji kununua hisa inabidi yy afanye uchunguzi au awatumie wataalam ili ajue kama uwekezaji wake utamlipa. Kosa sio la dse kosa ni watu kuwekeza kwa kukurupuka. DSE wana conditions zao kama ilivyo NASDAQ au NSE na yyt anaetimiza conditions basi ana haki ya kuwa listed mule.

Tatizo hii jatu naona inapigiwa promo hadi na millardayo, kitu ambacho kinafanya wengi wanunue kwa kufuata mkumbo tu. Shida kubwa ni ukosekanaji wa elimu ya uwekezaji kwa wananchi, hayo mengine utalaumu watu bure.
Elimu elimu, tupende kusoma kuuliza hata kama tutatukanwa, tusiogope kushambuliwa.

Tusipende kuhadithiwa hata tukihadithiwa basi za kuambiwa uchanganye kidogo na za kwako.

Binafsi nimejifunza SANA, hisa sitonunua tena, soko letu kuna kitu mahali hakijakaa fresh. BORA nijichange niende kule kwenye hati fungani.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
892
1,000
Elimu elimu, tupende kusoma kuuliza hata kama tutatukanwa, tusiogope kushambuliwa.

Tusipende kuhadithiwa hata tukihadithiwa basi za kuambiwa uchanganye kidogo na za kwako.

Binafsi nimejifunza SANA, hisa sitonunua tena, soko letu kuna kitu mahali hakijakaa fresh. BORA nijichange niende kule kwenye hati fungani.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Bonds(hati fungani) ni option nzr sana, uwe na mtaji tu.
 
kinywanyuku

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
3,017
2,000
Elimu elimu, tupende kusoma kuuliza hata kama tutatukanwa, tusiogope kushambuliwa.

Tusipende kuhadithiwa hata tukihadithiwa basi za kuambiwa uchanganye kidogo na za kwako.

Binafsi nimejifunza SANA, hisa sitonunua tena, soko letu kuna kitu mahali hakijakaa fresh. BORA nijichange niende kule kwenye hati fungani.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Hati fungani nako majanga
 
IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
766
1,000
Screenshot_20210611-005204.jpg

Mambo ya jatu ayo na piere liquid
 
kinywanyuku

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
3,017
2,000
Ukicompare na hisa, hati fungani ni bora.

Ziwe bonds za serikali au za makampuni

mwekezaji ana uhakika wa kulipwa kabla ya wanahisa endapo kampuni likifirisika.

Pia bonds hazishuki thamani, labda uanze kuongelea issue ya inflation
Mkuu hati fungani ukitaka hela yako insrudi kwa wakati au mpka uzungushwe?
 
truckdriver

JF-Expert Member
May 7, 2012
546
250
Sasa hivi wanapita masokoni/mitaani na mfuso wao(kama mashirika ya simu) ....wanapiga muziki na kuuza hisa kwa shs 5000. ...sijui kama wanaoshawishiwa wanalewa kitu wanachoshawishiwa kununua.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom