Simba zee 33
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 1,374
- 1,558
Wewe umesikia mbili tuKadiri kampeni zinavyodhidi kunoga ndio kila siku tunazidi kusikia kila aina ya tuhuma, tuhuma ambazo wagombea urais wanaona zinaweza kuwapa kete ya kupata kura.
Akiwa Kamachumu mkoani Kagera mgombea wa urais kwa kupitia Chadema ametoa tuhuma ambazo kwangu mimi naona kama zinahitaji kupatiwa majibu. Maana kwa taifa kama Tanzania ambalo linafuata misingi ya katiba na sheria tuhuma kama hizi ni kama nchi yetu inachafuliwa, japokuwa ni kipindi cha kampeni. Sheria ya uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanataka wagombea wawe wanakosoana kwa sera au hoja ambazo zina ukweli, sio uzushi.
Akiwa Kamachumu Lissu amesikika akidai kuwa serikali ya CCM ilitaka kumuua mwandishi wa habari Ansbert Ngurumo ndio maana akakimbilia ughaibuni, pia amesisitiza walewale waliompiga risasi na kumfanya awe kilema ndio waliotaka kumuua Ansbert Ngurumo.
Hizi tuhuma kwa Taifa letu ambalo limesaini mikataba mingi tu ya kimataifa kulinda haki za raia wake na hata kwenye katiba ya JMT haki ya kuishi imetambuliwa wazi, sio tuhuma nzuri na zinalichafua Taifa letu.
Kwa hiyo Serikali kukaa kimya bila kukanusha au kuzitolea ufafanuzi, tuhuma hizi zinalipaka matope Taifa letu na huenda zikaaminiwa na watu kuwa ni kweli.
Hivyo kama ambavyo imekuwa ikitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yanayopotoshwa, hata juu ya hizi tuhuma tuambiwe kama ni kweli au si kweli.
Mbona zipo nyingi tu ikiwemo Mtoto wa dadake pombe kuidhinisha peke yake mabilioni ya pesa kujenga uwanja
Uwanja wajengwa na mume mwenza bila zabuni
Kila sehemu mayanga construction company
Kujimilikisha ranch watu kuuawa na kupotezwa
Mbona mambo ni mengi wewe unatoka Tanzania gani?
Yaani kwa sababu media inebanwa sio kama wakati wa mkwere tungesikia mengi