January amvaa Kingunge, asema anakivuruga chama (CCM)

January amvaa Kingunge, asema anakivuruga chama (CCM)

ccm wanataka kuueleza umma kwamba demokrasia ni kukubali kila kitu hata kama utaratibu haukufuatwa hakuna kuoji wala kuuliza. ccm ni janga

Mkuu huko kote ni kulewa madaraka,lkn hatuna muda mwingi zaidi watakuja kujuta.
 
Janaurı na Mwiguru walikuwa na sifa kuliko Edo.Edu anachangiwa fedha na majambazii ili aingie nyumba nyeupee??Mwinyewe mwz, anachangiwa na wezi alafu mnampigia chapuo??Lazima nyie mtakuwa wehu si bure.Nchi za watu Edo asıngefka hata kwenye mchujo.Hafaı,hafai na ningejitoa muhanga km angepitishwa.

Asante.Wahuni wanataka kutuwekea mgonjwa mwizi nyumba nyeupe na wanalazimisha iwe wanavyotaka.Kingunge ni muhuni mwenzao tu nae,anayeweza kumfikia aniulizie kwa Kingunge,kama angepitishwa Lowasa kwa mchakato huo huo uliotumika,ungekuwa wa halali?
 
Naomba nisahihishwe kama nimekosea; Kingunge hajapinga uteuzi wa Mh. Magufuli bali anahoji jinsi mchakato ulivyofanyika hadi kumpitisha yeye kama mgombea. Ni vizuri Mh. Makamba akaweka wazi kati ya wachukua fomu wote 38, yeye na wenziwe wanne alipata kura ngapi ngapi kwenye Kamati kuu zilizowezesha majina yao kupelekwa Halmashauri kuu ili kuchujwa na kubakiza majina matatu?
 
Wee mr mb8 ni papasi mdogo sana ndani ya chama so funga tuu bakuli lako.
 
Huyu chali anaongea sana, kwa vile system imemfavour ndio maana
Mchakato haukuwa wa haki wala haukuna wa kuficha hilo
 
Janaurı na Mwiguru walikuwa na sifa kuliko Edo.Edu anachangiwa fedha na majambazii ili aingie nyumba nyeupee??Mwinyewe mwz, anachangiwa na wezi alafu mnampigia chapuo??Lazima nyie mtakuwa wehu si bure.Nchi za watu Edo asıngefka hata kwenye mchujo.Hafaı,hafai na ningejitoa muhanga km angepitishwa.
Mkuu nikumbushe hivi hao unaowaita Majambazi ni wanachama wa chama gani vile?tena nasikia wengine ni wajumbe wa nec
 
View attachment 269016
Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amemtolea uvivu mshauri wa zamani wa Siasa wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kuupinga mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM na kusema anakivuruga chama.

Kingunge aliyejitoa kindakindaki kumpigania mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa jina la Lowassa.

Kamati ya Usalama na Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ndizo zilizokuwa na kazi ya kuchuja majina hadi kupatikana mgombea mmoja, Dk John Magufuli.

Akizungumza jana kwa simu kutoka Bumbuli Tanga, Makamba (pichani) alisema: Mzee Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika siasa, lakini anakivuruga chama.

Alisema binafsi hakubaliani na kauli za Kingunge kupinga uteuzi wa Dk Magufuli kwa sababu makada wote wa chama waliokuwapo Dodoma, waliamua kumpitisha kwa kuwa walimuona anafaa na anaweza kukijenga chama.

Ndani ya chama kuna wazee wenye busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua mgombea kwani unaweza kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi hivyo, unaweza vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye ushindi.

Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini siwezi kukubaliana naye anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa sahihi, kila mtu ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa, tuna imani naye na anaweza kuongoza tangu zamani, alisema Makamba.

Makamba alisema, ana imani kwamba atafanya vizuri hivyo ni bora apewe ushirikiano kama walivyopewa viongozi waliopita ili kukinusuru Chama cha Mapinduzi na watu waendelee kukiheshimu kama awali.

Katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema kwamba, watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli wana masilahi binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho.

Kauli ya Kingunge

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki, Katibu huyo wa zamani wa halmashauri kuu ya CCM alisema, Kamati ya Usalama na Maadili iliteka majukumu ya Kamati Kuu baada ya kuamua kuchuja majina ya makada waliojitokeza kuwania urais hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo zilifanywa kwa kuvunja kanuni na zililenga kumuengua Lowassa kuwania kuingia Ikulu.

Kingunge alisema kitendo cha kumuengua Lowassa kwa kuvunja kanuni kimeacha kasoro kubwa ndani ya chama hicho tawala kwa sababu taratibu zilikiukwa ili kupata viongozi.

Alisema kosa hilo siyo la Dk Magufuli aliyepitishwa kuwa mgombea urais wa CCM, na wala si la Lowassa, bali ni la waliopendekeza majina ya walioingia tano bora.

Jina la Lowassa, ambaye alijidhihirisha kukubalika ndani na nje ya CCM kutokana na harakati zake za kusaka wadhamini kujaa watu, halikupelekwa kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kingunge na hivyo kutojadiliwa na chombo hicho ambacho kilimpitisha Dk Magufuli, Dk Asha-Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali

Chanzo: Mwananchi, July 18, 2015

KINGUNGE YUPO SAHIHI SANA
TUTAFAKARI KWA KINA SHERIA IMEVUNJWA ZITAKAPO ENDELEA KIVUNJWA NINI HATTIMA YA CHAMA/ii
 
Ila watu wengi humu JF wana upeo mdogo wa kuelewa. Hivi CCM ingepmeitisha Lowassa au Membe angeshinda??????? Mbona kila mtu kimoyomoyo kabla ya uteuzi walikuwa wanaogopa kusema Magufuli akipita basi CCM imekomboka, eti sasa nyie wachache kwenye mtandao mnaona huruma. Mbona Lipumba na Mbowe hawataki kuachia uenyekiti na hamlalamiki? Je mkiwapa hao nchi wataiachia??? Au wataendesha siasa za kung'ang'ania madaraka? Watu tumieni akili, CCM sasa wapo kwenye mstari mnyoofu na hakuna anayepinga. Nyie subirini October 2015, ngoma ni Magufuli tu
 
Naomba nisahihishwe kama nimekosea; Kingunge hajapinga uteuzi wa Mh. Magufuli bali anahoji jinsi mchakato ulivyofanyika hadi kumpitisha yeye kama mgombea. Ni vizuri Mh. Makamba akaweka wazi kati ya wachukua fomu wote 38, yeye na wenziwe wanne alipata kura ngapi ngapi kwenye Kamati kuu zilizowezesha majina yao kupelekwa Halmashauri kuu ili kuchujwa na kubakiza majina matatu?

Uko vizuri mkuu
 
Mwanaume (Msomi) huwa hakubali kila kitu kirahisi rahisi.....hata kama una huba juu ya jambo lizungumzwalo.

Kwahiyo wewe kubisha hovyo hovyo ndio ujanja?umepotezwa sana
 
Kama alikuwa na sifa mbona sasa yupo kwao anaweweseka badala ya kuendelea kupeperusha bendera ya ccm?

Una mtazamo finyu sana....nimekuambia nipe Takwimu kama alikuwa hana sifa kuwazidi Lowasa, Wasira and mwandosya kama ulivyoainisha katika moja ya bandiko lako.......maana hata huyo Lowasa wako hapeperushi bendera ya Mafisadi CCM
 
Janaurı na Mwiguru walikuwa na sifa kuliko Edo.Edu anachangiwa fedha na majambazii ili aingie nyumba nyeupee??Mwinyewe mwz, anachangiwa na wezi alafu mnampigia chapuo??Lazima nyie mtakuwa wehu si bure.Nchi za watu Edo asıngefka hata kwenye mchujo.Hafaı,hafai na ningejitoa muhanga km angepitishwa.

Moja ya wanaomuunga EDO mkono ni chenge...yule alieshirikiana na Samuel sitta kutengeneza katiba pendekezwa ya ccm..na mlishangilia sana!
 
Ila watu wengi humu JF wana upeo mdogo wa kuelewa. Hivi CCM ingepmeitisha Lowassa au Membe angeshinda??????? Mbona kila mtu kimoyomoyo kabla ya uteuzi walikuwa wanaogopa kusema Magufuli akipita basi CCM imekomboka, eti sasa nyie wachache kwenye mtandao mnaona huruma. Mbona Lipumba na Mbowe hawataki kuachia uenyekiti na hamlalamiki? Je mkiwapa hao nchi wataiachia??? Au wataendesha siasa za kung'ang'ania madaraka? Watu tumieni akili, CCM sasa wapo kwenye mstari mnyoofu na hakuna anayepinga. Nyie subirini October 2015, ngoma ni Magufuli tu

Wewe muda wote upo kona bar,haya endelea kutoa huduma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom