January amvaa Kingunge, asema anakivuruga chama (CCM)

Kambigoha

Member
Joined
Jul 17, 2015
Posts
66
Reaction score
10
makamba.jpg
Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amemtolea uvivu mshauri wa zamani wa Siasa wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kuupinga mchakato wa uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM na kusema anakivuruga chama.

Kingunge aliyejitoa kindakindaki kumpigania mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa jina la Lowassa.

Kamati ya Usalama na Maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ndizo zilizokuwa na kazi ya kuchuja majina hadi kupatikana mgombea mmoja, Dk John Magufuli.

Akizungumza jana kwa simu kutoka Bumbuli Tanga, Makamba (pichani) alisema: “Mzee Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika siasa, lakini anakivuruga chama.”

Alisema binafsi hakubaliani na kauli za Kingunge kupinga uteuzi wa Dk Magufuli kwa sababu makada wote wa chama waliokuwapo Dodoma, waliamua kumpitisha kwa kuwa walimuona anafaa na anaweza kukijenga chama.

“Ndani ya chama kuna wazee wenye busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua mgombea kwani unaweza kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi hivyo, unaweza vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye ushindi.

“Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini siwezi kukubaliana naye anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa sahihi, kila mtu ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa…, tuna imani naye na anaweza kuongoza tangu zamani,” alisema Makamba.

Makamba alisema, ana imani kwamba atafanya vizuri hivyo ni bora apewe ushirikiano kama walivyopewa viongozi waliopita ili kukinusuru Chama cha Mapinduzi na watu waendelee kukiheshimu kama awali.

Katibu mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema kwamba, watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli wana masilahi binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho.

Kauli ya Kingunge

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki, Katibu huyo wa zamani wa halmashauri kuu ya CCM alisema, Kamati ya Usalama na Maadili iliteka majukumu ya Kamati Kuu baada ya kuamua kuchuja majina ya makada waliojitokeza kuwania urais hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo zilifanywa kwa kuvunja kanuni na zililenga kumuengua Lowassa kuwania kuingia Ikulu.

Kingunge alisema kitendo cha kumuengua Lowassa kwa kuvunja kanuni kimeacha kasoro kubwa ndani ya chama hicho tawala kwa sababu taratibu zilikiukwa ili kupata viongozi.

Alisema kosa hilo siyo la Dk Magufuli aliyepitishwa kuwa mgombea urais wa CCM, na wala si la Lowassa, bali ni la waliopendekeza majina ya walioingia tano bora.

Jina la Lowassa, ambaye alijidhihirisha kukubalika ndani na nje ya CCM kutokana na harakati zake za kusaka wadhamini kujaa watu, halikupelekwa kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kingunge na hivyo kutojadiliwa na chombo hicho ambacho kilimpitisha Dk Magufuli, Dk Asha-Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali

Chanzo: Mwananchi, July 18, 2015

Overrated politician who rode on his dad's political cocktail,his name is January Makamba.
 
Huyu nae kachanganyikiwa baada ya kutemwa urais
 
Kwanza huyo makamba alipitishwa kuingia kwenye 5 bora kwa mizengwe,hakuwa na sifa ya kuwapita lowasa,na mwandosya na wasira.ni afadhali afunge mdomo wake
 
January ana haki ya kusema ivyo coz cdhani hata kama kadi yake ya mwanachama ina miaka zaid ya 10 toka kapewa coz huyu jamaa ni kijana wa mr invisble na yeyey alikuwa plan D ya mr invisble bt plan B akashinda na amesha jua ni post gani atapewa so ni lazima aseme maneno hayo bt cdhani kama mzee kingunge mwenye kadi namba 8 atakuwa akijui chama kama huyo mtoto wenye kadi ambayo hata miaka 10 aina toka kapata
 
View attachment 269016

Kingunge yuko sawa kwa kulalamikia utaratibu haukufuatwa, kwa maneno ya Makamba tutegemee ccm na kuendelea kutofuata taratibu hata watakaposhinda uchaguzi
 
Huyu jamaa bora angekaa kimya tu akaonekana ana busara kuliko kujifanya ana uchungu sana na chama ilhali kuna wenye hadi kadi za iliyokuwa TANU wanaangalia tu upepo unavyovuma.

Hiyo top 5 yenyewe kawekwa kimkakati tu kwa ajili ya 2025.
 
Kwanza huyo makamba alipitishwa kuingia kwenye 5 bora kwa mizengwe,hakuwa na sifa ya kuwapita lowasa,na mwandosya na wasira.ni afadhali afunge mdomo wake

ccm wanataka kuueleza umma kwamba demokrasia ni kukubali kila kitu hata kama utaratibu haukufuatwa hakuna kuoji wala kuuliza. ccm ni janga
 
Kwanza huyo makamba alipitishwa kuingia kwenye 5 bora kwa mizengwe,hakuwa na sifa ya kuwapita lowasa,na mwandosya na wasira.ni afadhali afunge mdomo wake

Janaurı na Mwiguru walikuwa na sifa kuliko Edo.Edu anachangiwa fedha na majambazii ili aingie nyumba nyeupee??Mwinyewe mwz, anachangiwa na wezi alafu mnampigia chapuo??Lazima nyie mtakuwa wehu si bure.Nchi za watu Edo asıngefka hata kwenye mchujo.Hafaı,hafai na ningejitoa muhanga km angepitishwa.
 
January ana haki ya kusema ivyo coz cdhani hata kama kadi yake ya mwanachama ina miaka zaid ya 10 toka kapewa coz huyu jamaa ni kijana wa mr invisble na yeyey alikuwa plan D ya mr invisble bt plan B akashinda na amesha jua ni post gani atapewa so ni lazima aseme maneno hayo bt cdhani kama mzee kingunge mwenye kadi namba 8 atakuwa akijui chama kama huyo mtoto wenye kadi ambayo hata miaka 10 aina toka kapata

Kweli mkuu naona unamuelwa vizuri huyu makamba
 
February kaakomya acha utotoo wamekufanya msukule kwenye list..usibweteke ukumbukwe kwenye uwaziri..magufuli kawashtukia wengi mliingia na nia mkumbukwe uwaziri...
 
Haya, huyu bwana mdogo naye anadhani ubunge wa viti maalumu ni swa na wa kugombea! Ngoja akayajue madhira ya
kupita bila kupingwa safari hii.

Mkuu hoja yako ina uhusiano gani katika mada tajwa hapo juu
 
Kingunge yuko sawa kwa kulalamikia utaratibu haukufuatwa, kwa maneno ya Makamba tutegemee ccm na kuendelea kutofuata taratibu hata watakaposhinda uchaguzi

Mkuu mpasuko ndani ya ccm utaendelea kuwepo kwani kila kiongozi aliye madarakani anataka chama kitekeleze matakwa yake
 
Hana lolote jema huyo Makamba, hatuwasikilizi tena mbumbumbu, Kingunge sema tu usikike.
 
Kwanza huyo makamba alipitishwa kuingia kwenye 5 bora kwa mizengwe,hakuwa na sifa ya kuwapita lowasa,na mwandosya na wasira.ni afadhali afunge mdomo wake

Acha blah blah thibitisha kwa takwimu kuwa hakuwa na sifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom