Japan: Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe afariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi

J. Kennedy alipigwa sembuse hyu mstaafu?

Kulindwa hufunikwi kama koti bado utadunguliwa tu.
JFK? Mwaka? Pope naye alipigwa shaba lini?

Baada ya tukio hilo, watu wamewekeza kiasi gani kulinda viongozi? Unadhani ni rahisi kumdungua Biden au Trump wakati huo? Boris? Macron, Putin etc? Au wamarekani wote wanawapenda viongozi wao? Unawasikia jinsi wanavyowapigana shaba kitaa? Mpaka sasa hawajamgonga hata mtendaji wa kijiji tu, iwe mstaafu wa juzi tu wa Japan?

Kwa huu umri wangu huyu ndo kiongozi wa kwanza kusikia kala chuma hadharani.
 
Ndio umeona sasa
 
Na waliokoswa kidogo tu ni Henry Ford na Ronald Reagan.
 

Suala hapa ni ulinzi, yaani hata kama mtu alindwe vipi anapotokea mtu, mtu asiyejali kitu, mtu anayesema; "na liwalo liwe"---hapo mtu huyo anaweza kuua anayelindwa kabla ya yeye kuuawa au kukamatwa na walinzi wa anayelindwa.

Kuhusu Anwar Sadat, yeye aliuawa na askari waliopita mbele yake kutoa heshima katika gwaride kwenye sherehe za uhuru na sio kwamba aliuawa na mlinzi wake, walinzi wake wakati huo walikuwepo kando yake.
 
Ila saadat kama sijakosea alikua bado raia pia kama sijakosea alitunguliwa na mlinzi wake
Anwar Sadat aliuawa na kikosi cha jeshi ambacho kilijiingiza kinyemela kwenye gwaride lililokuwa linapita mbele yake.

Wanajeshi walichukia kwa vile alishafikia makubaliano baina yake na Israel na waarabu hawakupenda kabisa.

Waliona kama amewasaliti wote wale waliopotea kwenye '6 days war'.
 
Sadat aliuawa na kikundi cha kigaidi cha Islamic jihadi kilichochukizwa na mapatano yake ya amani na Israel.
 
Hiyo terminology ya islamic jihad haikuwepo enzi zile.
Ndio walivyojiita na mmoja wao aliyekamatwa na kufungwa muda mrefu kabla ya kuachiwa ni Zawahiri kiongozi wa Sasa wa Al-qaeda na mrithi wa Osama bin Laden.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…