Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

*Riwaya : Mpango wa Congo

Sehemu ya sita*

Kuna nini! Hakujua na la muhimu zaidi ni kuomukoa kwanza binti kisha mengine yatajulikana badae.

Akamvutia nyuma na kuwa kinga yake.
Mchoro ukachorwa huku raia wakianza kujaa kushuhudia linalojiri.

****

KINSHASA CONGO

…kutoka pale alipokuwa Honda alibakiza hatua mbili tu afike kwenye ukingo wa daraja lililokuwa linapitisha maji kwa chini.
Na bado alikuwa amemkaba barabara Sajini Kebu.
Wale askari wengine walikuwa bado wanapiga hesabu za kumwokoa Sajini Kebu kwa kusuburi Honda afanye kosa lolote ambalo hadi wakati huo halikuwa limefanywa nae hivyo wakakosa la kufanya.

Lakini Honda mbali ya kuwa na hesabu za kutoroka bado alikuwa anawazia namna ya kuwatoroka ama kuzua varangati litakalo wafanya wasahau kuhusu mkoba na kile kidole pale chini.

Pale walipokuwa ilikuwa ni barabara isiopitisha magari kwa wingi.
Lakini kwa mbali masikio ya wote yalinasa sauti ya kuja kwa gari kubwa.

Honda alitabasamu huku watekaji wake wakiingiwa na mchecheto wa namna ya kumuokoa sajini Kebu kabla gari hakijafika.

Hesabu zilipigwa pande zote.

Dereva wa lori aliona tukio lililokuwa mbele yake. Kurudi nyuma akaona haiwezekani hivyo akaamua kuongeza mwendo ili avuke pale darajani kwa kasi huku woga ukiwa umemtamalaki na mkojo ukikaribia kugonga hodi kwenye kipamchulio.

Lori lilizidi kukaribia na Honda nae alizidi kujisogeza kwenye ukingo wa daraja huku akiwa bado amemtundika kabali matata Sajini Kebu.
Hatimae lori likafika na hapo ndipo lilitokea tukio ambalo yaezekana Sajini Kebu na wenzie hawatakuja kuliona likijirudia tena katika himaya za macho yao iwe akhera ama Duniani.

***
Kilikuwa ni kitendo cha gafla na cha kutumia akili zisizo za kawaida kutumiwa binadamu mwenye nyama. Ila kwa Honda iliwezekana.
Japo si kwa kupenda ila ni kujitoa muhanga kuikoa uhai wake.

Lori lilikuwa mita tatu kutoka walipokuwa yeye na mateka wake Sajini Kebu,ni wakati huo Honda alipomsukuma kwa nguvu sajini Kebu kwenye kingo za daraja kisha yeye akajirusha kwa kasi uvunguni mwa lori lililokuwa kasi ya aina yake.
Kitendo kile kilionwa vizuri na askari waliokuwa wanataka kumteka tena,lakini pia kilionwa na Sajini kebu aliekuwa amejipigiza kwa nguvu kwenye kingo za chuma za daraja na kumtoa ukelele wa woga.
Lakini hakuna alietegemea Honda angeweza kujirusha kwenye uvungu kwa hesabu kali namna ile na kwa lengo gani.

Hawakujua!!

Lori lilipita kwa kasi na kumwacha chini Honda aliekuwa amelala kwa kujinyoosha bila kutikisika ili asidhuriwe na tairi kubwa za lori.
Hatimae Lori lilimwacha salama chini na lilipokwisha kupita akanyanyuka kwa kasi ya ajabu na kisu chake mkononi,kisha akawatazama adui zake waliokua bado wamezubaa.

Akaitumia nafasi hiyo kuwashambulia kwa kasi ya aina yake, huku miguu ikinesa kama mcheza dansi ya Apakacha.

Kisu chake alikirusha kwa kasi kikaenda kujikita begani kwa askari mmoja aliekuwa mbele yake, kisha haraka akawageukia waliokuwa kushoto kwake wanajiandaa kuachia risasi.
Mmoja akamchota mtama safi kisha bila kumjali akaruka juu na kumshindilia teke la kifua mwingine aliekuwa anajiandaa kumpiga na kuwaacha wakienda chini kama mizigo huku bunduki ikiangukia mikononi mwake na bila kusita akajiangusha chini na kukoswa risasi kadhaa na alipoachia za kwake zikaangukia kifuani kwa askari wawili na kuwatupa chini wakiwa hawana uhai.

Sajini kebu aliyaona yote ila hakuwa na la kufanya mana kasi ya Honda ilizidi hata kasi ya upepeso wa macho yake.
Na bila kupenda akajikuta akitazamana na domo la AK 47 iliokuwa mikononi mwa Honda tayari kumsambaratisha.
Kebu alipotizama vijana wake akawashuhudia wakijizoa zoa bila kuwa na uimara milini mwao.
Hawakuwa na la kufanya wote wakawa mateka wa Honda.

“Nani kawatuma?” aliuliza Honda.

Hakupata jibu.
Akaona kuwauliza majasusi kama wale kirahisi vile ni kujisumbua anamengi ya kufanya huko mtaani.
Alichoamua nikuwaamuru kujirusha ndani ya mto uliokuwa ukipitisha maji chini ya daraja walilokuwa juu yake.

Sajini Kebu na wenzie wakagoma.

Honda nae ili kuonesha msisitizo akaamua kumpiga mmoja wao risasi ya mguu na kitendo bila kupenda askari wote wanne waliokuwa hai wakajirusha ndani ya mto ambao haukuwa mrefu sana.

Baada ya kuhakikisha hawatakuwa na madhara tena kwake, haraka Honda akakimbia hadi ilipokuwa gari ilokuwa imewafikisha pale na kabla hajafanya lolote akachingulia ndani yake na kuona funguo ipo pahala pake.

Akatabasamu!!

Kisha akafika ulipokuwa mkoba na kuuchukua na kuyafuata makaratasi mawili yaliokuwa yamepeperuka huku na huko.
Akataka kuondoka, akasita.

Kidole!

Aliangaza macho yake huku na huko,haikumchukua muda akakiona.
Akainama kukiokota.
Akasita tena.
Kilikuwa ni kidole cha ajabu sana,kilikuwa kimepasuka pasuka kuota sugu.
Kwa haraka ungelikitizama ungehisi ni kidole cha sokwe.
Akainama kukiokota tena.

Hakufanikiwa!

Nyuma yake alikuwapo mtu na uwepo wake aliuhisi lakini kabla hajafanya lolote akajikuta akipokea teke kali lililomtupa chini kama mzigo na kabla hajasimama akashindiliwa tena teke jingine mgongoni.
Kwa uzito wa mateke yale akaona akilemaa basi ataumia zaidi na pia hakutaka kujichosha sana kwa mapigano wakati bado anasafari ndefu ya kufuatilia kifo cha Bulembo na Balozi Aly Sapi.
Akajinyanyua kwa mtindo safi ila kabla hajakaa sawa akajikuta tena akijaa kwenye anga za mvamizi.
Ila sasa alimuona.

Honda akatabasamu tena, huku akilini akijilaumu kwa kushindwa kumkumbuka dereva wa Land Rover ile ya kipolisi, sasa ndie alikuwa amesimama kukabiliana nae.

Mchoro ukachorwa, huku kila mmoja akijaribu kumsoma mwenzie namna anavyojongea.
Ulikuwa ni mviziano wa akili.

Honda akanesa kwa mtindo wa kidalipoo, kisha akasubiri kwa sekunde bila kufanya maamuzi na ni wakati huo alipoona matunda ya hila zake.

Mvamizi alimfuata Honda kwa kasi ya umeme huku akiunguruma kama bweha, lakini akakutana na hewa kisha akaambulia maumivu ya mbavu za kushoto.

Ngumi ya Honda ilileta matunda chanya.

Wakati mvamizi akijikunja kuugulia maumivu ni wakati huo ambao Honda alienda juu kisha akarudi kwa kutanguliza mguu mmoja mbele na alipotua tayari alikuwa juu ya shingo ya mvamizi na kumsambaratisha chini kwa kutanguliza uso.

Mvamizi alipigwa cub ya Seth Rollins! Hakuwa na uhai tena, na hata angelikuwa nao shingo na uso vingekosa mawasiliano kwa miaka kadhaa.

Honda hakutaka kupoteza muda zaidi akakiota tena kidole kisha akakitia ndani ya mkoba na kuliendea gari la polisi na kutokomea kurudi Kinshasa huku nyuma akiwaacha Sajini Kebu na wenzie wakifanya jihada za kutoka chini ya daraja.

****

Katika watu waliokiwa wamevurugwa kwa wakati huo ni Kizibo na mpambe wake Kojo.
Na hii ni baada ya kupewa taarifa ya kutoroka kwa Honda mikononi mwa Sajini Kebu, na sasa walipewa kazi ya kumsaka katikati ya mji wa Ivuba na Kinshasa kiujumla.

Mapumziko yalitumbukia nyongo mchana kweupe!

“Dah hata kabla sijatuliza maumivu ya kipigo cha yule bwege narudi….” Alilalama Kojo huku akipunguza mwendo wa gari walilokuwamo.

“Acha uoga komredi,umeanza lini kugwaya mkojolea pembeni eeh” alimaka Kizibo huku akimkata jicho la fedheha swahiba wake.

“Wewe hujui tu,yule jamaa anapiga hadi mitindo ya mieleka aisee” alisema Kojo huku akisimamisha gari karibu na supermarket ya Grace market.

“Nini!” aliuliza Kizibo baada ya kuona gari inasimama.

“sasa kusimamisha gari tu unagwaya ukimuona je!” alijibu Kojo kwa lugha ya dhihaka huku akitizama lango la kuingilia ndani ya supermarket ile na hapo ndipo Kizibo nae akaamua kuangalia huko.

“eeh huyu bwege kafika saa ngapi huku” alijisemea taratibu Kizibo huku akisukutua ncha za meno yake kwa kutumia ulimi.

Hata!

Kizibo hakukubali kuendelea kuteseka ndani ya nafsi yake, akashuka ndani ya gari huku akipapasa usawa wa kitovu cha tumbo lake, alipohakikisha bastola yake ipo pahali salama, akafunga mlango wa gari na kuvuka barabara kisha kwenda kule alikokusudia.

“Hii gari imefikaje hapa!” Kizibo alijesemea huku akiangaza huku na huko kuona kama atamuona mtu anaehisi kuifikisha pale ile gari Land Rover ya kipolisi ambayo dakika chache nyuma walitarifiwa ilikuwa na mtuhumiwa wao Honda.

Alah!

“Sasa hapa kafika saa ngapi na yuko wapi?” alizidi kujiuliza Kizibo huku akilizunguka gari lile la kipolisi kwa umakini wa hali ya juu.

Akiwa bado analizunguka ,mara akasikia ving’ora vya gari la polisi likielekea pale haraka akavuka barabara na kurudi ndani ya gari.

Akajikuta yuko peke yake.

“sasa huyu bwege nae..” hakumalizia kauli yake mara mlango wa dereva ukafunguliwa akaingia Kojo huku usoni akizidi kuvimba zaidi ya mwanzo.

Hii kali!!

“hee komredi, kwani ulienda chokonoa mzinga wa nyuki tena!?” aliuliza kwa kushangaa Kizibo.

“Bora hata Nyuki, aisee” alisema Kojo huku akijaribu kuwasha gari lao.

“Aah mzee hebu tulia kwanza, umevimba hivyo huko mbele utaona kweli” alisema Kizibo huku akipeleka mkono ulipo ufunguo ili kumzui Kojo asiwashe kisha akauliza

“Kwani vipi umegongwa na nini tena?”

“Nilikwambia yule jamaa sio aisee,yani unatoka tu na yeye anakuja hapa dirishani na manati ya mzungu, sikuwa na namna kiukweli!”

Midomo ikamwanguka Kizibo.

Akabaki amezubaa kama mgeni aliepigwa denda na mtoto mchanga.

“ina maa…” kabla kizibo hajamalizia; Kojo akadakia

“jamaa kaniteka aisee,”

“Halafu!,”

“Halafu nini wakati unaona usoni matokeo yake!” aling’aka Kojo.

“Ukaumwaga tena” Kizibo akasema huku sasa akibinua kiti alichokalia.

Alichoka!

****

Wakati analiacha pori walilokuwako, Honda aligundua walikuwa wametembea zaidi ya kilomita ishirini na pale walipokuwa, walikuwa ni karibu na mpaka wa kuingia mji mdogo wa Ben ulioko kilomita thelathini kutoka Kinshasa.

Aliamua kutembeza Land Rover kama kichaa alietoroka Milembe na ndani ya nusu saa tu alikuwa ameingia Kinshasa na wakati akiwa kwenye barabara ya RTe Matadi ndipo alipoamua kuegesha gari karibu Grace supermarket.

Mwanzo aliona ni muhimu yeye kupitia chakula cha kopo pale ambacho aliamini kitamfaa mbele ya safari.

Lakini wakati anatoka ili achukue usafiri mwingine na kulitelekeza gari lile pale, akili nyingine ikampa ushauri na akaamua kuufuata.

“ili nifikie majibu haraka, yanipasa kukutana na mtu wa kwanza kulisogelea lile gari” alijiwazia baada ya kuhisi taarifa zake tayari zimewafikia wabaya wake na ambao watakuwa wanalisaka gari na dereva wake.

Akaamua kukaa upande wa pili wa barabara kulikokuwa na harakati mbili tatu za kuwaingizia watu kipato.

Subira yake haikuchukua muda ikawa heri.
Macho yake yakaliona gari jeupe aina ya Toyota Camry ikipaki, kisha akaona watu wawili wakijadili kitu na mmoja akashuka kuliendea lile gari la Polisi.

Hakutaka kungoja sana.
Alimhitaji aliesalia ndani ya gari.
Akapiga hatua na kulifikia gari,akagonga mlango huku bastola ikiwa mkononi mwake na bila kutarajia dereva akashusha kioo.
Pengine hakuwa ameiona bastola.

Hamadi!!!

Akaiona sura mbaya yenye kovu kubwa upande wa kushoto,alikuwa ni yule mtu mwenye ulimi mbaya aliepambana nae ahsubuh nyumbani kwa Bulembo.

Aisee!

Hakuwa na namna zaidi alimuamuru ashuke ndani ya gari nae mtu mbaya akatii.

“Tujifanye marafiki, tuelekee kulee!” alisema Honda huku akimpa ishara ya macho kuelekea upande wa pili kulikokuwa na uchochoro ambao uliufuata ungekufikisha kwenye kituo cha kujazia mafuta cha Total.

Wakaongozana kama mtu na rafiki yake.
Kojo mbele; Honda nyuma.

“Nani anawatuma?” aliuliza Honda.

Kimya!!

Honda akaona muda si rafiki,akaikoki bastola yake na tayari walikuwa wameingia ndani ya kichochoro hicho.

Lakini kabla Honda hajatimiza azima yake mara wakatokea vijana wawili waliokuwa wakikimbizana huku wakipiga kelele.

Kojo akajua lazima Honda atakuwa kazubaa nyuma yake nae hakutaka kufanya kosa.

Akaruka sarakasi moja kavu kwa kwenda mbele huku nyuma akisikia mlio mdogo wa chafya,akajua kakoswa na risasi.
Nae akataka amuoneshe Honda ni mjuzi wa hizo kazi.
Akageuka haraka kama tiara na kuipangusa bastola mikononi mwa Honda kisha akamshindilia konde usawa wa juu kidogo mwa jicho la kushoto.

Honda akarudi nyuma hatua kadhaa huku akiyumba.
Punde akamuona Kojo anamfuata kama Ngiri katikati ya mbio na Simba.
Akacheza kidogo na kumkwepa kisha akaunasa mkono uliokuwa unakuja kumshambulia, akaruka kurudi nao nyuma kisha akaachia makonde mawili ya harakara usoni kwa Kojo huku bado akiwa ameushika mkono wa Kojo, kisha akarudi nao kwa kasi huku akiwa amepinda mkono wake wa kuume na kiwiko kikakajaa tena usoni kwa Kojo na kumuacha akiyumba huku na huko bila kupata muhimili sawia.

Honda hakutaka kuchelewa,akaruka kwa mtindo wa flying kick na kumtandika Kojo mateke mawili ya kifua na kumwacha akisambaratika chini kama gunia la Karanga.

Honda alisimama wima huku akirekebisha mkoba wake na hapo masikio yake yaliponasa sauti mbili tofauti .
Sauti ya kwanza ni ya mwanamke aliekuwa anapita kichochoro kile na sauti ya pili ilikuwa ni ya king’ora cha polisi.

Akabaki njia panda.

Ni hilo ndo lilikuwa kosa lake.

Akashangaa akipigwa mtama safi kabisa uliompeleka chini bila kupenda na alipotaka kunyanyuka hakuamini macho yake.

Alishuhudia Kojo akiumwaga kwa mbio za sungura jangwani.

Hakumfuata!!

Akatokomea kuwahi sehemu nyingine aliohisi itampa majibu.
 
Safi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom