JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Mnamo tarehe 19 Oktoba 2018, JamiiForums ilifanya mafunzo mahususi kwa ajili ya bloggers wa Tanzania. Mafunzo hayo yalijikita katika kuwapa uwezo bloggers wa kufanya kazi zao za kuhabarisha, kuburudisha na kufundisha jamii.
Mafunzo yalifanyika katika hoteli ya New Africa iliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa siku nzima na yalihusisha bloggers 21 kutoka nyanja mbalimbali kama habari za kitaifa, siasa, mitindo, michezo na burudani.
Mkufunzi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Bwana Maxence Melo alifundisha kuhusu mambo mbalimbali kuanzia jinsi ya kuchagua jina kwa ajili ya blog au tovuti yako, kupata hakimiliki na jinsi ya kuwekea blog yako ulinzi.
Pia kulikuwa na mjadala kuhusu ubora wa maudhui(content quality) na jinsi ya kutengeneza maudhui yanayoridhisha. Hapa bloggers walipewa mbinu za kuwawezesha kuwa na maudhui anuai na yaliyoshiba kwa ajili ya watumiaji wa mtandao ili kupata wasomaji wengi zaidi.
Miongoni kwa bloggers waliohudhuria, wapo pia waliositisha kazi zao kutokana na Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni kuwabana kwa kushindwa kulipa kiasi kilichowekwa ili kuendelea na shughuli mtandaoni.
Katika kulizungumzia hili, Maxence aliwaambia licha ya kushindwa kufanya kazi kutokana na kukosa pesa lakini kama bloggers kwa ujumla wao ni muhimu kuangalia mbali zaidi katika athari za kanuni hata pale watakapolipia leseni.
Katika kufunga mafunzo haya, Maxence aliwaachia bloggers Kazi ya kuhakikisha wanawalisha watanzania maudhui yaliyo bora na yenye lengo la kukuza nchi kiuchumi, kiutamaduni na kujenga jamii bora.
Pia aliwaasa kutokata tamaa na kuendelea kupambana hata katika nyakati ngumu ili kutimiza ndoto zao.