January Makamba aliweza sana Wizara ya Mazingira, kwa sasa amepwaya

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
36,622
44,274
Wakati Makamba akiwa waziri wa mazingira katika serikali ya awamu ya tano aliifanya wizara hiyo ambayo huwa sio maarufu sana kuweza kunga'ara na kusikika sana. Aliweza kuisimamia kwa ubunifu mkubwa na kuipa umaarufu sana.

Mojawapo ya jambo kubwa alilosimamia kwa umahiri na weledi mkubwa ni kuondolewa kabisa kwa vifungashio vya mifuko ya plasitiki bila purukushani. Alikuja na mawazo bunifu ya jinsi ya kupunguza matumizi ya mkaa, alikuwa akihusika sana kusimamia upandaji miti, viwanda vilivyokuwa vikifanya uchafuzi wa mazingira viliadhibiwa vikali, alihamasisha teknolojia katika sekta ya mazingira.

Huenda Makamba angefaa zaidi katika mazingira kuliko alipo sasa ambapo anatupiwa lawama kibao kwa jinsi hali ya huduma ya umeme kutoka shirika la TANESCO ilivyo ya kusuasua. Pamoja na utetezi wake mwingi raia wengi bado wanamuona hatoshi, huenda nyota yake iko katika mazingira.
 
Binafsi naona Tanesco wamejitahidi kufanya maintenance kipindi chake
 
Kwani bado yupo?.

Au ndiyo ameamua kuakaa kimya huku akijiandaa kuokoka kuwa mlutheli kwa kigezo kumfuata mamake although lengo likiwa (ahahahahaaaa) eti di next presidenti..!
 
Next president wa wapi nani atampa hizo Kura?
 
Wakati Makamba akiwa waziri wa mazingira katika serikali ya awamu ya tano aliifanya wizara hiyo ambayo huwa sio maarufu sana kuweza kunga'ara na kusikika sana. Aliweza kuisimamia kwa ubunifu mkubwa na kuipa umaarufu sana.

Mojawapo ya jambo kubwa alilosimamia kwa umahiri na weledi mkubwa ni kuondolewa kabisa kwa vifungashio vya mifuko ya plasitiki bila purukushani. Alikuja na mawazo bunifu ya jinsi ya kupunguza matumizi ya mkaa, alikuwa akihusika sana kusimamia upandaji miti, viwanda vilivyokuwa vikifanya uchafuzi wa mazingira viliadhibiwa vikali, alihamasisha teknolojia katika sekta ya mazingira.

Huenda Makamba angefaa zaidi katika mazingira kuliko alipo sasa ambapo anatupiwa lawama kibao kwa jinsi hali ya huduma ya umeme kutoka shirika la TANESCO ilivyo ya kusuasua. Pamoja na utetezi wake mwingi raia wengi bado wanamuona hatoshi, huenda nyota yake iko katika mazingira.
Kipimo chako Cha kupwaya ni kipi utusaidie?
 
makamba ni overrated.
 
January yuko vizuri sana kimenejimenti. Ila Wizara aliyopewa Jamaa kashiba hela nyingi sana za Waarabu na Wachina. January Kwa sasa akaunti yake inasoma zaidi ya 2.8 Trilioni Kwa muda tu aliokaa Wizara hiyo. Bado ana mradi wa kufumua mfumo wote wa umeme nchi nzima kwa 7trilioni na Kuna 17% ya kwake kutoka kwa Waarabu.
 
Wakati Makamba akiwa waziri wa mazingira katika serikali ya awamu ya tano aliifanya wizara hiyo ambayo huwa sio maarufu sana kuweza kunga'ara na kusikika sana. Aliweza kuisimamia kwa ubunifu mkubwa na kuipa umaarufu sana.

Mojawapo ya jambo kubwa alilosimamia kwa umahiri na weledi mkubwa ni kuondolewa kabisa kwa vifungashio vya mifuko ya plasitiki bila purukushani. Alikuja na mawazo bunifu ya jinsi ya kupunguza matumizi ya mkaa, alikuwa akihusika sana kusimamia upandaji miti, viwanda vilivyokuwa vikifanya uchafuzi wa mazingira viliadhibiwa vikali, alihamasisha teknolojia katika sekta ya mazingira.

Huenda Makamba angefaa zaidi katika mazingira kuliko alipo sasa ambapo anatupiwa lawama kibao kwa jinsi hali ya huduma ya umeme kutoka shirika la TANESCO ilivyo ya kusuasua. Pamoja na utetezi wake mwingi raia wengi bado wanamuona hatoshi, huenda nyota yake iko katika mazingira.
Pumbavu wewe. Unamwambia nani?
 
Suala la vifungashio si yeye ila naweza sema ni kwa sababu ya uongozi imara WA JPM ulikuwepo kwa wakati huo na wananchi walilielewa na kuyajua vyema madhara ya mifuko ya plastiki na ndio ilipelekea zoezi kufanikiwa kwa ukubwa
 
Mbona hamumsifii JK kwa kujenga mtandao mkubwa zaidi wa barabara wakati JPM akiwa waziri wake wa ujenzi?
Na alipokuwa Rais sasa ndio akaifanya maajabu ya flyover,SGR,barabara za lami mitaani lakini mbona Kwa wengine hatuoni any initiative
 
Suala la ujenzi mtandao mrefu wa barabara kuunganisha wilaya za nchi hii ilikuwa ni yeye au JK?
Suala la vifungashio si yeye ila naweza sema ni kwa sababu ya uongozi imara WA JPM ulikuwepo kwa wakati huo na wananchi walilielewa na kuyajua vyema madhara ya mifuko ya plastiki na ndio ilipelekea zoezi kufanikiwa kwa ukubwa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom