Japan yaipa Tanzania mabilioni ya chakula | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Japan yaipa Tanzania mabilioni ya chakula

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, May 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Japan imesaini makubaliano ya kuipatia Tanzania msaada wa Sh. bilioni 14 zitakazotumika kununulia mchele kutoka Japan ili kukabiliana na upungufu wa chakula uliosababishwa na ukosefu wa mvua msimu uliopita.
  Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Balozi wa Japan nchini, Hiroshi Nakagawa, aliiwakilisha serikali ya nchi yake, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi, Ramadhan Khijjah, aliiwakilisha serikali ya Tanzania.
  Khijjah alisema msaada huo utasaidia mambo mbalimbali, ikiwamo kuongeza chakula nchini.
  Vilevile, alisema fedha zitakazopatikana katika mauzo ya mchele huo baada ya serikali kuununua, zitapelekwa katika kilimo cha umwagiliaji. Naye Balozi Nakagawa alisema msaada huo ni sehemu ya misaada, ambayo serikali ya nchi yake inaipa kipaumbele cha kwanza katika maendeleo ya Tanzania.
  Alisema lengo kubwa la Japan kutoa misaada hiyo kwa Tanzania ni kupunguza umaskini na kukuza uchumi, hasa katika maeneo ya kilimo na maendeleo vijijini.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. s

  smilingpanda Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aibu tupu.
   
Loading...