Japan ilifanya kosa kubwa sana kumwachia USA awe mlinzi wake mkuu baada ya kuisha kwa WWII

Mbona nilisikia regan alivyotembelea Japan alionyeshwa mtambo ambao kama marekani ikirusha tena lile kombora la nyuklia inalirudisha mpaka marekani na kulilipulia huko? au ni story za kijiweni. Inasemekana baada ya regan kuonyeshwa hivyo alizimia
 
Japan angefanyaje wakati alishashindwa vita na KUWA incapacitated Kwa atomic? Walimuacha Hirohito kama mfalme asiye na ngumu. Kidogo inafanana na yam zee Mugabe. OKINAWA Kikawa kituo Chao kikuu
 
Japan hakufanya kosa Bali alilazimishwa na hana namna nyingine! Hilo ndilo lilikuwa sharti la kumaliza vita! Kama angekataa alitishiwa kupigwa Bomu jingine la nyuklia! Huu ujinga ndo kiduku hautaki!
 
Unajua Japan wamesave pesa kiasi gani kwa kulindwa 'bure' na USA?? Unadhani Japan ingekuwa hapo ilipo leo kiuchumi kama wangekuwa na 'mzigo' wa jukumu la kuwekeza kwenye ulinzi kama nchi zingine?
 
Mbona nilisikia regan alivyotembelea Japan alionyeshwa mtambo ambao kama marekani ikirusha tena lile kombora la nyuklia inalirudisha mpaka marekani na kulilipulia huko? au ni story za kijiweni. Inasemekana baada ya regan kuonyeshwa hivyo alizimia
Hahaa haaa daahh bangi mbaya Sana
 
Hivi mshaangalia rank ya kijeshi japan anashika namba ngapi?,au germany?.

Kim anatest makombora uelekeo wa japan ,maana huko ndo hakuna jam ya nchi,eneo kubwa ni bahari,

hawezi elekezea uelekeo wa china maana eneo kubwa ni ardhi,ataua watu,
wild thought
 
Sasa nyie watanzania lini mmeanza jua maslai ya Japan wakati hospital tu Hamna na hamlalamiki
 
Ivi unadhani Japan hawawazi kama unavowaza.nadhani aliona Mbali zaidi hadi wakafikia maamuzi hayo.
 
Lilikuwa ni sharti la katika mkataba wa Kumaliza vita, alilazimika kukubali, vinginevyo alitishiwa kutupia Bomu lingine LA nyuklia Tokyo!
Akiamua kuunda jeshi kama LA mwanzo maana yake ni kuwa atakuwa amevunja mkataba wa kuvimaliza vita, kuwa katika vita na marekani moja kwa moja! Hilo haliwezekani!
Kwa mfano Japan wana teknologia tayari ya kuunda Bomu LA nyuklia na missile za masafa marefu, lakini marekani hawawezi kumruhusu maana wanahofia kuwa anaweza kuamua kulipiza kisasi! Wala hawezi kutengeneza kwa siri maana kila sehemu kuna wananeshi wa marekani wakiwaangalia!
Hakuna urafiki wa kweli hapo!
 
Ni kweli kwamba japan iliishaendelea muda mrefu sana,kiasi cha kuwa na makoloni kabisa mfano china.ila hiyo kauli ya kusema kawa mdebwedo sikubaliani nayo.

Hawa jamaa baada ya lile tukio ni kama walielewa madhara ya vita rasmi na kuamua kudeal na mishe zingine za maana,hulka hii ameambukiza lililokuwa koloni lake china.

Hata hivyo sijaona hasara yoyote mpaka sasa kwa mkataba ule.kim ni kichaa wa kupuuzwa tu.
Kweli mkuu wajapani wana uwezo mkubwa wa kufikili haya maamuzi waliona Mbali.
 
Back
Top Bottom