January Makamba kusababisha mpasuko CCM

January Makamba kusababisha mpasuko CCM

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Ni kufuatia kauli yake ya rais kijana urais 2015
Source: gazeti Majira leo
=================================


KAULI iliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January Makamba, akidai Tanzania kwa sasa inahitaji Rais kijana, imeanza kuibua maswali kwa baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Shinyanga.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Bw. Charles Shigino, alisema kauli ya Bw. Makamba aliyoitoa akiwa nchini Uingereza inaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM kwa vile inaonesha ubaguzi wa wazi kwa baadhi ya wanachama wake. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana, Bw. Shigino alisema yeye binafsi anailaani kauli hiyo ambayo ameifananisha na siasa za ubaguzi ndani ya chama ili kulibagua kundi moja la wanachama.

Alisema CCM, imekuwa ikipinga suala la ubaguzi wa aina yoyote hivyo kauli ya Bw. Makamba kutaka Rais ajaye mwaka 2015 awe kijana inaweza kusababisha mpasuko kwani inapingana na Katiba ya CCM.

"Makamba anapaswa kuelewa kuwa, ujana si kigezo cha kuwa na sifa za kugombea nafasi ya urais, nafasi hii ni nyeti na mtu anayechaguliwa anapaswa kuwa na busara, uwezo wa kuongoza nchi bila kuyumba.

"Wapo wazee wenye sifa hizi kuliko vijana...kauli hii pia inapingana na Katiba ya chama chetu labda paitishwe Mkutano Mkuu tuweze kufanya mabadiliko ya Katiba vinginevyo hoja ya ndugu yetu haitakuwa na mashiko kama wazee watajitokeza kuwania urais," alisema.

Aliongeza kuwa; "Katiba ya CCM Ibara ya 14 vifungu vidogo vya (1) hadi (3), vinafafanua wazi juu ya haki za mwanachama ikiwemo ya kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi, hapa haijataja wenye haki hiyo ni vijana tu, inawezekana Makamba," alifafanua Shigino.

Alisema ni vizuri Bw. Makamba akajifunza kutoka kwa wazee waasisi wa taifa hili ambao waliwahi kuongoza nchi kwa ufanisi mkubwa badala ya kutoa kauli zinazoashiria mianya ya ubaguzi ndani ya CCM hivyo kuhatarisha mstakabali wa chama katika chaguzi zijazo.

"CCM ni chama kikongwe nchini, ndani yake kuna akina mama, wazee na vijana ambao wote wana haki sawa kwa mujibu wa katiba yetu, mimi sioni tatizo la mgombea urais kwa tiketi ya CCM atokane na vijana au wazee, wote ni sawa, mradi wawe na sifa, vigezo vinavyohitajika," alisema.

Shigino aliviomba vikao mbalimbali vya uteuzi ndani ya CCM, kuipuuza kauli ya Bw. Makamba na wajumbe wake wasiwe tayari kuongozwa na matakwa ya watu, bali wazingatie katiba na kanuni za chama katika uteuzi wao na muhimu kuangalia mtu gani mwenye uwezo wa kuivusha CCM 2015 bila kujali ni mzee au kijana.

CHanzo; Majira
 
Hii habari bila maelezo kama inaishia hapa nakushauri post facebook
 
Mpasuko CCM upo kitambo Makamba kaongezea tu. Na watapasuka sana tu.
 
Huyu jamaa wa Shy asituletee mambo ya kambi zake. Mbona juzi alikuwa akipiga debe kuwa mtu fulani ( ) anafaa kuwa rais kwani maoni yake ndiyo yanakubaliwa na katiba kuliko ya wengine?
 
CCM Kupasuka sio leo wala kesho! ccm ni chama kitakatifu na watu wake
 
Rais wa awamu ya tano wa tanzania hawezi toka kanda ya kaskazini kamwe! Ni zamu ya kanda nyingine!
 
Chadema ndiyo marufuku kutangaza kugombea wala kutoa mawazo tofauti na Mbowe na Slaa, utaishia kuitwa msaliti na kufukuzwa.

January Makamba, hawezi kuleta mpasuko wowote CCM anayeamini hivyo atakuwa na matatizo ya ufahamu.

Chadema jikitene kujenga chama chenu kinakufa, kuliko kuhangaika na CCM.
 
Chadema ndiyo marufuku kutangaza kugombea wala kutoa mawazo tofauti na Mbowe na Slaa, utaishia kuitwa msaliti na kufukuzwa.

January Makamba, hawezi kuleta mpasuko wowote CCM anayeamini hivyo atakuwa na matatizo ya ufahamu.

Chadema jikitene kujenga chama chenu kinakufa, kuliko kuhangaika na CCM.

Umemaliza kila kitu mkuu
 
Tunahitaji mabadiliko...si jambo la kushabikia lakini Makamba hafai, sababu ni nyingi.
 
Makamba anapima maji tu. Hana ubavu wa kuogelea mpaka mwisho. Ndio maana hutujasikia keelele nyingi. Asubiri 2025.
 
tamko la UVCCM Bagamoyo mbona halikukemewa au kwa vile mwana-mfalme alihusika? mliposema ni zamu ya Spika kuwa mwananmke, mbona hamkukemea? Double standard za nini? Pumbavu zenu CCM.....nawaacha wafu wawazike wafu wao
 
Mtu aliyefeli form six akaiba matokeo anaweza kuwa rais?

Kama Mbowe alizungusha yai form six na mwaka 2005 akagombea urais kwa tiketi ya chadema na leo hii ni mwenyekiti wa chama(akili ndogo kuongoza akili kubwa) unafkri kitakachomzuia january makamba ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom