JamiiForums yalamba tuzo mbili kwa kupigania haki za kidigitali Tanzania

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,718
220,800


Tuzo moja ni ya kuhusu Taasisi bora inayotetea na kuhamasisha haki za kijamii na kisiasa mitandaoni, tuzo ya pili inahusu Taasisi bora kiongozi isiyo ya kiserikali inayofanya uchechemuzi wa masuala ya kidigital na uwajibikaji.

JF Imewashukuru waandaaji wa Tuzo hizo Tanzania Digital Award (TDA) Kwa kutambua mchango wa JF katika kuhamasisha haki za kidigital.

Mungu ibariki JF
 
Sikufanya kosa kujiunga na JF. Unaweza kunichukulia kama mchezaji wa reserve wa timu kubwa kama Simba, ambaye hucheza mazoezini tu.

Hatahivyo Nimepokea maua!

Heko JamiiForums na mamebers wote.
 
Kongole kwa viongozi wa JAMIIFORUMS


Kongole kwake ndg. Maxence Mello


Kongole kwa "staff" wote wa JF


Tuzo hizi mbili ni NZITO haswaa!!

Kila la heri kwa JF kuendelea kuwa mfano wa "digital forums" nyingine na la mno ni kuendelea kuzizoa tuzo nyingi zaidi ,amen


#SiempreJMT

#TanzaniaKwanzaKablaYaNafsiZetu
 
 
Sikufanya kosa kujiunga na JF. Unaweza kunichukulia kama mchezaji wa reserve wa timu kubwa kama Simba, ambaye hucheza mazoezini tu.

Hatahivyo Nimepokea maua!

Heko JamiiForums na mamebers wote.
Unayo namna yako ya kutumia maneno kiufundi sana, lakini kwa mpangilio wa kipekee kabisa na kufikisha ujumbe.

Sijui ngazi yako ni ipi, lakini kama ungekuwa mwandishi (makala/vitabu/majarida), nadhani ungekuwa mwandishi mzuri sana.

Sasa sijui, kama hili umelisomea, au ni kipaji tu ulichojaaliwa na Mwenyezi Muumba wako.
 
Asante kwa taarifa, Big Up JF, Big Up Maxence Melo , big up sana wana jf kwa ujumla wetu!.
P
 
Yule Nsala yuko wapi? Nshomile kayeyuka?
yupo sana tena sana. Kamfuate magufuli mume wako. lakini mlipigwa na kiu kizito hamtakuja kusahahu. Mungu ni fundi, akatuondolea shetani Luciferi. badi jingine nalo siku si nyingi Mungu atatenda
 
Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda waanzilishi Max Melo & Mike Mushi pamoja na wafanyakazi wote, bila kusahau mchango mkubwa wa members wote, Mungu ibariki Jamiiforum Mungu ibariki Tanzania.
 
Big ups!!
 
Hidumu Jamii forum
Miaka yangu kumi na tano ndani ya jf sijawahi juta
Sijutii kuichagua jf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…