Japan yamwaga billion 74 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Japan yamwaga billion 74

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa zaidi ya shilingi bilioni 74 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kupitia Mwenge
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, alisema msaada huo wa fedha utasaidia kupunguza foleni katika barabara hiyo pindi ujenzi huo utakapokamilika.

  Alisema barabara hiyo, ina urefu wa kilomita 12.9 italeta maendeleo na kurahisisha suala zima la usafiri na kuondoa kuwepo kwa msongamano mkubwa wa magari unaosababisha kuwepo kwa foleni.

  Pia alisema upanuzi huo utalazimu nyumba zilizopo kando ya barabara hiyo kubomolewa kwa kuwa mafundi wataingia ndani mita mbili kila upande wa barabara hiyo kuanzia Mwenge, Tegeta hadi Bagamoyo ili kupisha ujenzi huo.

  Alisema wakazi wote watakaobomolewa nyumba zao, watalipwa fidia kutokana na tathmini itakayofanyika kila mtu atapewa fidia yake kwa kigezo cha uthamani wa nyumba itakayobomolewa.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  JE WABONGO WENZANGU TUTATEGEMEA MISAADA MPAKA LINI JAMANI?
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Achalia mbali suala la msaada kinachosikitisha anasema msaada utapunguza foleni kwa hiyo hapo lengo ni kupunguza sio kumaliza, unaona thinking ya watanzania, tunafikia mwisho wa pua hatuende]i mbele zaidi. So in two years time foleni itarudi palepale.

  Halafu Katibu mkuu naye analeta utani kama bosi wake, mkopo in kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kilomita 12.9 halafu yeye anasema barabara itajengwa toka mwenge hadi bagamoyo, kipande ambacho umbali wake ni zaidi ya kilomita 12.9. Hivi watanzania ni lini tutakuwa serious. With this kind of attitute mnadhani kweli tutaendelea???
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni kosa la mwandishi kwa kuwa vyombo vingi vinasema Mwenge mpaka Tegeta(junction ya kwenda wazo hill)......nimepima leo na kupata 12786 metres exactly......ODO reading that is

  Ila nashangaa toka mwenge mpaka morocco pameachwa.....hii si sawa kuvaa suti na kandambili?......
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Imekaa kisiasa zaidi
   
 5. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ukipanua Mwenge mpaka Morogo, gharama itakuwa kubwa sana kutokana na majengo mengi ni ya thamani, na yamejengwa karibu na barabara. Nadhani pengine ndio maana wameamua kupaacha.

  Ni kama kupanua barabara katikati ya posta!
   
 6. W

  WaMzizima Senior Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uko mpango mwingine tofauti kupanua kutoka Morocco hadi mwenge huo ni mradi mwingine. Naaamini tathmini imeshaanza. Kuhusu ngambo Ngali na hoja ya kupunguza badala ya kumaliza foleni hiyo haipo ndugu yangu as long kuna magari foleni itaendelea kuwepo tu suala ni kupunguza kama wanavyodai. Hata LA ambako kuna freeways zenye njia nanenane foleni bado zipo tu ila barabara nzuri husaidia kuzipunguza...
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,460
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Sidhani........wakati Upanga(Ali Hassan Mwinyi siku hizi) Road inapanuliwa,eneo toka Palm Beach mpaka pale Peugeot house kulikuwa na wasiwasi huo lakini waqtaalam waliweza kupanua bila kuweka tuta(island) katikati na leo tunafaidika........hiii ya morocco ni pale Alpha House ndio siasa kibao....wakipanua tu hawa parking.....tukitaka njia nne zitatoka tu mbona tatu zipo na nafasi bado ipo
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Msaada - Msaada - Misaada mpaka lini. Sisi ni omba omba a.k.a TZ - MATONYA.
  Aibu.
   
 9. bona

  bona JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  bilioni 74 inaweza jenga dar mpaka bagamoyo na kulipa fidia?
   
Loading...