Jarida la Africa Events Kutoka Maktaba Lipo Katika Kavazi la Dr. Salim Ahmed Salim

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
JARIDA LA AFRICA EVENTS KUTOKA MAKTABA LIPO KATIKA KAVAZI LA DR. SALIM AHMED SALIM

Hiki kisa nimepata kukieleza siku za nyuma na hivi karibuni nilipokuwa naandika kuhusu uzinduzi wa Kavazi la Dr. Salim.

Mke wangu alikuwa katika Tume ya Warioba ya Katiba pamoja na Dr. Salim Ahmed Salim.

Siku moja nilimsindikiza mke wangu nyumbani kwa Salim tulipofika mimi nikaamua kubakia kwenye sehemu ya kuegesha magari mke wangu akaenda kumuona Dr. Salim.

Nilikuwa na gazeti la Africa Events ambalo jalada lake ilikuwa na picha ya Dr. Salim likimnadi kama: Africa's ''Super Person.''

Picha hii ilikuwa ya kuchora na ilipendezesha sana toleo lile.

Kabla ya kutoka nyumbani nikachukua gazeti lile kutoka Maktaba nikampa mke wangu nikamwambia ampe Dr. Salim kama zawadi kutoka kwangu nikimwambia mke wangu huenda ikawa hili gazeti yeye hana.

Mke wangu akampa gazeti lile na walipomaliza shughuli yao akaja mmoja wa wasaidizi wa Dr. Salim pale nilipoegesha gari langu na nadhani ni kati ya walinzi wake aliyetupokea akanikaribisha akiniambia nimfuate nikamsalimu Dr. Salim.

Hivi ndivyo nilivyokutana na Dr. Salim kwa mara ya kwanza na kuzungumza na yeye.

Nilimuomba tupige picha.

Nakumbuka kitu nilichomwambia ni yeye kuandika historia ya maisha yake.

Leo wakati naangalia uzinduzi wa Kavazi la Dr. Salim kwenye televisheni nikamsikia January Makamba akisema kuwa katika Kavazi la Dr. Salim kaikuta barua yake aliyomwandikia Dr. Salim miaka mingi sana nyuma.

Nilipoyasikia maneno haya ikanijia fikra kuwa huenda na lile gazeti nililompa Dr. Salim likawepo katika Kavazi.

Maneno yangu hayakuanguka chini.
Mpenzi msomaji wangu tazama hapo chini:

1696103018477.png

1696103054406.png

Kwa kiswahili chepesi "kavazi" lina maana gan???

Ingekua poa km ungetuwekea picha ya barua ya January
 
Hongera Mkuu tumeona kipenzi chako. Wa ujanani au wa ngapi huyo bi mkubwa?
 
Back
Top Bottom