Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,681
- 46,362
Wakati Makamba akiwa waziri wa mazingira katika serikali ya awamu ya tano aliifanya wizara hiyo ambayo huwa sio maarufu sana kuweza kunga'ara na kusikika sana. Aliweza kuisimamia kwa ubunifu mkubwa na kuipa umaarufu sana.
Mojawapo ya jambo kubwa alilosimamia kwa umahiri na weledi mkubwa ni kuondolewa kabisa kwa vifungashio vya mifuko ya plasitiki bila purukushani. Alikuja na mawazo bunifu ya jinsi ya kupunguza matumizi ya mkaa, alikuwa akihusika sana kusimamia upandaji miti, viwanda vilivyokuwa vikifanya uchafuzi wa mazingira viliadhibiwa vikali, alihamasisha teknolojia katika sekta ya mazingira.
Huenda Makamba angefaa zaidi katika mazingira kuliko alipo sasa ambapo anatupiwa lawama kibao kwa jinsi hali ya huduma ya umeme kutoka shirika la TANESCO ilivyo ya kusuasua. Pamoja na utetezi wake mwingi raia wengi bado wanamuona hatoshi, huenda nyota yake iko katika mazingira.