JF ni kila kitu kwangu,
Naiweka kwenye ratiba zangu,
Nawajua wabaya na Mungu,
Kuna mambo matamu na machungu,
JF iko juu kama sky
Kuanzia siasani, MMU hadi michezoni,
Tapata kitu maishani,
JF hakika imesheheni,
Iko juu kama sky
Wapo marafiki na wanafiki,
Watu wanakera na mahakamani hatufiki,
Like na komenti kama mkuki,
JF iko juu kama sky
Kutana na wanazuoni na wapambanaji,
Shuhudia wenye soni na waongeaji,
Tazama wapizani, na akina
gwijimimi
JF ni tishio
Kivutio majina ya ID zitumikazo,
Hazifanani na watu wazitumiazo,
Na ukiwataja ni mzozo,
JF ni gumzo
JF ni chanzo cha ukakika,
Habari na taarifa kote Afrika,
Asia, Ulaya na Amerika,
Kote huko members wamefika,
JF ni kitu ingine