Japan yatuma mtambo wa kufagia anga za juu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
_84676492_s8000040-space_debris,_artwork-spl.jpg


Japan imezindua chombo cha anga za juu ambacho kitabeba mtambo maalum wa kukusanya taka kutoka anga za juu.

Chombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700 (nusu maili) ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo. Nyaya hizo zitaundwa kwa madini ya aluminiamu na chuma cha pua.

Mtambo huo umeundwa kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya uvuvi.

Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande 100 milioni vya taka kwenye mzingo wa dunia.

Vipande hivi ni pamoja na vipande vya setilaini zilizoacha kutumika, vifaa na vipande vya roketi.

Vipand vingi kati ya hivi vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa (maili 17,500 kwa saa) na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.

Taka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kuruka kwenya anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957.

Mgongano kati ya setilaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya setilaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu.
 
Watume Na mtambo wa kukusanyia hewa ukaa huko anga za juu kwa kuwa hilo ndiyo tatizo kubwa zaidi linalosababisha mabadiliko makubwa ya tabia nchi kote duniani!
 
Sisi tunaruka na ungo - bila source of energy wala nini. Yaani tuna-mute kanuni zote za Fizikia haooo tunakwenda zetu. Sema tu usafiri wenyewe mpaka uwe uchi huku umejisiriba mihirizi na mavibuyu (Mshana Jr upo?)

On a serious note hawa wenzetu wako mbele mno. Utafikiri siyo sayari hii hii moja tunayoishi. Hii ngozi nyeusi hii we acha tu! Imagine wenzetu wanakwenda anga za juu kusafisha taka sisi tunaua albino ili tutajirike. Imagine that !!!
 
Wafanye yooote
Ila watambue Mungu yupo

Kwa hiyo wewe unataka Mungu afanye hiyo kazi ya Kukusanya hizo taka?Mungu akichukua jukumu hilo wewe kazi yako itakuwa ni nini?Hiyo pumzi na majaliwa mengine kama Chakula,Mavazi na Malazi sharti uvilipie.Wajapan wanaelewa wajibu huo na ndio wanatimiza wajibu wao.Wewe kaa hapo usubirie Mungu aje "azoe" taka za angani! Kwanza Yeye ndo kaziweka?
 
Hawa sasa wanaprove wrong ile myth eti "all human beings are equal". Proved to be FALSE.
We nawe. All humans are equal imesimikwa kwenye mahitaji yao ya msingi - chakula, hewa, kifo, haki ya kuwa na furaha, uhuru na mengineyo; na kamwe siyo mambo haya ya bandia kama tofauti za kiuchumi, kiteknolojia na ..... Usichanganye madesa mkuu!
 
We nawe. All humans are equal imesimikwa kwenye mahitaji yao ya msingi - chakula, hewa, kifo, haki ya kuwa na furaha, uhuru na mengineyo; na kamwe siyo mambo haya ya bandia kama tofauti za kiuchumi, kiteknolojia na ..... Usichanganye madesa mkuu!
If so, was supposed to read "... are partially equal". Teknolojia mambo ya bandia? Watu wana brains za ajabu unasema bandia? Ni brains zilizowafikisha hapo walipo; brains ambazo hata sisi tunazo lakini hatufiki huko means human brains are not equal and therefore the humans themselves.
 
Back
Top Bottom