Januari Makamba: Piga marufuku ukataji matawi ya miti kama kiashiria cha gari kuharibika barabarani

Right3

Senior Member
Aug 16, 2015
193
233
Imekua ni mazoea kukuta magari makubwa yameharibika na kuona matawi mengi ya miti yamekatwa na kuwekwa barabarani kama ishara kwa watumiaji wengine wa bara bara ili kuchukua tahadhari.
Lakini ni mara kwa mara magari haya yakitengemaa wahusika huanza safari na kuacha haya matawi barabarani.
Haya yamekua yakileta usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa barabara wafikapo eneo hilo na pia ni uharibifu wa mazingira.
Suluhisho: Waziri kutaneni na wadau wa usafirishaji mkubaliane na mwishowe muwape kazi wachina wadesign triangles kubwa ambazo hazitadondoka maeneo zitakapowekwa ili kuonyesha ubovu wa gari mbele na naamini gari likitengemaa baada ya ubovu watabeba triangle zao.

Baada ya kuleta hizo triangle kubwa marufuku ipigwe kukata miti yetu hovyo kwa ajili ya kuweka barabarani na atakayeenda kinyume basi sheria ichukue mkondo wake.
 
Very weak reason..... kwani wanakata miti mingapi? Siwanaepusha ajali nyingi kwakufanya hivo
 
Nafikiri ifike mahali tuache kuishi kienyeji na si kweli wanakata nyasi ni matawi ya miti tena makubwa naiona sana hiyo bara bara ya Mbeya-Tunduma.
Sio sahihi kusema ni manyasi badala ya miti inabidi tufike mahala tuishi kistaarabu kuliko kukata matawi ya miti ukiharibikiwa gari likitengenezwa matawi yanaachwa.
 
May be huwa unaona hayo matawi ukiwa unaendeshwa! Nikwambie kitu asilimia kubwa ya ajali husababishwa na cheche yaani gari bovu ghafla, ukiwa speed mbele kuna kona na kuna gari imeharibika haijaweka alama au hicho ki triangle mara nyingi wanaoweka triangle huwa zinakuwa karibu na gari zinaweza dodondoka aisee hamad cheche hili hapa na kulia kwako kuna gari inakuja acha utaita majina yote. Waendelee kuweka matawi tena nasisitiza gari ikiharibika weka matawi ya kutosha pande zote mbili, naongea kwa experience maana kwa mwezi natembea km 5000 mpaka 10000kms kwa hiyo naelewa changamoto za barabara zetu vizuri sana. Weka matawi acha kabisa story za ulaya kwa barabara zetu za ki tz.
 
Hoja yako ingekuwa kuondolewa kwa matawi baada ya tatizo la gari kuisha, vinginevyo lazima tuitumie miti iliyo kando ya barabara kwa usalama wa maisha yetu.
Usalama wa maisha ya watanzania ni muhimu kuliko vitawi vya miti
 
May be huwa unaona hayo matawi ukiwa unaendeshwa! Nikwambie kitu asilimia kubwa ya ajali husababishwa na cheche yaani gari bovu ghafla, ukiwa speed mbele kuna kona na kuna gari imeharibika haijaweka alama au hicho ki triangle mara nyingi wanaoweka triangle huwa zinakuwa karibu na gari zinaweza dodondoka aisee hamad cheche hili hapa na kulia kwako kuna gari inakuja acha utaita majina yote. Waendelee kuweka matawi tena nasisitiza gari ikiharibika weka matawi ya kutosha pande zote mbili, naongea kwa experience maana kwa mwezi natembea km 5000 mpaka 10000kms kwa hiyo naelewa changamoto za barabara zetu vizuri sana. Weka matawi acha kabisa story za ulaya kwa barabara zetu za ki tz.
Mtoa mada hajai changamoto za barabara zetu hasa maeneo yenye kona kali. muda mwingine unatakiwa kuweka alama zaidi ya mita 300 ili kuepusha ajali, na hii ni kutokana na kona kali au maeneo yenye milima na mabonde.
 
Back
Top Bottom