Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 5,277
- 7,994
Ningekufa tena hapohapo kwa maana yote nikiyoyafanya yalikuwa ni USHETANI, na ndiyo maana yamefutwaNawasalimu wana jamvi kwa jina la Jamii Forums. Hayati JP Magufuli hatafufuka. Hypothetically, kama ingekuwa inawezekana kufufuka, na kama ungekuwa wewe ungefanya nini baada ya kufufuka. Je ungemuita Harbinder Setih Singh na James Rugemalira Ikulu na kuwapa nishani au kuwazaba makofi na kuamuru warejeshwe korokoni. Je ungemwambia nini Dkt Bashiru Ally Kakurwa na Hamphrey Polepole bila kusahau Medard Kalemani? Je ungeongeaje na Rais SSH usawa huu? Je ungewaambia nini wamachinga? Je ungeshughulikiaje tetesi kuwa ule ujambazi wa kutisha wa Bandari ya Bagamoyo umehalalishwa? Je ungemteua nani kuwa makamu wako? Je ungeanza kufanya jambo gani? Maswali ni mengi na ni mawazo tu. Naomba kuwasilisha.