January, Wakala Wa Dowans (mafisadi), Punguza Kasi !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January, Wakala Wa Dowans (mafisadi), Punguza Kasi !!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Mar 2, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Chanzo Mwanahalisi

  Nyerere, katika moja ya hotuba zake alisema, ikulu ni mahali patakatifu. Alitumia neno ‘takatifu’ si kwa bahati mbaya. Kamusi inazungumzia neno hilo kama kitu kisichokuwa na dhambi, kilichotakasika.Kwa maono ya Nyerere ni kwamba, mtu yeyote ambaye ana mawazo ya kwenda ikulu lazima wakati wote ajue mahali hapo ni pasafi, kwa maana ya matendo yake na mwenendo mzima wake ni lazima wakati wote uwe juu ya tuhuma.Kukaa kwake ikulu kamwe kusihusishwe na dhambi yoyote, iwe ya kutenda mwenyewe kama vile ufisadi, au hata ya kusaidia kundi fulani katika jamii kutenda ufisadi au uchafu wowote.

  Katika kutekeleza majukumu yake, Rais hakika hawezi kufanya kila kitu peke yake, atakuwa na wasaidizi. Hawa ni watendaji na washauri wa Rais; ndio wanaotekeleza kwa vitendo halisi yale yote anayoamua.Haipendezi wala haivumiliki mtumishi wa umma ambaye anakaa ikulu, kwa maana ya kumsaidia Rais katika majukumu yake atajwe kwenye kashfa yoyote chafu; kwa maana ya mahusiano au uchafu wa ukwapuaji wa mali ya umma kwa njia za hila yeye binafsi au kusaidia kundi fulani la watu.Kwa maneno mengine, wale wote wanaoteuliwa na Rais kumsaidia kazi ikulu, lazima waishi kama watakatifu ili matendo yao yasije kuchafua mahali patakatifu—Ikulu.


  Kwa msingi huo huo, wale wote waliofanya kazi ikulu watokapo, ni vema wakaonekana wakiendelea na utakatifu huo, ili umma usije kudhania kwamba wakiwa ikulu walijifunza utukutu au ubazazi.Haya yote ninayazungumza baada ya kumtazama kijana mwanasiasa January Makamba, mbunge wa Bumbuli na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. January akiwa amekaa ikulu chini ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete tangu 2006 hadi 2010, ni matarajio ya wengi ikulu ilimlea na kumkuza kisiasa na kukomaa kwa uadilifu, ili kokote atakakokuwa ang’ae na kubeba ile taswira ya utakatifu. Kwamba January ameibuka kwa kasi katika anga za siasa nchini, si jambo la kustaajabisha, lakini pia kusema kwamba kupaa na kung’aa huko kumechangiwa sana na kukaa ikulu si kitu cha kubeza au kubishiwa na yeyote anayejua kupambanua mambo kwa mapana yake.
  Kwa haiba, January anaonekana kama kijana mwerevu, mcheshi na anayethubutu. Alijitahidi kujinadi kwa njia mbalimbali kujipenyeza kwenye jimbo la Bumbuli lililokuwa limekaliwa na William Shellukindo tangu mwaka 1995.


  Alifanikiwa kupitia njia halali za kura kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). January hakupata mpinzani kutoka vyama vya upinzani, kwa hiyo jasho lake lilitoka kwenye kura za maoni tu. Nyota ya January iling’aa zaidi mapema mwezi huu alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati nyeti ya Bunge ya Nishati na Madini. Kwa Kiswahili wanasema utuki yaani mambo yanayotokea kwa kufanana, nafasi ambayo pia alikuwa amekalia Shellukindo. Kabla hata ya kuukwaa uenyekiti wa Nishati na Madini, alikwisha kumwandikia barua Waziri wa Nishati na Madini akilalamikia mgawo wa umeme, lakini pia alitaka ‘siasa ziwekwe kando’ katika kushughulikia suala hilo .


  Barua hiyo, kwa njia ya ‘ki-spin doctor’ ilipenyezwa kwenye vyombo vya habari ilhali ilikuwa waraka kwa waziri kama ushauri juu ya umeme. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba January hakutaka kuchukua njia ya dhahiri ya kutaka kuiwajibisha serikali kama vile kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu suala la umeme, ila alitaka njia za majadiliano ya ndani kwa ndani. Lakini cha ajabu barua yake iliibukia kwenye magazeti! Muda si muda, January alivunja ukimya juu ya mitambo ya Dowans; alisema wazi kwamba alikuwa anaishauri serikali kuwashwa kwa mitambo hiyo, huku akijikinga kwenye jukwaa la ‘kuacha siasa katika masuala ya kiutendaji’. Hoja hii, duru zinasema, ilipowasilishwa kwenye kamati yake, ilikumbana na kizingiti kikali. Mmoja wa wabunge walimtaka atangaze maslahi yake kwa jinsi alivyokuwa analisukuma suala la Dowans kwa hisia na nguvu kubwa.


  Hakuna Mtanzania anayefuatilia masuala ya nchi yake asiyejua Dowans. Dowans ni mrithi wa mkataba wa Richmond ambao uliangusha baraza la mawaziri mwaka 2008. January alikuwa ikulu wakati kadhia hii ikitokea na kwa hakika alijua vilivyo hali hii ilivyomwathiri Rais wake. Lakini pia January shaka anajua vilivyo kuwa Dowans ina kesi na TANESCO juu ya kulipwa fidia ya Sh. 94 bilioni, ambazo kila Mtanzania ameipinga; taifa limeingia taharuki kubwa juu ya fidia hii iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Ushuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC). Umma una hasira na jazba papo! January anafahamu haya yote. Kubwa zaidi, January anajua kuwa kuna mapingamizi yamewasilishwa Mahakama Kuu juu ya hukumu hiyo, na kwa ujumla wake kuna mambo mengi yenye wingu zito nyuma ya mkataba wa Dowans kwa sababu ‘uliporwa’ kwa Richmond katika mazingira ambayo TANESCO hadi leo wamepigwa butwaa.


  Kwa maana hiyo, ingawa Dowans walizalisha umeme wa megawati 100 bado haijawa halali kwa Dowans kudai kuwa ni kampuni safi kwa sababu njia waliyoingilia nchini imejaa mbigiri na michongoma michungu. Binafsi naamini kwamba January ambaye ni mwerevu na kijana jasiri anaielewa historia hii, lakini tatizo linaloibuka sasa ni pale anapojaribu kujitia eti anajenga zama mpya za siasa za Tanzania kwa kushindwa kujua kuwa historia ndiyo inayofinyanga kila kitu katika maisha ya binadamu. Histioria ya kukaa karibu na waridi ndiyo imemfinyanga January kuwa hapo alipo leo; hizi ni pamoja na nafasi ya Baba yake, Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM tangu mwaka 2007; pia kuwa msaidizi wa Rais Kikwete, masuala ya hotuba.


  Ni kwa maana hiyo tunamkumbusha January kwamba hawezi kukwepa historia ya Dowans kama ambavyo hawezi kukwepa historia yake mwenyewe.
  La mwisho ambalo ndilo linalobeba muktadha wa uchambuzi huu ni juu ya historia ya kufanya kazi ikulu na utakatifu; kwamba kazi anayoifanya sasa ni kama mtu aliyepewa kazi maalum ya kutumwa kusafisha Dowans. Kusaidia malipo yatoke; kuhalalisha biashara yake na TANESCO, ndiyo maana ya lugha ya ‘kuacha kuingiza siasa katika mambo ya utendaji’. Hii ni kauli ya kutaka kufunika kombe ili mwanaharamu Dowans apite. Ni nguvu za nani zinamsukuma kufanya haya yote kwa kisingizio cha ‘siasa mpya za kutokuingilia watendaji?’ Ushauri wa bure ni huu, January punguza kasi utashika kaa la moto mapema mno.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tuliashaonywa kuhusu huyu dogo, na nijuavyo mimi dogo thinks he is the smartest dude in TZ

  Wahenga walisema "mbio za sakafuni, huishia ukingoni" ---- it either he change now or wait to be changed by people's power
   
 3. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  January Makamba ni hatati kwa taifa la Tanzania. This guy is deadly than Rostam Aziz. He thinks he is the smartest dude in the world, wakati kuna vijana kibao ambao hawezi kuwafikia kifikra. Ni katoto kaliko bahatika kuzaliwa kwenye familia ya kifisadi, lakini yeye haoni hilo, kuropoka kama baba yake kaanza mapema, na mdogo wake Mwamvitta. JK alikataa kumpa uwaziri kwa sababu ya baba yake na maneno mengine machafu aliyapata kumhusu. Watanzania inabidi waanze mapema kumtizama kwa jicho makini
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ana bahati mbaya moja tu

  maisha yamebadilika, na watanzania wa leo si mabwege tena, give him five years utaniambia
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Typical Kubenea na sewer journalism...

  Badala ya kutupatia options on what this kamati or Tanesco should do yeye kaamua ku angukiakwenye Character assassination as if hilo ndilo la muhimu kwetu kwa sasa.


  Kama si kusei Kubenea anaishi kwenye generator na anapigwa na kiyoyozi

  Now naelewa kwa nini IDRISSA RASHID aliwaambia wakubwa zake kuwa hataki kuingiliwa na wanasiasa. We just love to play politics kwenye kila kitu kuanzia Gongo la mboto mpaka hili la umeme.


  In other news:  How the power crisis is `biting`​

  The current power crisis has occasioned a worrying slowdown in the government’s revenue collection, which a senior official says is lagging behind by eight per cent of targeted projections for the 2010/2011 financial year.

  Deputy Permanent Secretary for the Ministry of Finance and Economic Affairs, Dr Servacius Likwelile , says Sh3trillion had been anticipated from domestic by mid-year, but the target has been missed.


  Speaking on the sidelines of a stakeholders meeting on the power crisis in Dar es Salaam yesterday, the Deputy PS said the government was targeting to collect Sh 6 trillion in 2010/2011 to finance its budget amounting to Sh 11.6 trillion.


  He said if the current power crisis is not averted, the whole budget may be affected by 5 per cent, pointing out that shortage of power had enormously affected tax collection after some industries had either reduced or stopped production.  “The power crisis has raised the cost of production and increased the cost of living reflected in the increased inflation rate,” he said, cautioning that if the current crisis is not contained the inflation may rise further. Currently, the inflation stands at 6.8 per cent.
  The cry from the government comes amid another discouraging report from Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) that the deficit of power into the national grid has increased from 230 to 250 megawatts.


  Tanesco Executive Director William Mhando told The Guardian on Sunday that Independent Power Tanzania Limited (IPTL) is now generating between 10 and 50 megawatts only while its maximum capacity is 80 megawatts.

  Though Mhando did not openly state the reason behind IPTL’s minimum power generation, it was evident that lack of funds to purchase heavy funnel oil to run the generators is the major factor. “IPTL is generating power below its capacity due to insufficient supply of oil but when it is supplied with sufficient fuel it can generate power to its capacity which is 80 megawatts,” Mhando said.
  The Chairman of Energy and Minerals Parliamentary Committee January Makamba whose committee members also attended the meeting at the Karimjee Hall called on the public to put ahead national interests when speaking about the power crisis, including offering possible solutions to the problem.

  Makamba said the nation was currently at a crossroads considering the truth that resolving the ongoing power crisis was difficult due to political and legal contradictions, adding that whatever decision is reached should be made carefully. Giving an example on how legal matters and politics were contracting in trying to resolve power crisis, Makamba gave an example of the ongoing debate on Dowans turbines whereby some people wanted the turbines nationalized while others wanted the government and Tanesco to accept Dowans offer. But, according to Makamba, any decision reached should not harm or cost the public in future.


  Until now Dowans has offered to drop the debt amounting to Sh 94 billion it owes Tanesco that emanated from the verdict reached by the ICC on condition that the power utility pays for the power it purchased from Dowans, costing Sh 24 billion.


  Makamba also promised stakeholders that his committee is expected to hold discussions with Tanesco and the Ministry of Energy and Minerals officials on Tuesday to reach a final decision on the subject. But, Minister for Energy and Mineral William Ngeleja told the press on Friday that the Tanesco board would also meet to discuss Dowans offer.

  Speaking on the sidelines of the meeting, Ubungo MP John Mnyika told this newspaper that Dowans generator should be nationalized for the interest of the nation but that process should be done with extra care.

  On Thursday Dowans came out in public to express its intention to forgive some of the compensation awarded to it by the ICC. The offer was made public by Dowans’ Financial Manager and its Country Representative, Stanley Munai.
  Later Ngeleja confirmed that Tanesco had already been served with a letter from Dowans on the matter, clarifying that the Tanesco Board of Directors would meet to discuss and decide on the offer and have the public informed accordingly.

  However, it has been difficult to reach Tanesco board chairman, Peter Ngumbullu for clarification. Late last year, the International Chamber of Commerce (ICC) ordered Tanesco to pay Dowans 94bn/- in compensation for breach of power generation contract.


  Meanwhile, the Deputy Minister for Industries Trade and Marketing Lazaro Nyalandu is traveling to China to finalise negotiations with a prospective investor who has shown interest of investing in power energy generation through wind farm plants.


  Speaking before departure, he said once an agreement is sealed, power will be generated in three phases starting with 50megawatts, and rising to 100 and 300 megawatts.


  Nyalandu said that project would cost about Sh130 billions, and Tanzania will be in a position of selling power to the East Africa Community member states.  Home
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Whats your solution to current power crisis?

  TANESCO wafanye nini

  KAMATI ya January idemand nini

  Private sector ifanye nini?
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  TRA predicts Sh840 billion loss in six months​
  Saturday, 26 February 2011 22:32


  By Bernard Lugongo, Citizen Reporter
  Dar as Salaam. The country is destined to lose about Sh840 billion from revenue collections in the second half of the current financial year, should the power crisis persist, a senior official of the Tanzania Revenue Authority (TRA), has warned.


  TRA Director of Research and Policy, Mr Tonedeus Muganyizi told members of the Parliamentary Committee for Energy and Minerals in Dar es Salaam yesterday that the anticipated deficit is about 30 per cent of the collection target for the second half of the year.


  TRA had originally planned to collect Sh5.6 trillion in domestic revenues during the financial year ending in June, meaning some Sh2.8 trillion was expected for each half of the period.


  However, Mr Muganyizi said that although the authority had raised 92 per cent of the revenue target in the first half of the year, it was now worried to fall short by 30 per cent due to the power shortage.


  The Authority fears that only Sh1.96 trillion is likely to be collected over the next few months, since businesses and other productive sectors of the economy have been forced to scale down or close their operations. The Confederation of Tanzania Industries (CTI) has confirmed that 50 factories had since closed shop in the wake of power outages.


  The meeting was chaired by Bumbuli MP, Mr January Makamba, and was attended by other interested parties to chart a way out of the power crisis, as the state power utility, Tanesco, grapples to satisfy growing demand for electricity.


  He cautioned that time was running out for a solution, adding: "there is no time for talks, let's take swift action to save our economy."

  The Permanent Secretary for Finance and Economic Affairs, Dr Servacius Likwelile also said the country's Gross Domestic Product (GDP) will drop by five per cent due to the same problem.

  He was worried that the government may not meet all its budgetary obligations, and the anticipated loss in domestic revenues would force it to rely more on donor support.

  "Let's change the way we make decisions and be serious and focused for the sake of the country's economy," the PS said.
  Mr Maliki Kasambala, the Managing director of Tanzania Investment Consultancy Agency blamed the government for bureaucracy and failure to effectively promote the private sector's participation in power generation.

  "Let's stop politicking and use available opportunities like Dowans to generate the much needed electricity," he said.

  Other speakers at the meeting also suggested that the government should look for quick solutions; including switching on the Dowans plant and supplying enough fuel to run the IPTL generators at full capacity of 100MW.

  Mr Makamba assured them that his committee would submit their concerns to the government and push for their implementation.


  TRA predicts Sh840 billion loss in six months
   
Loading...