PreGE2025 January Makamba: Miaka Minne ya Rais Samia imeleta Umoja na Maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,028
Reaction score
6,875
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa na maana kubwa katika ustawi wa maisha ya Watanzania, akisema nchi imekuwa na umoja, utulivu na mshikamano.

January, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Rais Samia amekuwa kiongozi sahihi kwa Watanzania kutokana na haiba, utulivu na mwenye dhamira ya dhati kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 20, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Bumbuli akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi wake.
 
Mimi binafsi nimesikia kwa masikio yangu sifa kama hizi akipewa Kikwete, Magufuli na sasa samia .
Kesho mwingine atasifiwa hivi kesho kutwa nayo itakuwa mwingine lakini maisha na hali ya taifa ipo palepale na heri hata jana kuliko leo.
 
Kuelekea uchaguzi mkuu mama ajiepushe na sifa za kupitiliza toka kwa matapeli wa kisiasa!
 
Mwimba kwaya mpya sauti ya tatu naona kaingia kwa makeke ingawa anaimba nyimbo ya kale tena iliyochosha kusikiliza
 
Hayo maendeleo huwa wanayaona viongozi wa CCM walioko madarakani tu wanapopanda majukwaani , ila sisi raia wa kawaida sio rahisi hata kuyahisi.
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa na maana kubwa katika ustawi wa maisha ya Watanzania, akisema nchi imekuwa na umoja, utulivu na mshikamano.

January, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Rais Samia amekuwa kiongozi sahihi kwa Watanzania kutokana na haiba, utulivu na mwenye dhamira ya dhati kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 20, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Bumbuli akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi wake.
Wezi wanafaidi sana awamu hii. Ila idadi kubwa ya watz namba wanaisoma maana huduma za kiijamii zimedumaa pesa zinaenda kwenye mifuko ya watu binafsi
 
Sometime unaweza kuhisi anamsifia kama anampenda kwa dhati kumbe anangata na kupuliza
 
Back
Top Bottom