Tangu mwaka huu uanze dunia imekuwa kwenye mtanziko mkubwa juu ya janga linalotishia uhai wa binadamu na uhai wa uchumi wa dunia, si lingine ni janga la covid-19 au Corona virus.
Hakuna anayebisha kwamba janga hili limetikisa dunia! Tunaona dunia inavyohangaika!
Hapo kwenye kuhangaika kudhibiti Ugonjwa huo ndo kunanipa maswali mengi!
Katika nchi nyingi shule zimefungwa, vyuo, ofisi mbalimbali, huduma za usafiri hasa wa ndege, Taasisi mbalimbali zimesimamisha kazi zake, wafanyakazi wako nyumbani!
Baadhi ya nchi zimeenda mbali zaidi na kulazimika kuwafungia ndani wananchi wake (lockdown)
Kila siku tunapewa takwimu za vifo na maambukizi mapya ya mataifa mbalimbali.
Takwimu zinapanda kila siku kiasi kwamba nchi zinazoripoti kiasi kidogo cha maambukizi zinatiliwa mashaka kuficha taarifa.
Nchi ambazo zimeripoti kutokuwa na maambukizi ya Corona zinaanza kutiliwa mashaka kwamba huenda hawana vifaa thabiti!
Nchi nyingi za dunia ya tatu zimepata maambukizi kutoka nje! Yaani Ugonjwa umekuja na watu!
Kwanini tunalazimisha kila nchi iwe na wagonjwa? Kwanini tutilia mashaka nchi zenye maambukizi kidogo? Kwanini tulazimishe takwimu za kila siku?
Hivi kupewa taarifa kila siku hatuoni kwamba kunaongeza taharuki na hofu kwenye jamii?
Kwanini tusimamishe shughuli za uzalishaji kwa kuwafungia watu ndani badala ya kufunga mipaka?
Shule , baadhi ya ofisi, na Taasisi mbalimbali zimesimamisha shughuli zake hata zile ambazo hazina muingiliano na wageni! Wakati huo huo sehemu zenye muingiliano na wageni zimeachwa huru! Tuko sahihi?
Baadhi ya nchi zimefungia watu wake ndani, wakati huo huo mipaka na viwanja vya ndege viko huru kupokea wageni!? Hii ni sahihi kweli wakati Ugonjwa haujaanzia ndani?
Hii Corona inaweza kuwa mwanzo wa matatizo mengine makubwa hasa ya kiuchumi.
Ukiangalia mbinu zinazotumika kuuzuia, ni mbinu zinazohamasisha uchumi kudidimia! Watu kukaa ndani!?!? Ofisi kufungwa!?!? Shule kufungwa!?!?
Tumekumbana na majanga mangapi na hatukufikia huko!? Leo kampeni ya dunia ni kuzuia watu wasiendelee na utaratibu wa Maisha waliyoyazoea.
Tusipuuze Maneno ya China kwa Marekani! Huenda Corona ni zaidi ya Ugonjwa, imelenga kuuwa uchumi wa dunia!
Sent using Jamii Forums mobile app