hahaha kaka mchanga wa Bahari una chumvi,chumvi ni hatari kwa ujenzi kwani jengo linajengwewa na mchanga wa baharini halidumuaiseee
Hivi hawa jamaa si wamezungukwa na bahari pande zote??
Au si kila mchanga unafaa kwa ujenzi??
Zanzibar ni nchi? Kwanini wasichukue mchanga bagamoyo? Nje ya nchi ndiyo wapi?Hamad Rashid ametangazia dunia kwamba Nchi ya Zanzibar imeishiwa mchanga kwaajili ya Ujenzi, hivyo wameruhusu kuagiza mchanga toka nje bila kodi.
Serikali ya Zanzibar imeomba wadau wajitokeze kuagiza mchanga nje ya nchi ili ujenzi uweze kuendelea.
Kwa sasa lori la mchanga linauzwa kwa laki moja na na bado haupatikani kwani kila sehemu walipokuwa wanachimba umeisha.
========
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekusudia kuagiza mchanga nje ya nchi kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa rasilimali hiyo hapa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na uvuvi Hamad Rashid amesema Zanzibar haina mchanga utakaokidhi mahitaji ya ujenzi kutokana na kiwango kikubwa cha rasilimali mchanga kuchimbwa kwa kasi unguja na pemba.
Hata hivyo amesema ili kupunguza tatizo hilo lazima serikali kutumia matumizi mbadala wa mchanga katika harakati za ujenzi au mbinu za kutumia mchanga kidogo na kubuni rasilimali nyengine badala ya mchanga ili kupunguza tatizo ambalo linaathiri hapa nchini.
Aidha amesema hali imekuwa mbaya kutokana na matumizi mabaya ya ardhi inayosababisha athari kuongezeka hivyo serikali inatumia hatua za dharura kudhibiti uchimbwaji wa mchanga lazima utaratibu wa utoaji vibali ubadilike kutokana na upungufu uliopo ili kudhibiti rasilimali chache ilobaki.
Ametoa wito kwa wananchi kuwacha kuchimba mchanga kiholela na wanaochimba katika maeneo ya kuvunia kuwachana na serikali itatenga maeneo mbadala yatakayo tumika kwa shughuli hizo na kwa utaratibu maalum.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni kwa Unguja na Pemba imeonesha kuwa Unguja inachimba hekta 3 kila mwezi na Pemba nusu hekta kila mwezi ambapo kwa mwaka 2016 uchimbaji huo umefikia tani Million moja laki nane na arobaini na sita elfu.
Credit: Amina Omar mwanahabari wa Zanzibar
Zanzibar si ni nchi? Sasa nchi inaanzaje kuishiwa bidhaa basic kama mchanga? Waambie waje waokoteze ule mchanga ambao Karume alichanganya na Nyerere kisha wakaumwaga huku bara, angalau watajaza kisado kimoja...
Kwa dola? Ina maana tuta export?Jaza mchanga toka kunduchi beach na Msimbazi WAUZIENI!
YES!!!!!!!Kwa dola? Ina maana tuta export?
Naona wenyewe wana create mazingira ya kuliwa pesa.YES!!!!!!!
Kwan sirikiali ya Zanzibar si ndio serikali ya tz si wasaidiane tuHamad Rashid ametangazia dunia kwamba Nchi ya Zanzibar imeishiwa mchanga kwaajili ya Ujenzi, hivyo wameruhusu kuagiza mchanga toka nje bila kodi.
Serikali ya Zanzibar imeomba wadau wajitokeze kuagiza mchanga nje ya nchi ili ujenzi uweze kuendelea.
Kwa sasa lori la mchanga linauzwa kwa laki moja na na bado haupatikani kwani kila sehemu walipokuwa wanachimba umeisha.
========
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekusudia kuagiza mchanga nje ya nchi kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa rasilimali hiyo hapa nchini.
View attachment 465030
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na uvuvi Hamad Rashid amesema Zanzibar haina mchanga utakaokidhi mahitaji ya ujenzi kutokana na kiwango kikubwa cha rasilimali mchanga kuchimbwa kwa kasi unguja na pemba.
Hata hivyo amesema ili kupunguza tatizo hilo lazima serikali kutumia matumizi mbadala wa mchanga katika harakati za ujenzi au mbinu za kutumia mchanga kidogo na kubuni rasilimali nyengine badala ya mchanga ili kupunguza tatizo ambalo linaathiri hapa nchini.
Aidha amesema hali imekuwa mbaya kutokana na matumizi mabaya ya ardhi inayosababisha athari kuongezeka hivyo serikali inatumia hatua za dharura kudhibiti uchimbwaji wa mchanga lazima utaratibu wa utoaji vibali ubadilike kutokana na upungufu uliopo ili kudhibiti rasilimali chache ilobaki.
Ametoa wito kwa wananchi kuwacha kuchimba mchanga kiholela na wanaochimba katika maeneo ya kuvunia kuwachana na serikali itatenga maeneo mbadala yatakayo tumika kwa shughuli hizo na kwa utaratibu maalum.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni kwa Unguja na Pemba imeonesha kuwa Unguja inachimba hekta 3 kila mwezi na Pemba nusu hekta kila mwezi ambapo kwa mwaka 2016 uchimbaji huo umefikia tani Million moja laki nane na arobaini na sita elfu.
Credit: Amina Omar mwanahabari wa Zanzibar
Kwa hiyo baada ya hizo chini panakua tupu!!!Zimebaki hector 4 tu za mchanga
Hii ni hatari.