Japan ilifanya kosa kubwa sana kumwachia USA awe mlinzi wake mkuu baada ya kuisha kwa WWII

Unajua Japan wamesave pesa kiasi gani kwa kulindwa 'bure' na USA?? Unadhani Japan ingekuwa hapo ilipo leo kiuchumi kama wangekuwa na 'mzigo' wa jukumu la kuwekeza kwenye ulinzi kama nchi zingine?
Hakuna cha bure mkuu ananunua mitambo ghali yoka USA kujilinda! US amlinde bure kwa kitu gani wakat japan ana uchumi mzuri
 
Ila Italy wamejipoteza kizembe sana. Wana uwezo wa kurudi kwenye game na nafasi yao lakini hawana mpango wowote ulr
Sun Tzu mmoja ya watu hodari kwenye mbinu za vita aliwahi sema
"When you are strong, pretend to be weak so as to tempt the enemy. When you are weak, pretend to be strong so as to deter him. Use speed and secrecy to make out that you concentrate at one place, then attack at another. If weaker than the enemy, avoid him, harass him, and draw him into terrain that is unfavorable for him; if equal to him, wait patiently until he commits an error. Confuse him and keep him ignorant of your designs by offering bait, mounting feints or spreading disinformation as appropriate. Finally, when you have the enemy where you want him (just when he feels secure) fall on him like a thunderbolt."
Italy yupo vizuri hajaamua kujishughulisha na masuala ya vita, lakini hadharauliki bado!. Na anajua madhara ya vita ndio unaona kama wakimbizi wanaokimbilia kwake anawarudisha sababu hakuhusika kuanzisha vurugu makwao!.
 
Baada ya kumalizika kwa WWII na Japan kushindwa vita baada ya kuangushwa kwa mabomu ya Atomic kule Hiroshima na Nagasaki Japan aliamua kusurender na kuachana kabisa na vita ili ajenge uchumi wake ambao uliporomoka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupigana vita kwa muda mrefu na mataifa mabalimbali makubwa na vita nyingi iliibuka mahindi hadi kuwa tishio la dunia
4d91474937fe7a623087a38fcebff80c.jpg

79ccae5632ae0a17da269cc9b5f71e2a.jpg


Historia inaeleza kuwa Japan ilikuwa ni tishio kubwa enzi hizo, Historia inaeleza kuwa Japan ilikuwa imeshapiga hatua kubwa sana kijeshi kipindi hicho huku ikijitengenezea zana zake yenyewe bila kutegemea taifa lolote lile

Pia historia inaeleza kuwa Japan ndio taifa pekee ambalo ilikaribia kuingia ndni ya ardhi ya marekani kijeshi baada ya lile shambulio kali la pearl habour attack ambalo lilipoteza uhai zaidi ya raia 2000 wa marekani katika lile shambulio la ndege za japan kwa mda mfupi tu
8689fb1b76d3f3d8df0f0b7288f1851e.jpg

cc1d122a16918bef2f2b4cfe37b68a80.jpg

Baada ya japan kufikia hatua kubwa za kutaka kuiangamiza marekani kivita ilibidi Raisi wa marekani kipindi hicho asaini kwa dharura kuangushwa kwa mabomu ya nuclear japan ili kumshinikiza Japan kuachana na ile vita maana Japan alishakuwa sugu kivita yaani alikuwa hapigiki kirahisi kivita

Historia inaeleza kuwa baada ya kuangushwa kwa yale mabobu kule hiroshima na Nagasaki Japan iliamua Kuachana na vita na kuamuru wanajeshi wake wote warudishwe nyumbani na katika mkataba wa kusurender japan aliamuriwa kuwa apunguze jeshi lake ili kumzuia kuja kuanzisha vita vingine na alimuriwa amuache Mmarekani ndio awe mlinzi wake mkuu kijeshi miaka yote
a779cabb136fbbcff6078e3b66c4db29.jpg


Baada ya Japan kukubali hiyo janja ya Mmarekani hivi leo mwaka 2017 Japan huko alipo najua sasa anajuta kwa nini alikubali kufanya upuuzi kama ule wa kumruhusu mmarekani ndio awe mshirika wake mkuu katika maswala ya ulinzi kwani kilichotokea ni kuwa Marekani badala ya kumfanya japan awe imara kijeshi mwishowe japan sasa imekuwa legevu na kila mitambo ya ulinzi na mbinu imekuwa ikimtegemea Mmarekani

Japan ilikuwa sio taifa la kuja kutishiwa na watoto wa juzi hawa akina kim jon un kama ingejiwekea misingi yake yenyewe ya kiteknolojia ya kujilinda kijeshi bila kutegemea msaada wa Mmarekani. Japan ilitakiwa iwe tishio na hakuna wa kumsogelea pale sio Mchina,mkorea wala Mmarekani.

Leo hii imefikia hatua mkorea makombora yake yote anayatestia japan kwasababu ashajua udhaifu wa japan ulivyo. Sasa ivi mjapan amekuwa akimtajirisha mmarekani kwa kununua mitambo mikubwa ya ghatama ya kujilinda na makombora kutoka korea na cha kusikitisha hiyo mitambo bado imeshindwa kutungua makombora yanayotoka korea

Japan sasa anatishiwa nyau na kim ?

Kweli mmarekani sio mtu kabisa
laiti kama mjapani na mjerumani wangebaki na nguvu zao,huenda mpaka sasa tungekuwa tunahesabu vita kuu ya 10 ya dunia,,german alishazingira russia,na ulaya yote isipokuwa uingereza sababu ni kisiwa,,sema russia msimu wa baridi kali uliingia ghafla,magari,wanajeshi vyote viliganda kama vilivyo,ndo russia akapata mpenyo,,japani alipiga pearly habour na darwin australia kwa kishindo sana...
 
Unajua Japan wamesave pesa kiasi gani kwa kulindwa 'bure' na USA?? Unadhani Japan ingekuwa hapo ilipo leo kiuchumi kama wangekuwa na 'mzigo' wa jukumu la kuwekeza kwenye ulinzi kama nchi zingine?
duniani hakuna kitu cha bure,kumbuka hilo siku zote...
 
Hata baada ya mika mingi kupita na kujionea maendeleo ya hali ya juu sana ya kijamii, kiteknolojia, kimiundo mbinu, kiutamaduni, kiustaarabu na kiuchumi bado Mnatamani Japan wangechagua kuwa kama North Korea dhidi ya vile walivyo sasa?
north korea mtoto sana kwa japan,hizo nchi za korea,china,burma,vietnam,sehemu ya russia nk,zilikuwa ni makoloni ya japan,russia iliwahi shindwa vita na japan..
 
laiti kama mjapani na mjerumani wangebaki na nguvu zao,huenda mpaka sasa tungekuwa tunahesabu vita kuu ya 10 ya dunia,,german alishazingira russia,na ulaya yote isipokuwa uingereza sababu ni kisiwa,,sema russia msimu wa baridi kali uliingia ghafla,magari,wanajeshi vyote viliganda kama vilivyo,ndo russia akapata mpenyo,,japani alipiga pearly habour na darwin australia kwa kishindo sana...
ujeruman na japan walikuwa wazuri sana kwenye mbinu tata za kivita hasa yamamoto na mbinu yake ya kamikaze
 
Back
Top Bottom