JamiiForums imeniokoa na Kifo

JamiiForums imeniokoa na Kifo

pole sana mkuu,ila nadhani ulipaswa kuchukua hatua zaidi maana kama umegundua dhamira yake kwako anaweza asiishie hapo,kuwa mwangalifu na mienendo yako kwa sasa anaweza kukutegea mtego mwingine atimize azima yake.
Asante mkuu, naishi Kwa tahadhari kubwa sana, bahati nzuri, Hajui ni eneo gani naishi Geita na mimi si maarufu.
 
Wiki hii mwanzoni ,nilisoma topic isemayo "Mungu atakulipia Frank ".
ilihusu habari za jamaa Frank ambaye alikuwa akimdai mtu sh mil 2,baadae akampigia simu na Kumwita aende vingunguti ili akamlipe, kufika huko akampigia kelele za mwizi, Frank akawa ameuawa.
Nilisikitika Sana baada ya kusoma habari hiyo, majuzi nami nikapigiwa simu na mtu ninayemdai sh 900,000 ,yupo Mwanza, mimi nipo Geita ,akadai atanitumia nauli ili niende Mwanza, na pia anipangishie Guest house na kesho yake anilipe.
Nilijiuliza maswali mengi sana, Kwa nini hadi niende Mwanza? Kwa nini asinirushie tu Kwa m pesa?
Niliogopa kwenda Mwanza, ila sikumwambia Kama naogopa kwenda.
Niliogopa Kwa Sababu alikuwa ameonyesha dalili za kunidhulumu kabisa.
Baadae nilimwambia anirushie nauli, akawa ametuma.
Kesho yake nilianza safari kwenda Mwanza, nikiwa ndani ya basi, taa ya tahadhari iliwaka kichwani mwangu baada ya kukumbuka tukio la marehemu Frank, nilihisi na mimi huu ulikuwa ni mtego wangu.
Nikaamua kuchukua tahadhari ya hali ya juu Sana.
Baada ya kufika Mwanza nilimpigia simu mdeni wangu, akaniuliza mahali nilipo, nikamwambia anielekeze tu Guest house aliyonichukulia nami ningeonana naye pale maana nilikuwa bado na mizunguko mingi.
Alinielekeza hiyo guest house, ipo maeneo ya mtaa wa Rufiji mjini kabisa, kisha nikamwambia nitakuwa hapo kuanzia saa 4 usiku.
Kabla ya saa 4 usiku kufika, saa moja na nusu usiku niliwasili kwenye hiyo guest house na kumkuta dada mmoja hivi muhudumu, nilipojitambulisha tu akanionyesha chumba, sikuingia ndani ya chumba, nilimwomba Yule dada Niongee naye, alipokubali nikamweleza kuwa simwamini huyu mtu aliyenichukulia chumba, nilimweleza Kwa kina akaridhika, akaniambia vp awataarifu police?
Nikamwambia asubiri kwanza Hadi tujiridhishe.
Niliondoka na kwenda kula, nikarudi saa 3,kisha Nikamwomba yule dada nikae kwenye chumba chake ili nijue kinachoendelea, yule dada aligoma, nikaamua kumnunulia bia, na sote tukawa tunakunywa.
Ilipotimia saa 3:30 usiku ule, mdeni wangu alinipigia simu akaniuliza Kama nipo tayari kwenye hiyo guest house, nikamjibu kuwa nipo njiani naelekea huko na nikifika nampigia.
Yule muhudumu alikubali kunihifadhi Kwa muda kwenye chumba chake, ili yeye aangalie kinachoendelea.
Saa 4:30 usiku ule mdeni wangu alinipigia simu na kusema kuwa angekuja saa 5 usiku pale guest ili aniachie pesa kidogo na kesho anilipe kabisa, nikamjibu kuwa angenikuta tu.
Na kweli mida ya saa 5 usiku ule, wanaume wawili wa miraba minne walifika pale kwenye ile guest house kuniulizia, niliwachungulia kupitia tundu la funguo cha ajabu mdeni wangu hakuwepo.
Yule muhudumu aliwajibu kuwa sijafika bado Kama vipi warudi baadae.
Wakati wanaondoka aliwafuatilia na kuwaona wakiingia kwenye gari ndogo nyeupe yenye vioo vyeusi.
Wanajamvi baada ya hapo, saa 6 usiku walirudi tena na yule dada akawajibu kuwa sijarudi, mdeni wangu akanipigia simu kuniulizia nilipo sikupokea.
Waliondoka huku wakifyonza, niliogopa kutoka nje, nikalala ndani ya chumba cha yule dada hadi saa 12 alfajiri nikaondoka.
Maswali ya kujiuliza, wale watu walikuwa ni kina nani? na Kwa nini mdeni wangu hakutokea?
Nilimpigia simu na kumwambia kuwa nilibaini njama zake za kunidhuru au kuniua hakujibu kitu akazima simu Kwa aibu hadi leo.
Kama siyo JF na ile makala ya marehemu Frank, ningeingia mkenge na kuuawa, Asante Sana jamiiforums, Wanajamvi tujifunze kutokuamini wanadamu, nimepata Somo kubwa sana.
Dah..ulimgonga huyo dada? Nauliza tu
 
Wewe ulikosea, ulitakiwa kutoa pesa kidogo uchukue polisi wenye silaha wao ndio wangeingia kwenye hicho chumba. Wale jamaa mabaunsa wangeenda kueleza polisi walikuwa wanakuulizia kwa dhumuni gani? Wanakujua?
Mkuu, tukio lote lilitokea nikiwa ktk hali ya kujiridhisha kwanza Kama nilikuwa nimetegwa au la.....na baada ya kujiridhisha niliogopa kabisa kutoka nje hadi kunakucha nilikuwa ndani ya chumba cha muhudumu.
 
Mchukulie hatua vinginevyo ataona umemuogopa. Pia ingekuwa safe kwako kutoa taarifa ili usjedhurika. Na pia ajue taarifa ziko police.
 
Mambo yakukopeshana siku izi bado yapo!!😉😉😉 Nakushauri uende police uripoti hilo tukio jamaa hakawiii kuja huko ulipo!
 
Mkuu, tukio lote lilitokea nikiwa ktk hali ya kujiridhisha kwanza Kama nilikuwa nimetegwa au la.....na baada ya kujiridhisha niliogopa kabisa kutoka nje hadi kunakucha nilikuwa ndani ya chumba cha muhudumu.

Mkuu hamu ya kumgonga unadhani ingetokea wapi?
Tulilala Kama mtu na dada yake hadi alfajiri, sote tukiwa na nguo, tena mzungu Wa nne.
Hata wangelala sanjari hamu itoke wapi
 
UMEFANYA MAKOSA HUKUREPORT POLICE ,ULITAKIWA UWEKWE MTEGO WA KUWAKAMATA HAO MAJAMBAZI
 
Ubinadamu kazi kukopa kwa watu huwa rahisi na mtu anakuja na shida zake akiwa anatia huruma
Tatizo linakuja kwenye kulipa ndo kasheshe hadi ugomvi
 
pesa imewatoka imani watu wengi sana kwa sasa na kupelekea kuwa makatili wa kutupwa wasio na hofu ya Mungu
 
Aisee pole sana!, huo ni ushindi shetani kaaibika nenda kanisani katoe shukrani alafu uendelee kumwamini Mungu tu na malaika zake, binadamu ishi nae kwa tahadhali tu
 
Back
Top Bottom