Uchaguzi 2020 Japokuwa kukaa kimya ni jibu, Serikali inatakiwa ijibu hizi tuhuma

Kadiri kampeni zinavyodhidi kunoga ndio kila siku tunazidi kusikia kila aina ya tuhuma, tuhuma ambazo wagombea urais wanaona zinaweza kuwapa kete ya kupata kura.

Akiwa Kamachumu mkoani Kagera mgombea wa urais kwa kupitia Chadema ametoa tuhuma ambazo kwangu mimi naona kama zinahitaji kupatiwa majibu. Maana kwa taifa kama Tanzania ambalo linafuata misingi ya katiba na sheria tuhuma kama hizi ni kama nchi yetu inachafuliwa, japokuwa ni kipindi cha kampeni. Sheria ya uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanataka wagombea wawe wanakosoana kwa sera au hoja ambazo zina ukweli, sio uzushi.

Akiwa Kamachumu Lissu amesikika akidai kuwa serikali ya CCM ilitaka kumuua mwandishi wa habari Ansbert Ngurumo ndio maana akakimbilia ughaibuni, pia amesisitiza walewale waliompiga risasi na kumfanya awe kilema ndio waliotaka kumuua Ansbert Ngurumo.

Hizi tuhuma kwa Taifa letu ambalo limesaini mikataba mingi tu ya kimataifa kulinda haki za raia wake na hata kwenye katiba ya JMT haki ya kuishi imetambuliwa wazi, sio tuhuma nzuri na zinalichafua Taifa letu.

Kwa hiyo Serikali kukaa kimya bila kukanusha au kuzitolea ufafanuzi, tuhuma hizi zinalipaka matope Taifa letu na huenda zikaaminiwa na watu kuwa ni kweli.

Hivyo kama ambavyo imekuwa ikitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yanayopotoshwa, hata juu ya hizi tuhuma tuambiwe kama ni kweli au si kweli.
Wewe umesikia mbili tu
Mbona zipo nyingi tu ikiwemo Mtoto wa dadake pombe kuidhinisha peke yake mabilioni ya pesa kujenga uwanja
Uwanja wajengwa na mume mwenza bila zabuni
Kila sehemu mayanga construction company
Kujimilikisha ranch watu kuuawa na kupotezwa
Mbona mambo ni mengi wewe unatoka Tanzania gani?
Yaani kwa sababu media inebanwa sio kama wakati wa mkwere tungesikia mengi
 
Kwa hiyo?
 
Aliyetaka kumuua Lissu ni nani?
tuanzie hapo kwanza..
Viashiria vyote vinaonyesha alietaka kumuua lissu ni Mr Pombe kwa sababu
1,. Masaa mawili kabla ya shambulio alisema watu wanaosema Sana kuhusu mikataba hawastahili kua hai
2. Wakati yupo Hoi walililazimisha apelekwe muhimbili wakakataa kumpeleka Nairobi wala ubalozi haukujihusisha na lolote
3. Mpaka Leo Tanzanian na Kenya hatuna mahusiano mazuri wakenya ealijitolea lissu alindwe na jeshi la Kenya
4. Pombe kwa maksudi alikataa kuidhinisha pesa ya matibabu yake
5. Yeyote alieenda hospitali kumjulia hali lissu pombe alimchukia
6. Alisema vita vya kiuchumi ni vibaya Sana
 
Kwa hio ujue kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tunaongozwa na dikteta maswali ni mengi kuliko majibu
Labda jaribu kumtafuta msemaji mkuu wa serikali umuulize
Yumo humu JF ndio maana hoja kibao zinazochangiwa humu huwa anazijibu. Leo hujaona anatoa ufafanuzi juu ya miradi inayotekelezwa na mapato yake? Kwa hiyo hata hili nalo atoe majibu.Kweli Ansbert alitaka kuuliwa na wale waliompatia ulemavu Lissu?
 
Mkuu, ilishaelezwa na Mzee wa Msoga kwamba akili za kuambiwa changanya na zako.

Tusubiri uchaguzi ufike tupige kura kwa kutumia akili zetu, baada baada ya kuwasikiliza wote. Na utasikia mengi kipindi hiki, maana tuliambiwa kuwa hata ndege za ATCL ni mitumba, na tena tukaambiwa kuwa bajeti ya ununuzi ndege hizo haikupita bungeni. Lakini tulivyochanganya na akili zetu kwa kutumia teknolojia tulienda kwenye hansard tukamuona mbunge wa Kawe akichangia hoja hiyo ya fedha zilizotengwa kwa miaka miwili mfululizo kwa ajili ya ununuzi wa ndege.
 
Lakini uongo ukivuma sana hugeuka ukweli,huu uongo lazima serikali iukanushe. Maana ni taswira mbaya kwa taifa letu.
 
Jeshi la polisi kila siku inamsikia Lissu akizungumza na kuituhumu kuhusu shambulio lake ,wao wametulia na wakati ndo wanaochafulia ,polisi wanazo ripoti hazifanyiwi kazi ,kama wao hawahusiki kwanini wasishughulikie wakati ndo wanaochafulia ,wangekuwa hawahusiki na hilo tukio ungeona wako busy kufanya uchunguzi kama manesi wa zamu
Mambo mengine yapo wazi ila kuna watu Wana roho za kishetani
Wanajaribu kujificha kwenye kimvuli Chao
 
Viashiria vyote vinaonyesha alietaka kumuua lissu ni Mr Pombe kwa sababu
1,. Masaa mawili kabla ya shambulio alisema watu wanaosema Sana kuhusu mikataba hawastahili kua hai
2. Wakati yupo Hoi walililazimisha apelekwe muhimbili wakakataa kumpeleka Nairobi wala ubalozi haukujihusisha na lolote
3. Mpaka Leo Tanzanian na Kenya hatuna mahusiano mazuri wakenya ealijitolea lissu alindwe na jeshi la Kenya
4. Pombe kwa maksudi alikataa kuidhinisha pesa ya matibabu yake
5. Yeyote alieenda hospitali kumjulia hali lissu pombe alimchukia
6. Alisema vita vya kiuchumi ni vibaya Sana
7. Wakamnyima kulipia matibabu yake
8. Wakamnyima kumlipa mshahara
9. Wakamfuta na ubunge
 
Sio kweli,ardhi huwa haiibiwi,bali inamilikiwa isivyo kihalali. Je hiyo anayosema Lissu, JPM anamiliki kihalalai?
Ukimiliki isivyo halali ndio umeiba gari yangu ukiimiliki wewe isivyo halali ndio umeniibia akili hizi ndizo zilizotufikisha hapa
 
Lissu ni mgonjwa wa akili kila mtanzania ana fahamu! Kama anajua waliotaka kumuua sasa mbona analilia polisi wafanye uchunguzi wakati anajua fika polisi ndio walihusika?

Huyo ni mgonjwa wa akili nafikiri kuna risasi ipo kwenye ubongo wa Lissu!
Mgonjwa wa akili anawakusanya viongozi wote kujibu hoja anazozitoa Mgonjwa wa Akili na hakuna hata mmoja anaejibu badala kujikanyaga tuu hapo ni Nani mgonjwa??
 
7. Wakamnyima kulipia matibabu yake
8. Wakamnyima kumlipa mshahara
9. Wakamfuta na ubunge
Naomba nyie wazandiki msitake kuharibu mada niliyoanzisha. Mimi nataka tupate ukweli, Lissu ni mkweli? Au sio. Serikali itoe ufafanuzi kwa manufaa ya taifa. Sio hayo mnayotaka kuongeza chumvi hapa.
 
Naomba nyie wazandiki msitake kuharibu mada niliyoanzisha. Mimi nataka tupate ukweli, Lissu ni mkweli? Au sio. Serikali itoe ufafanuzi kwa manufaa ya taifa. Sio hayo mnayotaka kuongeza chumvi hapa.
Tumekusifia uzi mzuri, sasa kwa nini utuite wazandiki?
 
Back
Top Bottom