Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,146
- 13,216
Japan imezindua chombo cha anga za juu ambacho kitabeba mtambo maalum wa kukusanya taka kutoka anga za juu.
Chombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700 (nusu maili) ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo. Nyaya hizo zitaundwa kwa madini ya aluminiamu na chuma cha pua.
Mtambo huo umeundwa kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya uvuvi.
Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande 100 milioni vya taka kwenye mzingo wa dunia.
Vipande hivi ni pamoja na vipande vya setilaini zilizoacha kutumika, vifaa na vipande vya roketi.
Vipand vingi kati ya hivi vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa (maili 17,500 kwa saa) na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.
Taka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kuruka kwenya anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957.
Mgongano kati ya setilaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya setilaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu.