Uchaguzi 2020 January Makamba akana kuporwa fomu kwa mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli kupitia CHADEMA

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
9,006
25,466
Mhe. January Makamba amenukuliwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akikanusha kuporwa fomu za kuteuliwa kugombe ubunge kwa muomba ridhaa ya kugombea Ubunge jimbo la Bumbuli kupitia CHADEMA. Habari zilianza kuenea mitandaoni mapema asubhuhi kuwa Mgombea wa CHADEMA jimboni Bumbuli ameporwa fomu za kuomba uteuzi wa kugombea Ubunge katika Jimbo la Bumbuli.

Bumbuli.jpg

Wagombea Ubunge katika Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba (CCM) na Abubakar Mashambo (CHADEMA) katika picha ya pamoja kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Bumbuli, wakati wa kurejesha fomu za uteuzi. 
Tapeli mwizi wa kula 2015 sisi tutamuamini vip?

Lengo la CCM Ni Majaliwa, Npe na January wapite bila kupigwa ili wazunguke na Jiwe kwenye kampeni kumsaidia.

Kitu ambacho hawaelewi Ni kwamba mahitaji ya wakati watu hawaitaki CCM.
Kapime macho, inamaana Mshambo we humuoni hapo akisubiri kukabidhi form? Chadema shida sana, no wonder nchi hamuwezi pewa kwa akili dizain hii
 
Yeye anawezaje kukana kwani yeye ndiye aliyeporwa mbona ccm ni wajinga kiasi hiki hebu nitoe mfano MTU akisema amepigwa na mtu fulani anawezaje kujitokeza mtu ambaye hakuwepo na kusema hajapigwa kwanza CCM ni watuhumiwa kwenye hilo so hawana moral authority ya kusema chadema hawajaporwa otherwise Niyeye 2020
 
Chadema wamekuwa na hofu sana, hawana imani na yeyote na kwa hili siwalaumu, mambo waliyofanyiwa na awamu hii yanawafanya wakose imani nao kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Chadema wamekuwa na hofu sana, hawana imani na yeyote na kwa hili siwalaumu, mambo waliyofanyiwa na awamu hii yanawafanya wakose imani nao kabisa.
Hapana mkuu mbona CHADEMA walikuwa wawazi mwanzo walitoa taarifa za kuporwa fomunmgombea wao na baada ya hapo wakatoa tena taarifa kuwa fomu karejeshewa sasa sijaona tatzo la CHADEMA kwani hata huyo January alianza kusema kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya CHADEMA kuweka taarifa kuwa mgombea wao karejeshewa fomu
 
Yeye anawezaje kukana kwani yeye ndiye aliyeporwa mbona ccm ni wajinga kiasi hiki hebu nitoe mfano MTU akisema amepigwa na mtu fulani anawezaje kujitokeza mtu ambaye hakuwepo na kusema hajapigwa kwanza ccm ni watuhumiwa kwenye hilo so hawana moral authority ya kusema chadema hawajaporwa otherwise Niyeye 2020
Duh... Umeandika kijinga mno
 
Kwanini CHADEMA wanaleta tahaluki namna hii au lengo ni kutafuta attention na kunogesha uchaguzi au kutafuta huruma?
 
Hapana mkuu mbona CHADEMA walikuwa wawazi mwanzo walitoa taarifa za kuporwa fomunmgombea wao na baada ya hapo wakatoa tena taarifa kuwa fomu karejeshewa sasa sijaona tatzo la CHADEMA kwani hata huyo January alianza kusema kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya CHADEMA kuweka taarifa kuwa mgombea wao karejeshewa fomu
Sasa hao chadema wanashindwa kuuliza aliporwa na nani na ni nani aliyemrudishia ili awe mfano kwa wengine?
Kwa hiyo taarifa ndio imeishia hapo?

Hawajui usumbufu waliosababisha kwa ndugu/jamaa wa mgombea, wanachama wa chadema , wananchi na serikali kwa ujumla?
Hiki chama kimekua cha kipuuzi sana
 
Huyo makamba ndiye mmiliki wa hilo genge la upororaji..

Yaani kila mwana ccm ni jangili miaka hii.. poa tuu ukiona hivyo ujue ukombozi upo karibu.

Ukipewa heshima heshimu wanao kupa heshima.

Ipo siku kuna watu wazima watakimbia wakiwa na boksa tu.
 
Katika chama ambacho hakieleweki Nadhani Chadema inaweza kuongoza africa kama si Dunia.

Chadema inakuwa kama ukoo wa makambale kila mtu anandevu leo habari za chama kila mwanachama au mpenzi wa Chadema akiwa na smartphone au PC bhasi amekuwa msemaji wa chama.

Haiwezekani chama makini hakina kitengo cha habari leo mtu yeyote anaweza toa taarifa ya chama ,taarifa wa wagombea wanazidiwa hata na Chauma hao wanaowaamini kwa taarifa zenu nadhani watakuwa wanaupungufu wa akili au fikra chama ambapo hata chizi akiamua kuandika Mbowe amevamiwa bhasi wanachama na wafwasi wake wanaanza kutomboka tu bila kujua hz taarifa ametoa nani na anamamlaka gani ya kutoa taarifa za chama.
 
January hawezi kufanya huo ujinga anajua siasa, nashangaa kwa nini NAPE kawa mpuuzi ghafla.
Issue hapa ni hawa waropokaji kuropoka na kuleta taharuki utadhani wagombea wao ni special na wanatisha kweli. Mbona vyama vingine hawatekwi. Hawa jamaa na masaburi yao wasengerema kweli kweli. Kipindi cha korona napo kila mara ilikuwa ni kuzua taharuki tu.
 
Back
Top Bottom