japo niridhike... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

japo niridhike...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nyamayao, Nov 12, 2010.

 1. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Ni rafiki yangu kipenzi sana, alikuwa na matatizo ya kumtosha na mume wake, mume alipata hawara akamfanya kama mke wa pili, kamjengea, kamfungulia biashara nzuri, yaani ni kama mke mdogo, wamezaa na mtoto 1, kipindi hicho my frnd alisota sana kwenye ndoa, manyanyaso yote aliyapata, mume aamua acje nyumbani hata week nzima yupo kwa huyo hawara, mume alifanya vituko vya kutosha, my frnd ktk kutaka kujifariji alitokea mfanyabiashara mmoja wakapendana, pendo limekuwa pendo.

  My frnd kasahau kama alikuwa kwenye matatizo ya ndoa, ndani ilikuwa kila mtu anakuja kwa ajili ya kulaza ubavu tu, mwanamke hakuwahi kuonyesha kama ana uhusiano nje, cku ya cku mume akamfumania huyo hawara yake yupo na mwanaume mwingine kwenye nyumba aliyomjengea yeye na kumuwekea kila kitu ndani, kasheshe likawa kasheshe, mume akaamua kwenda kufanya DNA ya mtoto aliezaa na hawara akakuta sio wake, kasheshe likaongezeka....

  Alivyoona hivyo alirudi kwa mkewe na kumuomba msamaha wa kutosha na kumuelezea kila kitu kilichotokea kwa hawara...mke kaamua kumsamehe na kwa maelezo ya mke ni kwamba amejirekebisha sana, ishu ya sasa ni mke na mfanyabiashara, mfanyabiashara nae huku amemjengea mke nyumba nzuri, juzi juzi kambadilishia gari nzuri anawasomesha watoto wa my frnd tangu mume alivyotekwa huko alikuwa hajui watoto wanalipiwaje ada au wanakulaje hapo nyumbani, ni kama ndio aligeuka baba mzazi wa watoto.....

  Mume amekuja dokezwa kwamba mke ana uhusiano na mtu fulani, mume amepeleleza vya kutosha lakini hajapata ushahidi, ni jana jioni mume kamtoa mke wake outing na kumuomba mpaka kumpigia magoti na machozi juu kwamba "japo aridhike" tu amwambie ukweli ili wawewze ku solve kikamilifu matatizo yao waaanze maisha mapya, hawakufikia muafaka coz mke aliendelea kukana, ni asubuhi hii kanical kunipa hii ishu ya kwamba amweleze ukweli au aendelee kukana?

  Mie nilimuuliza tu kama bado anaihitaji hiyo ndoa? alinijibu bado anahiitaji, kwa ushauri wangu nilimwambia kama unahiitaji uckae ukasema ukweli, endelea kukana hivyo hivyo, ni leo maongezi yao yataedelea, wewe kama wewe ungemshaurije huyu dada?
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  dah stor ni tamu na inafundsha saaaaaana nilitaman isiishe yan....wanaume wanazan akikubwaga na kwenda nje utadoda tu bila wengne kukutaman..dah fresh sana jamaa kaipata fresh YA SHAMBA TOKA KA HAWARA...
  FREND WAKO WALA ASIMWAMBIE ..ASIMWAMBIE...CZ uyo bwana hajaomba msamaha kwa kupenda its just bcz hawara KAMTIMUA KWA VTENDO ...na ameona afanyaje sasa?ngoja nimrudie yule wangu....angekuwa amejirud wakat wapo poa na uyo hawara yake apo sawa lakin kujirud uko kwa out of option...kiukweli kamfanya mkewake ni oltenativ afta kubwagwa na hawara
  ASISEME ASISEME..amchek jamaa km amejirud kweli bas apunguze kasi kwa mfanyabiashara....aambatane na mmewe
  DAH MPE POLE LAKIN.
   
 3. F

  Ferds JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nyamayao to be honest ur nt a good friend,ur killing your friend's conciuos, na hapo ndipo ndoa itakapo bomoka yaani wewe ni kama unamshauri shoga yako kulipiza kisasi, kama makosa kila mtu ametenda na sasa ndio wakati muafaka wa kuyamaliza, sasa kama hatamueleza ukweli mumewe.

  Hicho kimbunga chake katrina ni ndogo, na kwa hiyo story inavyoonekana huyo jamaa anapenda mambo ya ukweli , maana hata small house imeachwa kwa kumdanganya jemba, mwambie atoe siri kabla hilo jambo halijapoa , maana hakuna marefu yasio na ncha, cku atadakwa tu, mapenzi kikohozi unajua hilo
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Tena mwambie asije akathubutu kumbwambia jamaa ukweli ni kosa kubwa sana. Akae kimya tu atafute njia ya kuweza kuachana na mfanyabiashara maana kama mumewe kajirekebisha basi amsamehe sababu wanaume ndivo walivyo. Ila kucheki HIV muhimu asije akawa kamletea maradhi bure.
   
 5. F

  Ferds JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  MH , huyu nae ni wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa!!!!!!!!!!
   
 6. F

  Ferds JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  Msamaha wa kweli unakuja kwa kuzaliwa upya kwa kila mmja kutubu madhambi yake na kuacha no stone untouched ktk past life, muwe wapya kila mmja atamjua mwenzie ujinga wake upo wapi. kweli wanawake ni wakatili, yaani hata kama mtu kajirudi hamsamehi
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Kumsamehe amsamehe ila wanaume wakiambiwa ukweli masimango utakayopata utajuta kuzaliwa mie nakwambia ukweli.
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ..ahh APANA NYAMAYAO HAJAMSHAURI FREND AKE KULIPIZA KISASI EBU CHEK FRESH STOR
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kaka nimemwambia kile ambacho hata mie kingenitokea ningekana tena kwa nguvu zote, hapa hakuna mwenye uhakika kama ni kweli mume atavumilia kujua kwenye miaka miwili mke alikuwa hamuulizi mbona haurudi nyumbani, mbona mume wangu unanifanyia hivi na vile, kile kilio kilipoozwa na mfanya biashara, sasa huyu mume ataukubali ukweli kwamba kipindi chote hicho mke alichokuwa haulizi lolote juu ya mumewe ni kwamba alipatikana mtu wa kumzibia pengo mpaka kumlisha na kusomesha wanae?

  ...kama ingekuwa ni rahic hivyo bac ningemshauri aseme ukweli,na kinachomuumiza zaidi mume ni kwamba anajua jamaa ni "kaizer"...mnafahamiana kimjini mjini, uhakika unatokea wapi sasa kwamba kaizer ndio mwnyewe?amepeleleza mpaka amechoka.
   
 10. F

  Ferds JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Co wote dena amsi, Iam a man na napenda kuambiwa ukweli,hebu toa hizo preconcieved ideas kichwani mwako,kama mtu amebeg for the truth c dhani kama anataka jingine zaid ya suluhu ya kweli
   
 11. RR

  RR JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Dear Nyamayao,
  Kwanza umeandika paragrafu ndefu kupita uwezo wa macho yangu kusoma vizuri...
  Swali moja dogo...huyo rafiki yupo radhi kuachana na huyo mfanyabiashara wake?
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Ulishawahi kuona mtu anapenda kuambiwa uongo au kudanganywa wewe uliona wapi. Hapo haambiwi ukweli mtu hata kwa ncha ya upanga. Hasemi ila aachane na mfanyabiashara wewe acha mchezo kabisa wanaume wanapenda kuiba lakini kuibiwa BIG NOOOOO
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Duh wanawake bana, huku keshachakachuliwa na mfanyabiashara mashuhuri (sijui mwarabu ama muhindi?) kule mtoto siyo wake (sijui wa kichina?) matatizo kweli

  Sijui hata kama walikumbuka kupima ukimwi waliporudiana
  Kasheshe kweli uuuuuuuuuuuuuuuwwwwwwwwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 14. F

  Ferds JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nyamayao ki ukweli reaction ya mtu inategemea na jinsi ulivyopresenti hiyo matter mbele yake, tena kama ni mwanamke ni rahisi sana kuiwakilisha kwa mmeo, ni kuiwakilisha ktk wakati muafaka tu , kingine, ni bora areact ktk wakati huu ambapo naye anakisingizio kuliko wakati mwingine
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  my frnd anasema mfanyabiashara ni muelewa alivyomuelezea kuhusu yaliyotokea mwenyewe akamwambia wapumzike kidogo upepo mbaya upite lakini sio kuachana na mke hataki kuachana na mfanyabishara kwa amdai kwamba alimsaidia sana ktk kumrudisha kwenye hali ya ubinadamu kipindi kile cha matatizo, sasa unajua y mume hajapata uhakika mpaka sasa? coz mfanyabiashara kasema tupumzike kwanza lakini mawacliano kama kawaida, matatizo yake yanatatuliwa kama kawaida, yaani ni kwamba ni k2 kimoja watakimc kwa wakati huu lakini vingine vyote mambo yanaendelea kama kawaida, ni jana tu ametoka ku deposit ada ya mtoto ya skul.
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,415
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  hapo ndoa hamna mie nakwambia wameshaachana hao ila tu wanaishi kwa kuwa wana watoto ila dakika yoyote ndoa yao inavunjika rasmi, huyo m/ume atakapoambiwa ukweli ndio mwisho wa ndoa, na hao wote ni wakosefu wakubwa sana hakuna mwenye nafuu. Siku zote malipo ya dhambi uwa hapahapa duniani na si mbinguni na watalipwa hao hapa hapa duniani

  halafu hao nao ni wanaume wa wapi wanapojengea nyumba w/wake ovyo ovyo bora huyo wa nyumba ndogo (m/ume) alijenga labda kwa kufikiri anajenga kwa ajili ya mtoto ila huyo anayemjengea nyumba mke wa mtu ndio hana akili hata punje maana kuna siku ya siku mambo ya kitibuka unaweza kutolewa uhai bila hata kupewa sekunde ya kutubu

  Imagine unakuta mkeo kajengewa nyumba na mwanaume mwingine tena ndani ya ndoa na nyumba ni mali ya mkeo halafu bado mko kwenye ndoa na jamaa aliyemjengea bado yupo, nakwambia kwa hilo hapatakalika na wala ndoa haitakuwepo tena hapo ni ugomvi tena mpaka mauaji yanaweza kutokea

  Ushauri: Mwambie huyo rafiki yako aombe talaka au ajiandae kuondoka nakwambia hiyo ndoa itakuwa na mwisho mbaya sana na mpaka mauaji yanaweza tokea hapo utakuja tuambia siku moja na huyo mwanaume kuna kitu kinaendelea kichwani mwake sio bure tu
   
 17. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  et kajirud..kajirud afta machafuko ya awala?
  unajua kujirud weew?unajirud katika fare ground ...thats upo poa na hawara yako sema tu unasemayatosha nw naenda kumwangukia mke wangu...apo sawa lakin si km ivi kajirud afta kubaraswa kwa vitendo na hawwara:nono::nono::nono:
  yaaan km vile mlev anakwambia ...KUANZIA LEO NIMEACHA POMBE wakat ameishiwa hana ata sent ..wat do u thk akizipata?i nia kaitoa kwa dhat au out of option?
  aahh mazingira ya msamaha ndo yananitatiza jeee km wangekuwa hawajagombana na hawara yake akili ya kumrudia mke wake ingekwepo??????????????THK TWCE
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  pole my luv....hapana! hapana coz anasema mume amerudi home baada ya kilichomtoke huko, kama kicngemtokea bac acngerudi, so hana imani nae japo amesema amemsamehe ili watoto waite dady hapo ndani.
   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  rose hebu mwambie bwana huyu hajui maumivu yake. Mie nashangaa kujirudi baada ya small house kuharibu? Kasemi mtu hapo bwana
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nyamayao ngoja nipate gahawa nitarudi baadae.
   
Loading...