Jarida la Sani limerudi sokoni

mkuu utakua umesahau, mi nakumbuka timu hizo zilikua sani
Huyu mtoto wa juZi alihadisiwa tu huyu, bush star na born town .. Kina hui hui hawajawahi kigusa mpira hata mara moja toka azaliwe ila namba yake ipo . Dadeki.
 
Huyu mtoto wa juZi alihadisiwa tu huyu, bush star na born town .. Kina hui hui hawajawahi kigusa mpira hata mara moja toka azaliwe ila namba yake ipo . Dadeki.
Nilikua naburudika sana wakati wa maandalizi ya mechi kali kati ya watani hao wa jadi, yani kila timu inakwenda kwa mganga ila mambo ya huko sasa daaa!
 
Ladha ni ileile.
Ladha haiwezi kuwa ile toka alipokufa John Kaduma ambaye alikuwa mchoraji mkuu ladha ilianza kupotea, hata watunzi siyo wale wa zamani mf kumbuka wimbi la kitintale, visa vya betina n.k. Ngoja nitanunua nione km kuna mabadiliko mana lilishapoteza mvuto.
 
mkuu hata mi nna wasiwasi, ladha haiwezi kua ileile unless kama wale wachoraji wake wa zamani watakuepo japo wawili au watatu
 
Jarida lako pendwa la SANI lipo mtaani sasa, kila Alhamis.
Unazikumbuka Story za Madenge, Kifimbo cheza, Mzee Fukunuku, Zena na Betina. Lodi Lofa, Sokomoko, Pimbi n.K.

Usiwakose leo kwenye Jarida la SANI kwa Tsh.1000 tu.

Haliwezi kuwa kama lile la enzi hizo
 
mbona silioni sokoni jamani...nielekeze kwa huku karakoo na posta na mwenge ni kitaa kipi naweza liona nimeangaza macho tangu mwenge hadi kkoo hola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…