MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
January Makamba, mtoto wa katibu mkuu CCM na msaidizi wa raisi uandishi wa hotuba, ametangazwa kuwa mshindi katika kura za maoni jimbo la bumbuli baada ya kuwashinda wagombea wenzie kwa zaidi ya asilimia 80 (80%).
Taarifa tulizozipata mpaka sasa baadhi ya wagombea wameyapinga matokeo hayo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za matumizi ya rushwa, mmoja wa wagombea alisema "ushindi wa January sio wa wana bumbuli, bali ni wa chama kwani chama ndio kimeshinikiza ashinde, wana Bumbuli wanajua hawakufanya uamuzi huo bali ni mizengwe na rushwa na wizi wa kura ndio uliomuweka mshindi, ilibidi waufanye ushindi wake mkubwa ili ionekane hakuwa na upinzani jimboni, lakini nikwamba hali yake jimboni ilikuwa sio nzuri"...
Baadhi ya wananchi pia wamesema wanashangazwa na ushindi huo kwani hivyo sivyo walivyotegemea, mwanachama mmoja kutoka kata ya mgwashi alisema " tunashangazwa na matokeo haya na wengi wetu imefika hali wamelia, hapa watu walimfurahia sana Kaniki kwa sera na hata alipohutubia hapa kwenye mkutano wengi waliguswa na umakini wa kuzielezea kero zetu na jinsi atakavyosaidiana na watu kuzitatua, January hakuwa na sera zaidi ya kusema amezunguka na raisi, ameenda nchi nyingi anajuana na matajiri, yule sisi hatufai hata adabu hana maana wapambe wake ndio waliokuwa wanamzomea mzee shelukindo"
Wagombea walioshiriki katika kinyanganyiro hicho ni pamoja na Mzee Wiliam Shelukindo, Abubakari mshihiri, leonard kaoneka, joseph kijangwa,lea shemndolwa, Raphael Shemtambo na Abdulkadir Kaniki.
Wengi wanasema jimbo hili wananchi walikuwa wamepanga liende kwa kijana Kaniki lakini nguvu ya pesa na utawala imeamua tofauti, inasemekana usiku wa kuamkia kupiga kura watu wengi sana walivamia jimbo hilo, kulikuwa na zaidi ya pikipiki 100 zikizunguka jimboni na magari yenye vipaza sauti yakimnadi January wakati muda wa kampeni ulikwisha, waliingia nyumba kwa nyumba na kuwagawia pesa wapiga kura ili wamchague January, siku ya kupiga kura ndio iliuwa shida, maana uongozi wote wa wilaya na jimbo uliingia jimboni kufanya kazi moja tu ya kuhakikisha matokeo yanaenda kama ilivyopangwa, kwenye vituo vya kupigia kura mambo yaliyokuwa yakifanyika ni aibu.
baadhi ya wazee walimpongeza kijana kaniki kwa ujasiri alioonyesha na kusema kwamba kwa mambo yalivyokuwa yamepangwa huyu kijana hata kama angeshinda ingekuwa ni tatizo kwake, hawa watu amewatia hasara sana kwani walikuja wakijua wakumuondoa ni mzee shelukindo lakini wakakutana na kisiki cha kijana huyu, kaniki ni kijana safi, anayejiamini, akiongea wote munatamani asimalize, ni hadhina kwa chama.
baadhi pia ya wapambe wa January tulioongea nao wengi wamemsifu ndugu kaniki na kukubali ndiye aliyetishia hali yao, "huyu kijana bwana anakubalika sana hata January amekubali,lakini kazi yetu ni kumdhibiti", baadhi ya wananchi wa kata ya Bumbuli walisema pia kaniki ndio chaguo lao.
Tulipowasiliana na ndugu kaniki kwa simu na kumuuliza ameyachukuliaje matokkeo, alisema "inasikitisha lakini ndio wana bumbuli walivyoamua,tulikuwa wagombea tisa lakini wamemchagua waliyemuamini zaidi,lazima tuheshimu maamuzi ya wengi", alisema pia atakuwa tayari kushirikiana na mshindi yeyote atayetangazwa na chama ili kukipa chama ushindi wa kishindo mwezi octoba.
Ndugu January naye alisema amepokea matokea hayo kwa furaha na amesema alitarajia ushindi huo kwa imani aliyokuwa nayo kwa wananchi kwani imani huzaa imani, tulipomuuliza kuhusu malalamiko juu ya ushindi wake, alisema hao wanaosema hivyo ni wapinzani walioshindwa, lakini pia nayeye aliwashukuru wagombea wenzie na kuahidi atawatumia katika kuwatumikia wana Bumbuli,"ninahitaji ushauri wa mzee shelukindo lakini pia mdogo wangu kaniki ameonyesha uwezo mkubwa na busara ya hali ya juu,nitafurahi kifanya naye kazi kwani nia anayo ya kuwatmikia wannachi"
wapo wananchi wanaohisi ushindi wa January unaweza kukiletea chama cha mapinduzi matatizo kwenye uchaguzi mkuu endapo kitatokea chama cha upinzani chenye mgombea anayekubalika, kwani january si chaguo la wananchi, inasemekana ushindi wa january ulikuwa ni lazima kwani angeshindwa ingekuwa ni fedheha kubwa kwa Mzee Makamba na chama.
source: Tanzania Daima