JamiiForums imeniokoa na Kifo

JamiiForums imeniokoa na Kifo

Hongera mkuu kwa kutegua mtego. Mshukuru Mungu.
 
Wewe kma ulishindwa kuwaarifu police basi ilo deni lenu lina uwakini
 
Ubinadamu kazi kukopa kwa watu huwa rahisi na mtu anakuja na shida zake akiwa anatia huruma
Tatizo linakuja kwenye kulipa ndo kasheshe hadi ugomvi
....kukopa dukani kulipa polisi...pole mkuu
 
Mkuu hamu ya kumgonga unadhani ingetokea wapi?
Tulilala Kama mtu na dada yake hadi alfajiri, sote tukiwa na nguo, tena mzungu Wa nne.
...na kwa kumuexpose hivi hudhani kama unamuweka hatarini?
..ama maadamu yako yamejiishia,yeye atajijua?
 
Wiki hii mwanzoni ,nilisoma topic isemayo "Mungu atakulipia Frank ".
ilihusu habari za jamaa Frank ambaye alikuwa akimdai mtu sh mil 2,baadae akampigia simu na Kumwita aende vingunguti ili akamlipe, kufika huko akampigia kelele za mwizi, Frank akawa ameuawa.
Nilisikitika Sana baada ya kusoma habari hiyo, majuzi nami nikapigiwa simu na mtu ninayemdai sh 900,000 ,yupo Mwanza, mimi nipo Geita ,akadai atanitumia nauli ili niende Mwanza, na pia anipangishie Guest house na kesho yake anilipe.
Nilijiuliza maswali mengi sana, Kwa nini hadi niende Mwanza? Kwa nini asinirushie tu Kwa m pesa?
Niliogopa kwenda Mwanza, ila sikumwambia Kama naogopa kwenda.
Niliogopa Kwa Sababu alikuwa ameonyesha dalili za kunidhulumu kabisa.
Baadae nilimwambia anirushie nauli, akawa ametuma.
Kesho yake nilianza safari kwenda Mwanza, nikiwa ndani ya basi, taa ya tahadhari iliwaka kichwani mwangu baada ya kukumbuka tukio la marehemu Frank, nilihisi na mimi huu ulikuwa ni mtego wangu.
Nikaamua kuchukua tahadhari ya hali ya juu Sana.
Baada ya kufika Mwanza nilimpigia simu mdeni wangu, akaniuliza mahali nilipo, nikamwambia anielekeze tu Guest house aliyonichukulia nami ningeonana naye pale maana nilikuwa bado na mizunguko mingi.
Alinielekeza hiyo guest house, ipo maeneo ya mtaa wa Rufiji mjini kabisa, kisha nikamwambia nitakuwa hapo kuanzia saa 4 usiku.
Kabla ya saa 4 usiku kufika, saa moja na nusu usiku niliwasili kwenye hiyo guest house na kumkuta dada mmoja hivi muhudumu, nilipojitambulisha tu akanionyesha chumba, sikuingia ndani ya chumba, nilimwomba Yule dada Niongee naye, alipokubali nikamweleza kuwa simwamini huyu mtu aliyenichukulia chumba, nilimweleza Kwa kina akaridhika, akaniambia vp awataarifu police?
Nikamwambia asubiri kwanza Hadi tujiridhishe.
Niliondoka na kwenda kula, nikarudi saa 3,kisha Nikamwomba yule dada nikae kwenye chumba chake ili nijue kinachoendelea, yule dada aligoma, nikaamua kumnunulia bia, na sote tukawa tunakunywa.
Ilipotimia saa 3:30 usiku ule, mdeni wangu alinipigia simu akaniuliza Kama nipo tayari kwenye hiyo guest house, nikamjibu kuwa nipo njiani naelekea huko na nikifika nampigia.
Yule muhudumu alikubali kunihifadhi Kwa muda kwenye chumba chake, ili yeye aangalie kinachoendelea.
Saa 4:30 usiku ule mdeni wangu alinipigia simu na kusema kuwa angekuja saa 5 usiku pale guest ili aniachie pesa kidogo na kesho anilipe kabisa, nikamjibu kuwa angenikuta tu.
Na kweli mida ya saa 5 usiku ule, wanaume wawili wa miraba minne walifika pale kwenye ile guest house kuniulizia, niliwachungulia kupitia tundu la funguo cha ajabu mdeni wangu hakuwepo.
Yule muhudumu aliwajibu kuwa sijafika bado Kama vipi warudi baadae.
Wakati wanaondoka aliwafuatilia na kuwaona wakiingia kwenye gari ndogo nyeupe yenye vioo vyeusi.
Wanajamvi baada ya hapo, saa 6 usiku walirudi tena na yule dada akawajibu kuwa sijarudi, mdeni wangu akanipigia simu kuniulizia nilipo sikupokea.
Waliondoka huku wakifyonza, niliogopa kutoka nje, nikalala ndani ya chumba cha yule dada hadi saa 12 alfajiri nikaondoka.
Maswali ya kujiuliza, wale watu walikuwa ni kina nani? na Kwa nini mdeni wangu hakutokea?
Nilimpigia simu na kumwambia kuwa nilibaini njama zake za kunidhuru au kuniua hakujibu kitu akazima simu Kwa aibu hadi leo.
Kama siyo JF na ile makala ya marehemu Frank, ningeingia mkenge na kuuawa, Asante Sana jamiiforums, Wanajamvi tujifunze kutokuamini wanadamu, nimepata Somo kubwa sana.
Pole sanaa ndugu yangu, mungu kakusaidia ni kweli kuna msemo unasema TRUST NO BODY.!! YAANI HUU MSEMO NIMEANZA KUAMINI
 
Wiki hii mwanzoni ,nilisoma topic isemayo "Mungu atakulipia Frank ".
ilihusu habari za jamaa Frank ambaye alikuwa akimdai mtu sh mil 2, baadae akampigia simu na Kumwita aende vingunguti ili akamlipe, kufika huko akampigia kelele za mwizi, Frank akawa ameuawa.

Nilisikitika Sana baada ya kusoma habari hiyo.

Majuzi nami nikapigiwa simu na mtu ninayemdai sh 900,000 ,yupo Mwanza, mimi nipo Geita ,akadai atanitumia nauli ili niende Mwanza, na pia anipangishie Guest house na kesho yake anilipe.

Nilijiuliza maswali mengi sana, Kwa nini hadi niende Mwanza? Kwa nini asinirushie tu Kwa Mpesa?

Niliogopa kwenda Mwanza, ila sikumwambia Kama naogopa kwenda.
Niliogopa Kwa Sababu alikuwa ameonyesha dalili za kunidhulumu kabisa.

Baadae nilimwambia anirushie nauli, akawa ametuma.

Kesho yake nilianza safari kwenda Mwanza, nikiwa ndani ya basi, taa ya tahadhari iliwaka kichwani mwangu baada ya kukumbuka tukio la marehemu Frank, nilihisi na mimi huu ulikuwa ni mtego wangu.

Nikaamua kuchukua tahadhari ya hali ya juu Sana.
Baada ya kufika Mwanza nilimpigia simu mdeni wangu, akaniuliza mahali nilipo, nikamwambia anielekeze tu Guest house aliyonichukulia nami ningeonana naye pale maana nilikuwa bado na mizunguko mingi.

Alinielekeza hiyo guest house, ipo maeneo ya mtaa wa Rufiji mjini kabisa, kisha nikamwambia nitakuwa hapo kuanzia saa 4 usiku.

Kabla ya saa 4 usiku kufika, saa moja na nusu usiku niliwasili kwenye hiyo guest house na kumkuta dada mmoja hivi muhudumu, nilipojitambulisha tu akanionyesha chumba, sikuingia ndani ya chumba, nilimwomba Yule dada Niongee naye, alipokubali nikamweleza kuwa simwamini huyu mtu aliyenichukulia chumba, nilimweleza Kwa kina akaridhika, akaniambia vp awataarifu police?

Nikamwambia asubiri kwanza Hadi tujiridhishe.
Niliondoka na kwenda kula, nikarudi saa 3,kisha Nikamwomba yule dada nikae kwenye chumba chake ili nijue kinachoendelea, yule dada aligoma, nikaamua kumnunulia bia, na sote tukawa tunakunywa.

Ilipotimia saa 3:30 usiku ule, mdeni wangu alinipigia simu akaniuliza Kama nipo tayari kwenye hiyo guest house, nikamjibu kuwa nipo njiani naelekea huko na nikifika nampigia.

Yule muhudumu alikubali kunihifadhi Kwa muda kwenye chumba chake, ili yeye aangalie kinachoendelea.

Saa 4:30 usiku ule mdeni wangu alinipigia simu na kusema kuwa angekuja saa 5 usiku pale guest ili aniachie pesa kidogo na kesho anilipe kabisa, nikamjibu kuwa angenikuta tu.
Na kweli mida ya saa 5 usiku ule, wanaume wawili wa miraba minne walifika pale kwenye ile guest house kuniulizia, niliwachungulia kupitia tundu la funguo cha ajabu mdeni wangu hakuwepo.

Yule muhudumu aliwajibu kuwa sijafika bado Kama vipi warudi baadae.
Wakati wanaondoka aliwafuatilia na kuwaona wakiingia kwenye gari ndogo nyeupe yenye vioo vyeusi.

Wanajamvi baada ya hapo, saa 6 usiku walirudi tena na yule dada akawajibu kuwa sijarudi, mdeni wangu akanipigia simu kuniulizia nilipo sikupokea.

Waliondoka huku wakifyonza, niliogopa kutoka nje, nikalala ndani ya chumba cha yule dada hadi saa 12 alfajiri nikaondoka.

Maswali ya kujiuliza, wale watu walikuwa ni kina nani? na Kwa nini mdeni wangu hakutokea?
Nilimpigia simu na kumwambia kuwa nilibaini njama zake za kunidhuru au kuniua hakujibu kitu akazima simu Kwa aibu hadi leo.

Kama siyo JF na ile makala ya marehemu Frank, ningeingia mkenge na kuuawa, Asante Sana Jamiiforums, Wanajamvi tujifunze kutokuamini wanadamu, nimepata somo kubwa sana.
Hongera pia yaani wangekubakia huko na kukudhuru huko huko
 
Nakupongeza kwa kuhepa mtego.. pia nakulaumu kwa kutushirikisha polisi wangetia adabu
 
Pole sana kwa mkasa na hongera kwa kuepuka kifo...watu wasenzi sana yani umuue MTU kwa ajili ya sh laki Tisa?
Umejuaje kama walitaka kumuua! Adhabu zipo nyingi tu.
 
Mkuu hamu ya kumgonga unadhani ingetokea wapi?
Tulilala Kama mtu na dada yake hadi alfajiri, sote tukiwa na nguo, tena mzungu Wa nne.
Dah...mbona ishu yenyewe iliisha poa? Ungemgonga tu.... inawezekana alikudharau..
 
Pole aisee,hivi kweli jamaa alitaka kukutoa roho kwa sh laki 9? Au kuja behind the scene? Kama ni hivyo kweli tuanaelekea pabaya.Alafu yule dada ukamnunulia bia ukakesha kwake hivi hivi tu? Ebu tupe na hizo michapo.
 
[]
Hawakua na kitu kama dawa ya meno?? Kama hiki
KYJelly.jpg
 
Kwahiyo umeamua kumuachia laki tisa zako ulizozipata kwa jasho kisa tu anataka kukudhuru?
 
Back
Top Bottom