Mungu Mweusi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 1,474
- 1,086
Hiyo mbuni na masikini wa mwisho anataka aache majonzi ya watoto na familia Kisa laki 9? Si angeomba Tu umsamehe deni?
Hahahaha acha kabisa kaka... mpaka sasa nashangaa... halafu ntakutafuta kaka sijakuona long timeNakuona jinsi unavyomdharau..
Mimi kuna mtu kanirusha laki mbili tu. Ila nafikiria sana na kujichekea rohoni, hivi kama laki mbili inamtoa mtu uaminifu atakuja kuishi maisha ya aina gani hapa duniani?
Kweli, Jf inatoa elimu na maarifa kwa yenye manufaa.Ni gesti gani hapo mtaa wa rufiji? Kuna kitwima,sumaye hotel, na ile pale karibu na wanapouza mafriji used. Kama ni Kweli usemayo na si hadithi ya kutunga,kuna Kituo cha polisi hapo cha mirongo masaa 24 kinafanya kazi, kwanini hukwenda kutoa taarifa mtego uwekwe? Ulishauriwa na mhudumu,kwanini hukuzingatia? Au madai yenu yalikuwa yamepatikana kwa njia isiyoWiki hii mwanzoni ,nilisoma topic isemayo "Mungu atakulipia Frank ".
ilihusu habari za jamaa Frank ambaye alikuwa akimdai mtu sh mil 2, baadae akampigia simu na Kumwita aende vingunguti ili akamlipe, kufika huko akampigia kelele za mwizi, Frank akawa ameuawa.
Nilisikitika Sana baada ya kusoma habari hiyo.
Majuzi nami nikapigiwa simu na mtu ninayemdai sh 900,000 ,yupo Mwanza, mimi nipo Geita ,akadai atanitumia nauli ili niende Mwanza, na pia anipangishie Guest house na kesho yake anilipe.
Nilijiuliza maswali mengi sana, Kwa nini hadi niende Mwanza? Kwa nini asinirushie tu Kwa Mpesa?
Niliogopa kwenda Mwanza, ila sikumwambia Kama naogopa kwenda.
Niliogopa Kwa Sababu alikuwa ameonyesha dalili za kunidhulumu kabisa.
Baadae nilimwambia anirushie nauli, akawa ametuma.
Kesho yake nilianza safari kwenda Mwanza, nikiwa ndani ya basi, taa ya tahadhari iliwaka kichwani mwangu baada ya kukumbuka tukio la marehemu Frank, nilihisi na mimi huu ulikuwa ni mtego wangu.
Nikaamua kuchukua tahadhari ya hali ya juu Sana.
Baada ya kufika Mwanza nilimpigia simu mdeni wangu, akaniuliza mahali nilipo, nikamwambia anielekeze tu Guest house aliyonichukulia nami ningeonana naye pale maana nilikuwa bado na mizunguko mingi.
Alinielekeza hiyo guest house, ipo maeneo ya mtaa wa Rufiji mjini kabisa, kisha nikamwambia nitakuwa hapo kuanzia saa 4 usiku.
Kabla ya saa 4 usiku kufika, saa moja na nusu usiku niliwasili kwenye hiyo guest house na kumkuta dada mmoja hivi muhudumu, nilipojitambulisha tu akanionyesha chumba, sikuingia ndani ya chumba, nilimwomba Yule dada Niongee naye, alipokubali nikamweleza kuwa simwamini huyu mtu aliyenichukulia chumba, nilimweleza Kwa kina akaridhika, akaniambia vp awataarifu police?
Nikamwambia asubiri kwanza Hadi tujiridhishe.
Niliondoka na kwenda kula, nikarudi saa 3,kisha Nikamwomba yule dada nikae kwenye chumba chake ili nijue kinachoendelea, yule dada aligoma, nikaamua kumnunulia bia, na sote tukawa tunakunywa.
Ilipotimia saa 3:30 usiku ule, mdeni wangu alinipigia simu akaniuliza Kama nipo tayari kwenye hiyo guest house, nikamjibu kuwa nipo njiani naelekea huko na nikifika nampigia.
Yule muhudumu alikubali kunihifadhi Kwa muda kwenye chumba chake, ili yeye aangalie kinachoendelea.
Saa 4:30 usiku ule mdeni wangu alinipigia simu na kusema kuwa angekuja saa 5 usiku pale guest ili aniachie pesa kidogo na kesho anilipe kabisa, nikamjibu kuwa angenikuta tu.
Na kweli mida ya saa 5 usiku ule, wanaume wawili wa miraba minne walifika pale kwenye ile guest house kuniulizia, niliwachungulia kupitia tundu la funguo cha ajabu mdeni wangu hakuwepo.
Yule muhudumu aliwajibu kuwa sijafika bado Kama vipi warudi baadae.
Wakati wanaondoka aliwafuatilia na kuwaona wakiingia kwenye gari ndogo nyeupe yenye vioo vyeusi.
Wanajamvi baada ya hapo, saa 6 usiku walirudi tena na yule dada akawajibu kuwa sijarudi, mdeni wangu akanipigia simu kuniulizia nilipo sikupokea.
Waliondoka huku wakifyonza, niliogopa kutoka nje, nikalala ndani ya chumba cha yule dada hadi saa 12 alfajiri nikaondoka.
Maswali ya kujiuliza, wale watu walikuwa ni kina nani? na Kwa nini mdeni wangu hakutokea?
Nilimpigia simu na kumwambia kuwa nilibaini njama zake za kunidhuru au kuniua hakujibu kitu akazima simu Kwa aibu hadi leo.
Kama siyo JF na ile makala ya marehemu Frank, ningeingia mkenge na kuuawa, Asante Sana Jamiiforums, Wanajamvi tujifunze kutokuamini wanadamu, nimepata somo kubwa sana.
Nipo kaka. Ni kitambo sana hatujaonana.Hahahaha acha kabisa kaka... mpaka sasa nashangaa... halafu ntakutafuta kaka sijakuona long time
Wiki hii mwanzoni ,nilisoma topic isemayo "Mungu atakulipia Frank ".

Wasingemuua ila wangemla kalio hadi asubuhiPole sana kwa mkasa na hongera kwa kuepuka kifo...watu wasenzi sana yani umuue MTU kwa ajili ya sh laki Tisa?