Janga jipya: Zanzibar yaishiwa Mchanga, sasa kuagizwa nje ya nchi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,484
Hamad Rashid ametangazia dunia kwamba Nchi ya Zanzibar imeishiwa mchanga kwaajili ya Ujenzi, hivyo wameruhusu kuagiza mchanga toka nje bila kodi.
16387173_10154987811204339_7125259314100577276_n.jpg

Serikali ya Zanzibar imeomba wadau wajitokeze kuagiza mchanga nje ya nchi ili ujenzi uweze kuendelea.

Kwa sasa lori la mchanga linauzwa kwa laki moja na na bado haupatikani kwani kila sehemu walipokuwa wanachimba umeisha.

========

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imekusudia kuagiza mchanga nje ya nchi kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa rasilimali hiyo hapa nchini.
image.jpeg

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Waziri wa kilimo Maliasili Mifugo na uvuvi Hamad Rashid amesema Zanzibar haina mchanga utakaokidhi mahitaji ya ujenzi kutokana na kiwango kikubwa cha rasilimali mchanga kuchimbwa kwa kasi unguja na pemba.

Hata hivyo amesema ili kupunguza tatizo hilo lazima serikali kutumia matumizi mbadala wa mchanga katika harakati za ujenzi au mbinu za kutumia mchanga kidogo na kubuni rasilimali nyengine badala ya mchanga ili kupunguza tatizo ambalo linaathiri hapa nchini.

Aidha amesema hali imekuwa mbaya kutokana na matumizi mabaya ya ardhi inayosababisha athari kuongezeka hivyo serikali inatumia hatua za dharura kudhibiti uchimbwaji wa mchanga lazima utaratibu wa utoaji vibali ubadilike kutokana na upungufu uliopo ili kudhibiti rasilimali chache ilobaki.

Ametoa wito kwa wananchi kuwacha kuchimba mchanga kiholela na wanaochimba katika maeneo ya kuvunia kuwachana na serikali itatenga maeneo mbadala yatakayo tumika kwa shughuli hizo na kwa utaratibu maalum.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni kwa Unguja na Pemba imeonesha kuwa Unguja inachimba hekta 3 kila mwezi na Pemba nusu hekta kila mwezi ambapo kwa mwaka 2016 uchimbaji huo umefikia tani Million moja laki nane na arobaini na sita elfu.

Credit: Amina Omar mwanahabari wa Zanzibar
 
Wafungue kiwanda cha kuutengeneza kwani wakiuchukua wa Tanganyika iko siku utasababisha ukoloni wa Machogo urudi kwa kasi sana Zanzibar!!
 
Nimeshangazwa kuadimika kwa mchanga huko Zanzibar, haya ni maajabu. Ni laana au? Hivi wengine wanalalamika kuadimika kwa mvua, chakula, sukari, mwenyewe udongo. Haya majanga mie nadhani ni........ Kha nchi yetu haiishi vituko.
 
Waziri wa kilimo na mifugo na uvuvi wa Zanzibar ndugu Hamadi Rashid Mohamedi nakumbuka alikuwa ameanzisha chama chake Alisha achana nacho nini nijuzeni mwenzenu.
 
sawa siwachimbe tu fukwen ili kuongeza kina cha Bahari....Holand walidanya ivyo ndio maana meli zinapita mpaka Mitaani
 
Back
Top Bottom