Uchaguzi 2020 Japokuwa kukaa kimya ni jibu, Serikali inatakiwa ijibu hizi tuhuma

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kadiri kampeni zinavyodhidi kunoga ndio kila siku tunazidi kusikia kila aina ya tuhuma, tuhuma ambazo wagombea urais wanaona zinaweza kuwapa kete ya kupata kura.

Akiwa Kamachumu mkoani Kagera mgombea wa urais kwa kupitia CHADEMA ametoa tuhuma ambazo kwangu mimi naona kama zinahitaji kupatiwa majibu. Maana kwa taifa kama Tanzania ambalo linafuata misingi ya katiba na sheria tuhuma kama hizi ni kama nchi yetu inachafuliwa, japokuwa ni kipindi cha kampeni. Sheria ya uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanataka wagombea wawe wanakosoana kwa sera au hoja ambazo zina ukweli, sio uzushi.

Akiwa Kamachumu Lissu amesikika akidai kuwa serikali ya CCM ilitaka kumuua mwandishi wa habari Ansbert Ngurumo ndio maana akakimbilia ughaibuni, pia amesisitiza walewale waliompiga risasi na kumfanya awe kilema ndio waliotaka kumuua Ansbert Ngurumo.

Hizi tuhuma kwa Taifa letu ambalo limesaini mikataba mingi tu ya kimataifa kulinda haki za raia wake na hata kwenye katiba ya JMT haki ya kuishi imetambuliwa wazi, sio tuhuma nzuri na zinalichafua Taifa letu.

Kwa hiyo Serikali kukaa kimya bila kukanusha au kuzitolea ufafanuzi, tuhuma hizi zinalipaka matope Taifa letu na huenda zikaaminiwa na watu kuwa ni kweli.

Hivyo kama ambavyo imekuwa ikitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yanayopotoshwa, hata juu ya hizi tuhuma tuambiwe kama ni kweli au si kweli.
 
Taifa linalopakwa matope ni pamoja na wewe, basi anza wewe kumjibu Lissu

Baadhi ya Watanzania ni wapumbavu sana.

Vitendo vya mauaji utekaji wanaoshutumiwa ni viongozi, ninyi mmekazana taifa linatukanwa linapakwa matope

Jibu hili

Jumuia ya kimataifa ikithibitisha tuhuma hizi ni kweli na mahakama ya Hage ikawachukua, na wewe au watanzania wote tutashitakiwa The Hage?
 
Kitendo cha serikali kushindwa kufanya uchunguzi hata wa uongo tu dhidi ya kile kilichomtokea Lissu na wengine, kinainyima haki ya kujitetea unaanzaje kwanza maana kazi ya kwanza ya serikali ni kuhakikisha ustawi wa watu wake,sasa kama watu wanauwawa,watu wanapigwa risasi na serikali haifanyi kitu inaanzaje kwa mfano kujitetea?
 
Hawawezi kutoa ufafanuzi kwa sababu siyo tuhuma bali ndiyo ukweli wenyewe.

Kwani umewahi kusikia ufafanuzi wa:
1) Nani alitaka kumwua Lisu?
2) Nani alimpoteza Saanane?
3) Nani alimpoteza Azory?
4) Nani alimwua Mawazo?
5) Na yule diwani wa Dar, Morogoro, Kigoma?
6) Ambaye amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi amewahi kuhojiwa na yeyote?

Lililo wazi ni kuwa hao wote walikuwa ama wakiikosoa Serikali au Rais.

Taifa halipakwi matope bali Taifa linadhulumika kwa mauaji yanayofanywa na hayawani walioaaminiwa. Na hata wao wauaji hawapakwi matope bali wanaelezwa kwa namna ambavyo wapo.
 
Taifa linalopakwa matope ni pamoja na wewe, basi anza wewe kumjibu Lissu

Baadhi ya watanzania ni wapumbavu sana

Vitendo vya mauaji utekaji wanaoshutumiwa ni viongozi, ninyi mmekazana taifa linatukanwa linapakwa matope

Jibu hili

Jumuia ya kimataifa ikithibitisha tuhuma hizi ni kweli na mahakama ya Hage ikawachukua, na wewe au watanzania wote tutashitakiwa The Hage?
Watanzania sio wapumbavu,mpumbavu ni wewe ambae umeshindwa kufahamu kuwa serikali ndio inayowakilisha watanzania mil 60 ndio inatakiwa kujibu hizi tuhuma. Hata Au au Un wakifuatilia hizi tuhuma za watu kuuwawa ni serikali ndio itawajibishwa,sio kila Mtanzania.
 
Kitendo cha serikali kushindwa kufanya uchunguzi hata wa uongo tu dhidi ya kile kilichomtokea Lissu na wengine, kinainyima haki ya kujitetea unaanzaje kwanza maana kazi ya kwanza ya serikali ni kuhakikisha ustawi wa watu wake, sasa kama watu wanauwawa,watu wanapigwa risasi na serikali haifanyi kitu inaanzaje kwa mfano kujitetea?
Kwa hiyo ulitaka ifanye uchunguzi wa uongo ili idanganye? Tunataka ukweli, wewe vipi?
 
Hawawezi kutoa ufafanuzi kwa sababu siyo tuhuma bali ndiyo ukweli wenyewe.

Kwani umewahi kusikia ufafanuzi wa:
1) Nani alitaka kumwua Lisu?
2) Nani alimpoteza Saanane?
3) Nani alimpoteza Azory?
4) Nani alimwua Mawazo?
5) Na yule diwani wa Dar, Morogoro, Kigoma?
6) Ambaye amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi amewahi kuhojiwa na yeyote?

Lililo wazi ni kuwa hao wote walikuwa ama wakiikosoa Serikali au Rais.

Taifa halipakwi matope bali Taifa linadhulumika kwa mauaji yanayofanywa na hayawani walioaaminiwa. Na hata wao wauaji hawapakwi matope bali wanaelezwa kwa namna ambavyo wapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lissu,Zitto na wapinzani wanachukua hatua gani? Kuongea majukwaani kama Kamachumu? Hii haitoshi wanatakiwa waibane serikali
 
Sasa kama uongo waliompiga risasi Lissu wamekamatwa? Kama huamini mkosowe bwana yule na hakika tutaokota kiloba chako baharini.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Huyo bwana na serikali yake watupe majibu kama ni kweli, au Lissu athibitishe madai yake.
 
Back
Top Bottom